Kwa mujibu wa macho ya mashuhuda, Snura alisisitiza kuwa, ana siri nzito za Wema na siku akiamua kuzianika, basi mrembo huyo hatakatiza mitaani kwa aibu.
Kwa maneno ya Snura, kila aliyetazama kipindi kile alisema hata kama mcheza filamu huyo hakuzitaja moja kwa moja siri za mwenzake, lakini kila mtu anajua Wema anatembea na aibu yake.
“Sasa kama Snura hakutaka kuzitaja hizo siri, kusema vile tu si tayari ameshamuumbua mwenzake, kila mtu anajua Wema ana mambo mabaya,” alisema Nice, mdada anayemiliki saluni moja iliyopo Kijitonyama, Dar.
Kama hiyo haitoshi, tayari Snura yupo kwenye mchakato wa kuandaa filamu inayoitwa Uozo wa Super Star ambayo ndani yake ni Wema mwanzo mwisho. Filamu hiyo inaandaliwa na Kampuni ya Chuz Entertainment ya Tuesday Kihangala ‘Chuz’.
Habari nyingine zinadai kuwa mara baada ya kumwagana na Wema, Snura kwa sasa amejipeleka kwa Chuz ambako ameigiza baadhi ya ‘sini’ kwenye Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu ambayo inaingia mtaani hivi karibuni.
WEMA AMTAHADHARISHA SNURA
Wakati Snura akiwa na mengi ya moyoni, kwa upande wake, Wema alitoa msemo wa Wahenga akimwambia Snura, Kimya Kingi Kina Mshindo.
Alimtaka Snura anyamaze na afute nia yake kwani yeye akianza kuzungumza ya kwake anaamini Snura hataweza hata kutembea mitaani.
“Nayasikia mengi sana anayozungumza Snura lakini mi ni muungwana, asinione nipo kimya. Nikiamua kufunguka sitaweza kusikia la mnadi swala wala la muadhini.
“Hakuna mtu asiyejua kama mimi ndiye nilikuwa naendesha maisha yake kama mke wangu. Kila nguo nzuri anayoivaa kwa sasa au pochi anayobeba ni fedha zangu. Namuomba kabisa asinichokonoe,” alisema Wema.
Akaongeza: Nimeshamlipia kodi ya nyumba Snura, nimeshamsaidia kulipa ada ya mtoto wake, sasa ni kwa nini asiniheshimu?”