ODAMA NDANI YA HOT MIX-EAST AFRICA
Msanii wa filamu Tanzania Jeniffer Kyaka a.k.a ODAMA wiki iliyopita
alifanyiwa mahojiano na EATV kuhusiana na filamu yake mpya ya RUDE
inayofanya vizuri sokoni kwa sasa. Mbali na hivyo alielezea maisha yake
kwa ujumla na jinsi alivyofaidika na kazi ya filamu.
Kutoka
kushoto ni mtangazaji wa Hot Mix, Anna Mbanjo, akifuatiwa na msanii wa
filamu, Jeniffer Kyaka (Odama) na Fatna Ramole wa Hot Mix wakiwa katika
studio za EATV
Jennifer Kyaka mbali na uingizaji pia ni Mkurugenzi wa kampuni yake ya
J-FILM 4 LIFE iliyoko Biafra Kinondoni Dar es Salaam. Aliongeza kwa
kusema mbali na kucheza filamu za watu wengine na pia ametengeneza
filamu katika kampuni yake ya J-FILM 4 LIFE kama The Avenger, Life 2
Life, All About Love, Loreen, RUDE na filamu mpya nyingine ambayo
inakuja karibuni inayoenda kwa jina la HOUSE MAID .
Odama akiwa katika pozi baada ya kufanya interview
Odama alimaliza kwa kuwashukuru wapenzi wake wanaom-support kwa kununua filamu zake, na hasa wanaotembelea blogu yake ( www.odama1.blogspot.com) ambayo imekuwa gumzo kubwa kwa kukusanya matukio ya wasanii wa filamu Tanzania na nje ya nchi.
Wakitokelezea ndani ya EATV
Posted: 11 June 2012
No comments:
Post a Comment