INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Wednesday, April 16, 2014

GRACE RWEGASHA MWENYE NDOTO ZA KUIGIZA KWA SASA AMETOA ALBAMU YAKE YA MY SAVIOUR GOD

Mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzani mwenye ndoto kubwa za kuwa mwigizaji wa filamu Tanzania ambaye kwa sasa anamtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji. Amesema anatamani sana kuigiza kwani ana kitu hiki ndani ya moyo wake kwa muda mrefu sana. Yupo tayari kufanya kazi na mtu yeyote yule ili atimize ndoto yake.

Grace akishirikiana na mdogo wake  Joshu Rwegasha wameamua sasa kumuimbia Mungu na kumtukuza ili Mungu mwenyewe ajitwalie utukufu. Waimbaji hawa ni ndugu (ni mtu na mdogo wake). Baada ya Bwana Joshu kuona ana kitu ndani yake cha kumtukuza Mungu aliamua kumjulisha dada yake Grace Christian Rwegasha kwamba anahisi kumuimbia Mungu na wakati umeshafika, Grace alikubaliana na wakaamua kuingi studio na kufanya albamu yao hii ya kwanza.

Grace Christian Rwegasha

Grace anasema kwake ni mara ya kwanza kufanya huduma ya uimbaji ni alipata wakati mgumu sana wa kuamua kuanza kuimba kwani alikuwa hajajipanga kwa kazi hii ya Bwana. Ila alisema hali ya kumuimba alikuwa nayo moyoni tangia muda mrefu sana lakini hakufikiria kwamba atakuja kuingia studio na kufanya kama alivyofanya siku ya leo. Garce alisema katika uimbaji wake anapata ugumu sana kuimba kwa kutumia lugha ya Kiswahili  ila anapoimba kwa lugha ya Kiingereza anajisikia huru zaidi na ukiangalia albamu yao nusu ni nyimbo za Kiswahili na nusu ni nyimbo za Kiingereza.

Grace Christian Rwegasha
Ukisikiliza nyimbo zao hakika utatambua ya kwamba waimbaji hawa wamekuja kufanya mapinduzi ya muziki wa Injili Tanzania, kuna vitu vya kipekee ambavyo huwezi kusikia kwa waimbaji wengine wanavyotumia katika huduma yao  ya uimbaji.

Grace Christian Rwegasha
Joshua (Joshu) ni kijana ambaye amekuwa mtundu sana katika eneo la muziki kwa muda mrefu sana, na sasa yuko Mwanza kimasomo katika chuo cha St. Agastine. Amekuwa akitamani sana muziki na ikafikia kipindi anatengeneza biti za muziki na kuimba. Kuna baadhi ya nyimbo alizoimba katika albamu hii ametengeneza biti yeye mwenyewe. Kwa sasa Joshu yuko Mwanza kimasomo na dada yake Grace yupo hapa Dar es Salaam.

Grace Christian Rwegasha
Waimbaji waliomba sana watu wawapokee kwani ndio wameanza kufanya kazi ya Mungu na pia waliwaomba watu wa media kuonyesha ushirikiano wao katika kupiga nyimbo zao na kufanya mahojiano ili watu waweze kujua ya kwamba kuna kitu kipya Mungu anatumia kwa kazi yake. Pia aliomba ushirikiano na watumishi wa Mungu katika huduma zao na matamsha yao kuwashirikisha

Rumafrica iko katika maandalizi ya kutengeneza DVD yao ya maohojiano ambayo utasikia katika Youtube, Facebook na katika blogu hii na blogu mbalimbali.

Grace na Joshu wamesema wako tayari kufanya kazi ya Mungu mahali popote na wakati wowote kwani wameojitambua ya kwamba wameitwa na Mungu kufanya kazi  ya Bwana.

Mbali na uimbaji, Rumafrica iliona kuna kitu ambacho watumishi hawa wanacho hasa katika kuhubiri na kutoa ushauri. Utakuja kujua haya utakaposikia mahojiano yetu.

Unaweza kuwasiliana na Grace kwa simu +255 788 443 346 au +255 654 407080

MUNGU AKUBARIKI

Thursday, April 3, 2014

FILAMU YA JICHO LANGU SASA IKO MADUKANI.

Ile siku tuliyokuwa tukisuribi sana sasa imefika, hatimaye filamu ya JICHO LANGU imetoka siku ya leo. Sasa unaweza kujisogeza taratibu madukani kujipatia nakala yako. Usisubiri wenzako waangalie ndipo usimuliwe, wewe unatakiwa kuwa wa kwanza kuwasimulia wenzanko juu ya kile utakachokiona katika filamu hii ambayo Watanzania wengi na wana Afrika Mashariki  wamekuwa wakiisubiri kwa hamu sana.

Kama ulikuwa hujui, filamu hii imetengenezwa na kampuni ya J-FILM 4 LIFE  kwa viwango vya kimataifa, hasa ukiangalia color, sound na wahusika waliocheza katika filamu hii. Ujumbe uliomo hakika unafaa kabisa katika jamii yetu inayotuzunguka. Utaweza kumuona Odama akifanya yake katika filamu pamoja na wasanii wengi maarufu ambao umewasikia. Usipange kuikosa filamu hii maana imefunika mbaya.

FAHAMU HISTORIA FUPI YA WASTARA SAJUKI TOKA ALIPO ANZA KUIGIZA MPAKA SASA


Wastara Sajuki si jina geni kwenye ulimwengu wa bongomovies. Ni mmoja wa wanadada wanofanya vizuri sana kwenye filamu nchini na wenye ushawishi mkubwa sana ndani ya tasnia hii. Ifuatayo ni historia fupi ya mwanadada huyu.

Early life
Wastara Juma Issa alizaliwa Septemba 27, mwaka 1983 huko mkoani Morogoro. Mwaka 1989 akajiunga na Shule ya Msingi Mvomelo ‘A’ na kufanikiwa kumaliza elimu yake ya msingi mwaka 1995. .Mwaka 1996 alijiunga na Sekondari ya Agricalture mkoani humo.

Career
Mwaka 1999 Wastara aliingia rasmi kwenye sanaa ya maigizo na filamu yake ya kwanza kucheza iliitwa Utaishia kunawa akiwa na gwiji wa vichekesho nchini King Majuto.

Mwaka 2004 mpaka 2006 alianza kuonekana kwenye mchezo wa Miale uliokua unarushwa na kituo cha television cha ITV

Akutana na Jennifer Mgendi

Wastara hakudumu sana kwenye kundi hilo, alikutana na kina Jenifa Mgendi ambaye pia walifanikiwa kuigiza naye filamu iliyowashirikisha baadhi ya wasanii wa kitambo akiwamo Dino na wengineo.

Mwaka 2007, Wastara alifanya usahili kwenye filamu ya mdau Ande John iliyofahamika kama Pelemende, akafaulu na kuigiza kwenye filamu hiyo kisha zikafuata filamu nyingine kama Penina kabla ya kutimkia nchini Kongo kufanya biashara.

Akutana na Sajuki

Aliporejea kutoka Kongo, Julai, 2007, Wastara aliitwa na mwigizaji Shija ambaye alimuomba aigize naye filamu baada ya kumuona kupitia kazi mbalimbali alizowahi kufanya hapo nyuma.

Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa Wastara kukutana na Sajuki ambaye sasa ni mumewe wa ndoa kwani Shija alikuwa akifanya kazi zake za uigizaji kwa kupata msaada mkubwa kutoka kwa Sajuki.

Wastara alicheza filamu kadhaa akiwa na Shija pamoja na Sajuki hadi baadaye walipokuja kugundua kuwa matatizo ya uhusiano yaliyowakuta (Sajuki na Wastara) yanafanana kwani kila mmoja wao alitendwa na mpenzi wake ndipo walianzisha uhusiano wa kimapenzi.

“Eeeeh! Kazi na dawa, tuligundua kuwa matatizo yetu yanafanana. Taratibu tukaanza uhusiano ili kufarijiana,” anasema Wastara.

FILAMU WALIZOZALISHA

Wakiwa ndani ya umoja wao, Sajuki na Wastara, walifanikiwa kuporomosha filamu zaidi ya 20 ikiwemo Mboni yangu iliyopata umaharufu mkubwa

APATA AJALI

Wakati harakati za ndoa zikiwa zimepamba moto, mwaka 2009 Wastara alipata ajali ya pikipiki iliyosababisha akatwe mguu.

Wakati huo tayari alikuwa ameshachumbiwa na Sajuki.

Juni mwaka huo huo,

wasanii hao waliopitia changamoto kadhaa za maisha, walifunga ndoa na kuanza rasmi maisha ya mume na mke.

Baada ya hapo, kupitia kampuni yao ya Wa-Jey waliendelea kuzalisha filamu kama Briefcase, The Killers, Seven Days na nyinginezo.

Tarehe 2 mwezi wa kwanza (1) mwaka 2013 Wastara alimpoteza mume wake kipenzi Juma Kilowoko (sajuki) jambo lillilosababisha kupumzika sanaa kwa muda na badae alilejea kwenye tasnia na kutoa filamu ya Shaymaa amabayo ilipata umaharufu mkubwa

Nampaka sasa anaendelea kufanya filamu nchini Tanzania
There was an error in this gadget