INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, January 26, 2015

ODAMA ASHINDA SHINDANO MSANII BORA KATIKA KIPINDI CHA FILAMU ZETU - REDIO UHURU 95.7 FM

Siku ya leo mwigizaji wa filamu Tanzania na mkurugenzai wa J-Film 4 Life, Jeniffer Kyaka (Odama) aliweza kupata mualiko wa kufika katika redio wa UHURU iliyopo maeneo ya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam Tanzania kufanya mahojiano juu ya ushindi alioupata katika kipindi cha Filamu Zetu kinachoendeshwa na mtangazaji wa redio hiyo Mama Abdul.

Kipindi hicho kilikuwa kinapambanisha waigizaji bora Tanzania ambapo Odama alipambanishwa na mwigizaji mwenzake Irene Paul. Wasikilizaji wa redio Uhuru waliweza kupiga simu na wengine kutuma meseja za kupiga kura kwa yule msanii waliona ni bora kwao. Hatiamye Jeniffer Kyaka (Odama) aliweza kuchukua ushindi

Mtangazaji wa Redio Uhuru katika kipindi cha filamu Zetu Mama Abdul (kushoto) akisoma historia ya msaanii wa filamu nchini Kenya, na kulia ni Odama akifuatilia historia hiyo.

Odama alimshukuru Mungu kwa ushindi alioupata na pia kwa wale wote waliompigia kura kwa njia ya simu. Ni kitu ambacho hakutegemea kabisa kuwa ataibuka mshindi wa shindano hilo kabambe. Aliwashukuru sana watangazaji wa redio hiyo na uongozi mzima kwa kumpa heshima ya kufanya mpambano huu mkali. Radio Uhuru ni moja ya redio bora Tanzania kwa kazi za wasanii na ndio maana wameamua kuanzisha kipindi cha Filamu Zetu.

Jeniffer Kyaka (Odama) na Mama Abdul (kulia)

Wadau waliweza kuuuliza maswali juu ya malengo yake ya baadae, naye Odama aliweza kufunguka na kuwaeleza kwa sasa yuko katika maandalizi ya kufungua kituo kwaajili ya kuinua vipaji vya wasanii wadogo ili waweze kujulikana kama yeye alivyojulikana na jamii ya Tanzania

Mtangazaji wa Redio Uhuru katika kipindi cha filamu Zetu Mama Abdul (kushoto) akisoma historia ya msaanii wa filamu nchini Kenya, na kulia ni Odama akifuatilia historia hiyo.
Wengine walitaka kujua idadi ya filamu ambazo amecheza, naye alisema mpaka sasa amecheza filamu zaidi ya 20 na hivi sasa ametoa filamu mpya inayoenda kwa jina la JADA ambayo itakuwa sokoni tarehe 19.02.2015 kwahiyo wadau wakae mkao wa kula kujipatia filamu mpya. Katika filamu hiyo wataweza kuona mtoto anayeishi na mama wa kambo anavyosumbua familia na kusababisha malumbano na kuvunjika kwa amani ndani ya familia.
Mtangazaji wa Redio Uhuru katika kipindi cha filamu Zetu Mama Abdul (kushoto) akisoma historia ya msaanii wa filamu nchini Kenya, na kulia ni Odama akifuatilia historia hiyo.
 Baadhi ya wadau walitaka kujua siri kubwa ya Odama kutokuwa na skendo mbaya kama baadhi ya wasanii wenzake, naye alisema, hii ni kutokana na jinsi yeye alivyojiwekea katika maisha yake kuwa atajitahidi sana kuishi kama Jeniffer Kyaka na sio kuishi yale maisha ambayo anaigiza katika filamu. Hii imemsaidia sana Odama na ndio maana mpaka leo jamii inamtambua Odama kama mwigizaji asiye na skendo. Pia malezi aliyolelewa na wazazi wake ambayo ni wacha Mungu na hapendi kuona anawaangusha wazazi wake kwa skendo.
 Jenifer Kyaka (Odama)
Wadau waliweza kupiga maswali mengi sana na hasa juu ya waigizaji wa filamu kuvaa mavazi ya ajabu katika jamii inayowazunguka kama wanavyofanya katika filamu zao, naye Odama alisema, hiyo ni tabia ya mtu na sio kitu kingine, kama mtu amezoea tabia hiyo ataendelea kuwa hivyo. Pia aliwaomba watu wasiwachukulie wasanii kama wote wana tabia mbaya kutokana na wanavyoona katika filamu zao bali watambue ya kuwa kile wanachofanya ni kuwakilisha vitu vinavyotokea katika maisha ya watu mitaani.
 Mama Abdul (kushoto) na Jeniffer Kyaka (Odama)
 Odama
  Odama
 Odama na mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Filamu Zetu
  Odama
  Odama
 Mtangazaji wa Filamu Zetu - Redio Uhuru Mama Abdul

  Odama
  Odama
 Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Rumafrica (www.rumaafrica.blogspot.com), Mtangazaji wa Filamu Zetu Mama Abdul, Odama
 Mkurungenzi wa Rumafrica, RuleaSanga (kulia) na mtangazi wa kipindi cha nyimbo za tarabu redio Uhuru
 Mkurungenzi wa J-Film 4 Life, Odama (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa redio Uhuru, Angel A. Akilimali (kulia)
 Mkurungenzi wa J-Film 4 Life, Jeniffer Kyaka -Odama (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa redio Uhuru, Angel A. Akilimali (kulia)
 Kaimu Mkurugenzi wa redio Uhuru, Angel A. Akilimali
  Mkurungenzi wa J-Film 4 Life, Jeniffer Kyaka -Odama
  Mkurungenzi wa J-Film 4 Life, Jeniffer Kyaka -Odama
 Mkurungenzi wa J-Film 4 Life, Jeniffer Kyaka -Odama (kushoto) akikabidhiwa zawadi ya kalenda ya CCM na Kaimu Mkurugenzi wa redio Uhuru, Angel A. Akilimali (kulia)

ULIFIKA WAKATI WA KUPIGA PICHA ZA PAMOJA
Baadi ya wafanyakazi na watangazaji wa redio Uhuru waliweza kupiga picha za kumbukumbu na Odama na ilikuwa kama hivi"-

 Mtangazaji wa redio Uhuru kipindi cha Burudani Ambiance Shtuka, Cecy Jerry aka Mama Cecy au Mwasii Kitoko (kushoto) akiwa na Jeniffer Kyaka (Odama)
Mtangazaji wa redio Uhuru kipindi cha Burudani Ambiance Shtuka, Cecy Jerry aka Mama Cecy au Mwasii Kitoko (kulia) akiwa na Jeniffer Kyaka (Odama)

 Mtangazaji wa redio Uhuru Scolastica Salim (kulia) akiwa na Odama
 Mtangazaji Neema Mwangomo (kulia) na Jennifer Kyaka (Odama)
  Mtangazaji Neema Mwangomo (kulia) na Jennifer Kyaka (Odama)
 Mtangazaji wa redio Uhuru kipindi cha Hello Tanzania, Sheila Simba (kulia)  na Jennifer Kyaka (Odama)
  Mtangazaji wa redio Uhuru kipindi cha Hello Tanzania, Sheila Simba (kulia) na Jennifer Kyaka (Odama)
 Mtangazaji wa redio Uhuru, FurahaLuhuembe (kulia) na Jennifer Kyaka (Odama)
 Mtangazaji wa redio Uhuru, FurahaLuhuembe (kulia) na Jennifer Kyaka (Odama)

No comments:

Post a Comment