INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

R.I.P STEVEN KANUMBA

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjxtbLjQ52zxhUpIRxNzqcLwzu5iZf6X7huMYHLtpxZyHAM6bKcIp-0ZKa6J0cW9pp4fv9TLFyvmX2picNM7Y7onyGpUHTcGAsQb64f15I1C6GDW-Aa0iNtfDmPeqbYh26sbqSwD_zb7C0N/s1600/Steve+Kanumba.jpg

HISTORIA YAKE:

Steven Charles Kanumbaa alizaliwa Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga kabla ya umauti kumfiia Aprili 6, mwaka 2012.

Elimu ya msingi alipata katika shule ya Bugoyi, na baadaye akajiunga na sekondari ya Mwadui, kabla ya kuhamia Dar Christian Seminary.

Baada ya kumaliza Kidato cha Nne Dar Christian, Kanumba alijiunga na sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam pia kwa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.

Ni ni wakati huo akiwa Jitegemee Kanumba alianza shughuli za sanaa katika Kundi la Kaole Sanaa Group la Magomeni, Dar es Salaam.

Baada ya kukomaa Kaole, Kanumba aliamua kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya filamu na hadi anakutwa na umauti alikuwa mwigizaji anayefahamika Afrika nzima.

Ameshirikiana na wasanii wakubwa duniani kama Ramsey Nouah wa Nigeria na amefanya kazi na mastaa wengine kadhaa wa Nigeria.

Miongoni mwa filamu ambazo alifanya ni Dar To Lagos, She is My Sister, Ancle JJ, Oprah, Tufani, Johari, Gharika, Baragumu, Sikitiko Langu, Dangerous Desire, Cross My Sin, Village Pastor, Family Tears na kadhalika.

Hivi karibuni, alikaririwa akisema atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi.

Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasniya ya filamu Tanzania. Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.

Nigeria sasa wanajua Tanzania sasa filamu. Nchi nyingi za Afrika zinajua sasa nah ii sehemu ya kazi nzuri kwa Kanumba.

Mwenyewe aliwahi kukaririwa alifika hadi Hollywood hadi Marekani, ambayo ni ‘makka’ ya wacheza filamu. Kwa sasa mwili wa marehemu upo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.

Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.




STEVEN KANUMBA AFARIKI DUNIA 

Muigizaji wa filamu nchini Stephen Kanumba amefariki usiku wa kuamkia leo,baada ya ugomvi na mpenzi wake huko nyumbani kwake Sinza Vatican.Mpenzi huyo ametoroka na inadaiwa alimsukuma marehemu kwa nyuma na kudondokea kisogo.Kanumba alilalamika maumivu makali ya kichwa ambapo alimwuita mdogo wake ampeleke hospitali,lakini alifariki kabla hajafika huko.Mwili wake umehifadhiwa Muhimbili.Source: Radio One
 Mkurugenzi wa Global Publisher, Erick Shigongo akishirikiana na watengenezaji wa hema.
 Ndani ya geti la marehemu Steven Kanumba


Blogger Rulea Sanga aliyevalia njano halkukosa msibani

H-BABA akihojiwa na waandishi wa habari
Wapenzi na ndugu wa marehemu Steven Kanumba nyumbani kwake
Mwigizaji Mainda wa pili kutoka kushoto akimfariji rafiki yake
Waigizaji wa filamu
Mwimbaji huyu alielezea jinsi alivyoaagana na Marehemu Steve Kanuba alipohudhuria katika bendi yake siku ya jana usiku, anasema  marehemu alimtania kuwa kesho ambayo ni leo kuwa atakuja na suti kali sana ambayo ameinunua katika bendi yake
Mjasiliamali Shigongo wa Global Publisher akihojiwa na waandishi wa habari, alisema ni kitu chema kufanya kazi yako kwa kumkumbuka Mungu
Ruge wa Clouds FM alisema, ni pengo kubwa sana kwani katika sanaa alikuwa anahitajika sana

--------------------------

MH. RAIS JK KIKWETE ATUMA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898

E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com au press@ikulu.go.tz

Fax: 255-22-2113425

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania –TAFF- kuomboleza kifo cha msanii maarufu nchini Steven Charles Kanumba, aliyeaga dunia usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, Aprili 7, 2012. Katika salamu hizo, Rais Kikwete amemwomba kiongozi huyo wa TAFF kufikisha salamu za rambirambi za dhati ya moyo wake kwa wana-familia ya Kanumba na kwa wasaani wote nchini ambao wamepotelewa na mdau na Rais Kikwete amesema kuwa ameshtushwa na kuzunishwa na kifo cha msanii huyo ambaye amemwelezea kuwa msanii mahiri na mwenye kipaji kikubwa ambaye katika uhai wa maisha yake mafupi na akiwa bado kijana sana amechangia kwa kiwango kikubwa maendeleo ya sanaa ya filamu nchini na kupitia sanaa hiyo kuitangaza Tanzania kimataifa. Amesema Rais: ”Nimepokea kwa mshtuko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Ndugu Steven Charles Kanumba. Kupitia filamu zake, ameburudisha na kuelimisha jamii yetu kwa namna ambayo haiwezi kupimika. Alikuwa msanii mahiri na mwenye kipaji kikubwa ambaye mchango wake mkubwa katika kuanzisha, kukuza na kuimarisha sanaa ya filamu nchini hautasahaulika.” Ameongeza Rais Kikwete: “Ndugu Kanumba pia ametoa mchango mkubwa katika kuitangaza nchi yetu ya Tanzania mbele ya mataifa mengine kupitia sanaa ya filamu na uwezo mkubwa wa kisanii. Tutaendelea kumkumbuka
kwa mchango wake huo kwa nchi yetu.”  “Nakutumia wewe Rais wa TAFF salamu zangu za rambirambi na kupitia kwako kwa wasanii wote wa filamu na sanaa nyingine kufuatia msiba huu
mkubwa kwa fani yetu ya sanaa. Aidha, naomba unifikishie salamu za dhati ya moyo wangu kwa wanafamilia wote. Wajulishe kuwa niko nao katika msiba huu mkubwa. Waambie naelewa machungu yao katika kipindi hiki kigumu cha msiba,” amesema Rais Kikwete na kuongeza: “Namwomba Mwenyezi Mungu awape subira na nguvu za kuweza kuhimili kipindi hiki kigumu kwa sababu yote mapenzi yake. Aidha, naungana na wana-familia na wasanii wote nchini kuwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke pema peponi roho ya Marehemu Steven Charles Kanumba. Amen.”

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Dar es Salaam.

07 Aprili, 2012


_________________________________________________________

ELIZABETH MICHAEL AU “LULU” ANAYESHIKILIWA NA POLISI KUHUSIANA NA KIFO CHA STEVEN KANUMBA


Sambamba na jina lililotawala vinywani na akilini mwa watu wengi hivi leo, jina lingine ni la Elizabeth Michael au maarufu kama Lulu ambaye kama ilivyokuwa kwa Marehemu Steven Kanumba, naye pia ni muigizaji wa filamu nchini Tanzania(Bongo Movies).



Tunaamini kwamba Jeshi la Polisi litaweka hadharani taarifa kamili juu ya uchunguzi wao. Tuendelee kumuombea Steven Kanumba apumzike kwa Amani.Amina.



_____________________________________________________

MWILI WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA KABLA YA KUINGIZWA MOCHWARI
Hii ndiyo sura ya ndugu yetu Steven Kanumba, mara baada ya kufikishwa hospitalini

MARAFIKI NA NDUGU WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA NYUMBANI KWAKE SINZA VATICAN
 Nyumbani kwa marehemu
 MC Nova

 Ndani ya geti-nyumbani kwa marehemu

 Steve Nyerere aliyevalia Polo shirt ya mistari mweusi na mweusi

 Mwigizaji a.k.a Chopa Mchopanga (katikati)
 Msanii wa Bongo Flava, Noora wa tatu kutoka kushoto

 Mvua akinyesha, alkini watu bado wako msibani
 Gari la Marehemu Steven Kanumba
 Mwigizaji wa Bongo Movie aliyekuwa muongozaji wa magari na kutoa tahadhari kwa wapenzi wa marehemu
 Dogo akipigwa mvua kali

 Mjasiliamali, Dotnata aliyenyoosha mkono wake wa kulia akipigwa mvua msibani
 Mwigizaji a.k.a Judy akihojiwa Live Channel Five
 Watu hawaamini kifo cha Kanumba (jembe)
 Mwigizaji Johari akilia katika mahojiano na EATV
 Mwigizaji maarufu sana, a.k.a Ray aliyevalia kofia akiwasiliana na jamaa baada ya mahojiano na waandishi wa habari
 Nyumbani kwa Steven Kanumba



Blogger na Graphic Designer, Rulea Sanga (mwenye njano) akitafuta matukio kwaajili yako wewe mdau wa blogu hii




_________________________________________________________

PICHA ALIZOPOST MAREHEMU STEVEN KANUMBA TAREHE 6 APRIL 2012, NA KIFO CHAKE KIKAMCHUKUA SAA 7 USIKU WA TAREHE 7 APRILI 2012

**********

HAPPY 5TH ANNIVERSARY TMH,SAMBAMBA NA UZINDUZI WA DUKA/OFISI & TRAINING CENTER

SEHEMU YA DUKA LA NGUO TOKA KWA DESIGNER MBALIMBALI.
TULIOSAPOTI MPAKA KITUO HIKI KUFIKIA HAPA KILIPO SOMA MAJINA HAPO JUU JINA LANGU LIPO HAPO,KUSEMA UKWELI INAPOKUJA MAMBO YA KUSAIDIA JAMII NAJITAIDI KUTOA NINACHOKUA NACHO MAANA HAPA HUKUMBUKA MANENO YA MWANDISHI ALBERT PINE..''"What we do for ourselves dies with us. What we do for others and the world remains and is immortal."
'' KANUMBA THE GREAT PIONEER MOTO WA VOLCANO'' NIKIWA KTK OFISI ZA TANZANIA MITINDO HOUSE.

Tembelea blogu yake: www.kanumbathegreat.blogspot.com

__________________________________________________

MAMA WA KANUMBA CHINI YA UANGALIZI WA DAKTARI
Kanumba
MAMA wa marehemu Steven Kanumba, ameanza kusumbuliwa na presha kiasi cha kulazimika kuwa chini ya uangalizi wa daktari.

Dk. Nassor Matuzya kutoka hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam ambaye amewahi kuwa Dakatri wa klabu ya Yanga, enzi za kocha Mserbia, Profesa Dusan Savo Kondic ameiambia bongostaz joni hii kwamba yupo kwa ajili ya kufuatilia hali ya Mama Kanumba.

“Mama anasumbuliwa na presha, inapanda sana, lakini namtibu na kwa sasa anaendelea vizuri,”alisema Dk. Matuzya.

Matuzya alisema Mama Kanumba leo usiku atapelekwa hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam kuuona mwili wa mwanawe kabla ya kuagwa na mazishi kesho.

Mama huyo aliyewasili jana kutokea Bukoba, ameridhia mwanawe azikwe Dar es Salaam, ingawa baba wa msanii huyo alipenda kijana wake azikwe karibu na kaburi la babu yake, Mzee Kanumba huko Shinyanga.

Wakati huo huo: Mwanamitindo Millenne Happiness Magesse ameongezwa kwenye kamati ya Mazishi. Millene ameonekana tangu jana akiwajibika ipasavyo kwenye msiba huo.

Kanumba ataagwa kesho kuanzia saa nne asubuhi, viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar es Salaam na kuzikwa kwenye makaburi ya Kinondoni.

Wakati huo huo: Watu wameendelea kumiminika nyumbani kwa marehemu Sinza Vatican kutoa rambirambi na miongoni mwao ni aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Yanga, Wakili Imani Omar Madega.

Madega alifika kutoa salamu zake za rambirambi na ubani kisha kuungana na waombolezaji wengine. Mwanamuziki mkongwe, Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’ naye alifika. Chanzo;mama pipiro blog


_______________________________________________________

FIRST LADY MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA MSIBA WA KANUMBA LEO

LEO IKIWA NI SIKU YA TATU YA MSIBA WA KANUMBA, WAMESHAKUJA VIONGOZI KIBAO, NA LEO JIONI TULIKUWA NA MKE WA PREZIDAR MAMAA SALMA, AMBAPO ALIKUJA TOA MKONO WA POLE KWA WAFIWA 

 MSISITIZO::
KESHO YATUPASA TUWAHI MAPEMA LEADERS CLUB KWANI SAA 4 SHARP SHUGHULI ZINAANZA , KUTAKUWA NA PERFOMANCE ZA LIVE TOKA KWA WANAMUZIKI WALIOTOA SINGLE MAALUM KWA MAREHEMU STEVEN KANUMBA, KUTAKUWA NA MISA NA KUMUAGA MAREHEMU NA KISHA MAREHEMU ATAZIKWA MAKABURI YA KINONDONI KWENYE SAA KUMI N KWA MUJIBU WA RATIBA

R.I.P KANUMBA
BAADA YA KUSAINI KITABU
ALIENDA MPA POLE MAMA MZAZI WA STEVE KANUMBA
WAOMBOLEZAJI NI WAKO WAKUTOSHA FAMILIA ,NDUGU NA MASHABIKI WA KANUMBA


________________________________________________

RAISI JAKAYA KIKWETE AWAFARIJI WAFIWA WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili nyumbani kwa marehemu Steven Charles Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam April 8, 2012 kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa wafiwa na kupeana mkonon na mdogo wake Kanumba.

Rais Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Steven Charles Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam April 8, 2012 kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa wafiwa.

Rais Kikwete akiwafariji wafiwa  nyumbani kwa marehemu Steven Charles Kanumba Sinza 'Vatican' jijini Dar es salaam April 8, 2012 alikofika kuomboleza nao kifo hicho.PICHA ZOTE NA FREDDY MARO WA IKULU


_____________________________________________________


STEVEN KANUMBA AANDIKA HISTORIA NYINGINE BAADA YA BABA WA TAIFA

Watanzania hii leo wameweza kumuaga kwa heshima mwigizaji nyota marehemu Steven Kanumba katika ibada iliyofanyika kwenye viwanja vya Leaders club Kinondoni jijini Dar es salaam,na kuhudhuriwa na Makamu waRais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mh.Dkt Gharib Bilal,mke wa Rais mama Salma Kikwete na viongozi wengine pamoja na familia ya marehemu,waigizaji wenzake pamoja na wanakwaya wa kwaya ya Neema gospel (NGC)kutoka AIC Chang'ombe alikokuwa muumini na mwanakwaya wa kwaya hiyo.

Umati mkubwa ambao ulikusanyika katika eneo la Leaders club kisha makaburi ya Kinondoni umeweka historia kwajinsi msanii huyo alivyokubalika katika jamii ya Watanzania,mpaka sasa akiwa ameshika nafasi ya pili kupata watu wengi,nafasi ya kwanza ikiwa ni msiba wa Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye mwili wake ulitolewa heshima za mwisho kwenye uwanja wa zamani wa Taifa jijini Dar es salaam.
Sehemu ambayo ilikuwa ikiandaliwa kuwekwa jeneza lenye mwili wa Kanumba.

Hemed pamoja na Yusuph ambao ni waigizaji wakiingia Leaders asubuhi ya leo kumuaga mwenzao.

Watoto ambao waliigiza na Kanumba wakiwa wanaingia viwanjani hapo asubuhi ya leo.

Mama wa marehemu Steven Kanumba akiwapungia maelfu ya watu asubuhi ya leo kuonyesha shukrani kwa kujitokeza kumuaga mwanae.


Viongozi wa serikali wakiwa wamekaa kwenye jukwaa maalumu.


Kijana Samuel Limbu akiwaongoza wenzake wa Neema gospel Choir kuimba viwanja vya Leaders club.

Wasanii wakiliingiza jeneza la mwenzao viwanja vya Leaders Kinondoni.

Wasanii wakipeleka jukwaani jeneza lenye mwili wa Steven Kanumba.

Waigizaji wakishusha jeneza la mwenzao taratibu jukwaani.

Jukwaa kuu kwaya ya Neema Gospel Chang'ombe wakiimba kumsindikiza mwimbaji mwenzao.


Kuna watu walishindwa kuhimili hisia zao kwa marehemu nakujikuta wakizimia,msalaba mwekundu wakitoa huduma.

Makamu wa Rais Dkt.Gharib Bilal akitoa heshima zake za mwisho.

Mke wa Rais mama Salma Kikwete akitoa heshima zake za mwisho.


Baadhi ya umati wa watu uliokuwepo asubuhi ya leo viwanja vya Leaders club Kinondoni.

Mh.Bernard Membe akitoa heshima zake za mwisho.

Kamanda wa polis mkoa wa Dar es salaam Kova akitoa heshima zake za mwisho.

Wanahabari wakihakikisha hawapitwi na jambo.

KUTOKA MAKABURI YA KINONDONI NAKO HUKO MAELFU YA WATU WALIKUSANYIKA ILI KUSHUHUDIA MAZISHI YAKE,AMBAPO POLISI WALIKUWA NA KAZI YA ZIADA KATIKA ULINZI,AMBAPO PIA TAARIFA ZINASEMA KUNA WATU WAMEJERUHIWA BAADA YA KUANGUKA KUFUATIA TAWI WALILOKALIA KUKATIKA.















___________________________________________________

........BABA WA KANUMBA ASHINDWA KUHUDHURIA MAZISHI YA MWANAE.......SHIBUDA AMWAKILISHA.......
MBUNGE wa Maswa Magharibi, John Shibuda jana alimwakilisha baba wa msanii maarufu wa filamu nchini marehemu Steven Kanumba katika mazishi ya msanii huyo akidai kuwa baba huyo Charles Kusekwa Kanumba ameshindwa kuhudhuria mazishi hayo kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya malaria na shinikizo la damu na si matatizo yake na merehemu huyo. Kupitia uwakilishi huo, Shibuda pia alisoma barua aliyoeleza kutoka kwa mzazi huyo wa Steven Kanumba akieleza kushindwa kwake kufika kwenye mazishi hayo na kwamba ametuma watoto wake na wakwe zake kumwakilisha. "Baba yake Kanumba siku ya Jumamosi alikuwa anajisikia vibaya na alipokwenda hospitali alipimwa na kukutwa ana malaria 15 na shinikizo la damu likiwa 180 - 140. Lakini pia ana matatizo ya miguu kwa muda mrefu, anatembea kwa msaada wa baiskel,"alisema Shibuda. Akisoma barua hiyo Shibuda alinukuu barua ya baba wa Kanumba akisema:"Salam, nashukuru wana kamati ya mazishi ya mwanangu kwa kunitumia nauli ili niweze kuja kumzika mtoto wangu. Lakini kutokana na maradhi yanayonikabili sitaweza kuja, ila nawatuma wanangu Michael na Mjanael, pia mkwe wangu Chrisant Msipi waniwakilishe. Matatizo yangu na mwanangu yalishakwisha." "Msianze kuleta maneno yenu ya umbea umbea na uzushi eti hajafika kwenye msiba wa mwanawe kwa kuwa hawaelewani huo ni uzushi, walishaelewana na alikuwa na mawasiliano mazuri na mke wake mama Kanumba na ndiyo maana akatuma wawakilishi wake,"alisema Shibuda.


____________________________________________________


HATIMAYE ELIZABETH MICHAEL AKA LULU APANDISHWA KIZIMBANI LEO KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA KANUMBA


Muigizaji wa Filamu nchini anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie,Marehemu Steven Kanumba,Bi Elizabeth Michael a.k.a Lulu amepandishwa kizimbani mapema leo asubuhi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa kusomewa mashtaka yake kuhusiana na kuhusika kwa kifo cha Muigizaji huyo nguli hapa nchini.

Elizabeth Michael amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ya mauaji ya Muigizaji wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba yaliyotokea huko sinza vatcan jijini Dar es Salaam april 7 mwaka huu.

Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo kwani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena april 23 mwaka huu.

Muigizaji huyo aliletwa mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi kama mshale na kwa ulinzi mkali na pia ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba hakuna hata mwandishi alieweza kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye tuhuma za mauaji Na kupandishwa katika gari ndogo nyeupe aina ya suzuki grand vitara yenye nambari za usajiri T 848 BNV huku kwenye kioo nambari zake zikisomeka PT 2565.Credits Michuzi Blog


________________________________________________________


NDUGU YETU PUMZIKA KWA AMANI STEVEN KANUMBA THE GREAT














 Ni majonzi makubwa sana kwa Watanzania wote sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi, inauma sana kwa kijana mdogo kama Kanumba kufariki wakati alikuwa bado hajazitima ndoto zake .Mungu ailaze roho ya marehemu Swaiba wangu Steven Kanumba ni mengi sana tuliyoyafanya mimi na wewe katika gurudumu ili la sanaa bila kujali yote yaliyotokea ni kawaida ya binadamu kutoelewana kama Baba na Mama wanafunga ndoa kanisani na wanakula viapo vya utii mbele za Mungu lakini wanagombana na kufikia hatua ya kuachana kwanini ishindikane kwetu ni hali ya kwaida katika maisha binadamu kutofautiana mengi yanazungumzwa juu yangu ila kila kitu mimi namuachia Mungu mimi ni mnyonge siwezi kupambana nanyi mnaoniongelea vibaya maumivu nayoyapata juu yenu Mungu hatowaacha siwezi kuzizuia hisia zenu kuzungumza yale mnayojisikia kuzungumza

 Muda mfupi tu baada ya kufariki Steven Kanumba akiwa kwenye gari lake la kifahari Lexus tangulia ndugu yangu sisi tuko nyuma yako maana kila nafsi itaonja umauti. wadau nilikuwa kimya kwa kutowaletea matukio  kwa sababu ya shughuli zilkuwa nyingi sana katika msiba nilikuwa kwenye kamati ya mazishi hivyo sikuwa nakipata muda wa kutosha na sio watu wanavyofikiria jamani hata kama kuna matatizo ndio katika maswala ya msiba hapana jamani mimi sijafikia hali hiyo  yakuwa na roho ya kinyama namna hiyo

 Hapa tukiutelemsha mwili wa marehemu katika hospital ya Muhimbili ni mtu wa kwanza kufika katika eneo la tukio















 Safari yetu ya mwisho binadamu wote mara ya kwanza nilipofika  walikataa kumpokea pale hospital mpaka wapate PF 3 ndipo nilipowasha gari na kwenda Salenda polisi na kuwapata askari watatu  ndipo tukapata fursa ya kwenda kumpuzisha marehemu

 Tukimfunika macho maana yalikuwa wazi kama anasinzia















 Hapa akiongea jambo na baadhi ya wanakamati ya mazishi













 The Greatest nikimsikiliza Rais













 Mwenyekiti wa Bongo Movie Jb akiteta jambo na Mueshimiwa Rais














 Baada ya kuondoka Rais tukawa tunateta jambo ambalo lilimchekesha sana mtoto wa Rais Riz One Kkikwete

 The Greatest nikiwa katika maojian na mwandishi wa habari













Salama Jabir na Madam Ritha wakiwa kwenye majonzi 

Dulla wa Planet Bongo na Salama 
Jabir



_______________________________________________________

MCHAWI ADONODOKA NA UNGO JUZI KWENYE MSIBA WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA NYUMBANI KWAKE SINZA..


_______________________________________
LUCRECIA KALUGILA (MAMA LULU) ASEMA ACHENI UMUHUKUMU MWANAE





Mama mzazi wa msanii wa filamu anayehusishwa na kifo cha nyota wa filamu nchini Tanzania, Steven Kanumba (28), Elizabeth Michael 'Lulu' amesema, jamii isimuhukumu mwanawe kuwa amemuua ' Kanumba The Great'

Lucrecia Kalugila amesema, wakati Kanumba na Lulu(18) wakiwa wanagombana chumbani, walikuwa wawili tu, hivyo hakuna mwingine anayefahamu kilichotokea hivyo watu wasimuhukumu mwanawe kuwa kamuua Kanumba.

Mama huyo amesema, Kanumba ni mwanawe, na kwamba, hata yeye kifo cha msanii huyo kimemsikitisha na kwamba, kama Kanumba angekuwa hai leo, angesema namna walivyokuwa wanashirikiana.

Ametaka watu waache kuegemea upande mmoja kwenye tuhuma zinazomkabili Lulu, wasubiri sheria ichukue mkondo wake.

Amempa pole mama Kanumba, na kumshauri asiyafuate yanayosemwa mitaani kuhusu kifo cha Kanumba.

Mama Lulu amewaomba wanasheria wajitokeze kumtetea binti yake ili haki itendeke.

Lulu yupo rumande tangu Jumamosi, akihusishwa na kifo cha Kanumba, na kwa mujibu wa Polisi, atapandishwa kizimbani kujibu mashitaka ya mauaji.

KWA MUJIBU WA MDOGO WA MAREHEMU, SETI, LULU ALIKWENDA NYUMBANI KWA KANUMBA KUKAWA NA UGOMVI, WAKAINGIA CHUMBANI.

WAKATI WAKIWA HUKO, BAADA YA MUDA, LULU ALITOKA NA KUMUITA YEYE KUMUAMBIA KANUMBA KAANGUKA.

ALIPOENDA AKAMKUTA Kanumba KAANGUKA, AKAENDA kumuita DAKTARI WA KANUMBA ALIPORUDI HAKUMKUTA LULU.

Inadaiwa kwamba, Lulu aligombana na Kanumba ambaye inasemekana alikuwa mpenzi wake baada ya kukutwa akiongea na mwanaume mwingine, kwenye simu.

Hivi karibuni Lulu alinukuliwa katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa East Africa TV 'EATV' akisema, hana MPENZI, na aliapia kiislamu kuthibitisha kauli yake.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyella alinukuliwa akisema, Kanumba alikuwa katika `ugomvi’ na LULU ambaye inasemekana kuwa alikuwa mpenzi wake.

-----------------------------------------------------------------------------

KANUMBA NA FREEMASONRY: MASWALI HAYA YANAWEZA KABISA KUTOA MAJIBU


PART II
KUHUSU KANUMBA KUNA MENGI YAMEZUKA KUWA ALIKUWA FREEMASON AU LA?
Mambo yafuatayo yanaweza kutusaidia kuamua bila maswali yoyote kuwa Steven Kanumba alikuwa Freemason ama la?

  1. Alama za Freemasons- Hapa ndio panaweza kutupa jibu kuwa Steven Kanumba au alikuwa kipenda kujiita Kanumba “THE GREAT”, alikuwa wa kipnda hicho ama la! 
  2. Mazishi ya wanachama wa Kundi la Freemasons huwa yanakuwaje?- pia hapa panweza kutufumbua macho kujua uhalisia wa Kanumba na Freemasons kwa kuyachunguza mazishi yake yalivyokwenda.
  3. Sanduku/Jeneza lililioubeba mwili wa Mwigizaji nguli wa Tanzania katika Bongo Movies Steven Kanumba- linaweza kutupa ushahidi wa kutosha bila chenga.
Source: jaizmelaleo.blogspot.com/

_____________________________________________

VICENT KIGOSI (RAY) THE GREATEST AMPA POLE MAMA WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA (THE GREAT) NA KUONYESHA JINSI ALIVYOJISHUGHULISHA KATIKA SUALA LA KUMUWEKA MAHALI PA KUMPUMZIKA MILELE RAFIKI YAKE
 Muda ulifika wa Mama Kanumba kuwasili uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere maana wakati mauti yanamfika mwanae alikuwa safarini Bukoba.Mama yangu mzazi(mwenye nguo nyeupe) ndiye aliyeongoza msafara wa kwenda kumpokea Mama Kanumba

 Kamati ya mapokezi ikimsubiri Mama Kanumba kuwasili.

 Muda ulifika na Mama akawasili na majonzi yakatawala.

Kilio na simanzi vilitawala uwanjani hapo(kulia) ndiye Mama yangu mzazi, Mama Mary Kigosi akimsaidia rafiki yake.

 Pole sana Mama kwa msiba mkubwa uliokupata ninakuwaidi nitakuwa pamoja nawe kwenye shida na raha

Mama alishindwa kabisa kuzuia hisia zake mpaka kuzimia.
 
 Njiani kuelekea msibani.

 Tukimsubiri Mama mzazi wa Marehemu Kanumba.

Baada ya kufika nikaenda kumpa pole,alilia sana aliponiona na kuniambia pacha wako mwanangu yuko wapi umebaki peke yako? Niliumia sana.

 Mazungumzo yakaendelea.

Akia kwa uchungu mkubwa sana. Pole mama.

 Kesho yake nikaenda kutafuta jeneza la kumzikia ndugu yetu mpendwa.

Hili ndilo jeneza aliozikiwa Marehemu Steven Kanumba.

 Baada ya kutoka kwenye majeneza nikaenda kuwachukua maskali kwa ajili ya postmortem

 Tukiendelea kusubiria.

Nikiwa nimeshamaliza hatua zote.

No comments:

Post a Comment