INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Saturday, April 23, 2016

Filamu Ya MKWE Yapokelewa Vizuri Sokoni.

Filamu ya MKWE toka kampuni ya J-Film 4 Life imeingia sokoni tayari humo ndani ikiwa na wasanii kama Odama na Hemedy. Nunua nakala yako halisi sasa.

Wezi Wa Kazii Za Wasanii Kufungwa jela Miaka 5

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) itaendelea na msako mkali kwa wafanyabiashara wote wanauza kazi za filamu na muziki bila kubandika stempu halali za kodi, ili kulinda kazi hizo kwa ajili ya kuwanufaisha wasanii pia kuhakikisha serikali inapata kodi kutoka na kazi za wasanii.

Rammy Galis Apata Shavu La Kuigiza Nigeria.

Muigizaji wa filamu nchini, Rammy Galis amepata shavu la kuigiza filamu mpya Nigeria iitwayo Her Shoes.
Rammy alienda Lagos kumalizia kurekodi video yake iitwayo Red Flag lakini imebidi aendelee kuwepo huko baada ya kupata shavu la Nollywood.

Picha: Odama Atoa Msaada Kwenye Kituo Cha Kulelea Watoto.

Staa wa Bongo Movies, Jennifer Kyaka ‘Odama’ akiwa na wasanii wenzake siku ya jana walitembelea na kutoa sadaka kwenye kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazigira magumu, kituo cha Kituo Cha UMRA Kilichopo Magomeni Mikumi  jijini Dar.

TANAPA Kutoa Locations Kwa Wasanii Wa Filamu Na Muziki Nchini.

MENEJA Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa (Tanapa), Pascal Shelutete, amesema wasanii wa filamu nchini wanatakiwa kutumia mandhari za asili zilizoko katika hifadhi za Taifa kwa ajili ya kurekodi filamu zao ili kutangaza utalii wa ndani.
Shelutete alisema hayo katika tamasha la chama cha wasanii wa filamu wa jijini Arusha (TFDAA) katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, akidai kwamba Tanapa itatoa ushirikiano kwa wasanii watakaoonyesha nia ya kurekodi filamu zao katika maeneo ya hifadhi ambayo ni salama na yenye mvuto mkubwa.

Saturday, April 9, 2016

Filamu Ya MKWE kuingia Sokoni Tarehe 18 Mwezi Huu.

Filamu kali ya MKWE toka J-Film 4 Life itaingia sokoni tarehe 18 mwezi huu. Huko ndani Hemedy, Odama, Mama Kibakuli, Mutrah na wasanii wengine wameonyesha uwezo wa vipaji vyao. Usikose kununua nakala yako halisi.

"Aisha" Filamu Ya Kitanzania Kuonyeshwa Nchini Marekani.

BAADA ya mafanikio makubwa iliyopata filamu ya ‘Aisha’ ilipoonyeshwa kumbi mbalimbali ikiwemo Nafasi Artspace na Pangani, filamu hiyo imechaguliwa kwa ajili ya kuonyeshwa katika tamasha la kimataifa la filamu la New African Films litakalofanyika Washington D.C. nchini Marekani, mwaka huu.
Pia filamu hiyo imechaguliwa kuonyeshwa katika tamasha la kimataifa la filamu duniani katika maeneo manne mashuhuri ambayo ni Los Angeles, Toronto, New York na Singapore.

Riyama Ally Awachana Wanaosema Anapenda Vijana Wadogo.

Msanii wa filamu nchini Riyama Ally ambaye siku za karibuni ametolewa mahali na msanii wa muziki wa kizazi kipya Leo Mysterio amevunja ukimya kwa watu ambao wamekuwa wakisema kuwa anatoka na dogodogo huyo.
Riyama amesema kuwa wanataka atoke na mzee ndiyo wamuone kuwa ana heshima.
Kupitia kipindi cha eNEWS kinachorushwa na EATV Riyama amesema kuwa Leo Mystereo ndiyo furaha yake, na ujio wake katikia maisha yake umemuongezea changamoto kwenye maisha yake na kumfanya awe na furaha muda wote.

Sitaki Kutoka Kimapenzi Na Star: Shamsa Ford

Msanii wa filamu nchini, Shamsa Ford hivi karibuni alifunguka kupitia mtandao wa Instagram kuwa mahusiano na mastaa wa Bongo hayadumu kwa miezi mitatu na amemuomba Mungu amuepushe mbali nayo.
Akiweka picha ya Beyonce na Jay Z, Shamsa alidai ni uhusiano wao tu ndiyo anaouelewa miongoni mwa mastaa.

Monday, April 4, 2016

Frank Na Hashim Kambi Wala Shavu La Kucheza Filamu Huko Marekani.

WAIGIZAJI kutoka  Hashim Kambi ‘Ramsey’ akiwa na msanii mwenzake Mohamed Mwikongi ‘Frank’ wamebahatika kutembelea katika viwanja vya Ikulu ya Marekani maarufu kwa jina la White State House katika jiji la Washington Amerika.
Swahilihood Hashim Kambi aka Ramsey anafunguka kwa bahati hiyo ya kuweza kufika katika eneo lenye ulinzi katika kiwango cha juu pengine kuliko Ikulu nyingi Ulimwenguni, anasema amesikia faraja kubwa sana.

Sijawahi Kutoka Na Nisha: Baraka Da Prince

Msanii Baraka de Prince ambaye kwa sasa anafanya poa na ngoma yake ya ‘SIWEZI’ na ambaye amedondoka kwenye penzi la msanii mwenzake Najma Datan amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake yeye hajawaji kutoka kimapenzi na msanii wa filamu nchini Salma Jabu alimaarufu kama ‘Nisha’.
Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live, Baraka de Prince alisema kwamba yeye hajawahi hata kuwa na ushikaji na msanii huyo na kusema kwamba inawezekana ni shabiki mzuri wa kazi zake ila hajawahi kutoka nae kimapenzi kama ambavyo inazungumzwa mtaani na kama ambavyo msanii huyo alivyowahi kusema kuwa anatoka na Baraka de Prince.

Aunty Ezekiel Na Moze Iyobo Bado Wapo Pamoja Kwa Sana Tu.

MAMA aliyejitambulisha kuwa ni mama mzazi wa dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond’ Moses Iyobo, amefungukia habari iliyozagaa mitandaoni kuwa mwanaye ameachana na mzazi mwenziye, mwigizaji Aunt Ezekiel kwa kusema habari hizo si za kweli.

Mapema wiki hii, kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, iliandikwa kuwa Moses amemwaga Aunt na kuamua kuondoka nyumbani walipokuwa wakiishi na Aunt maeneo ya Mwananyamala-Kwa mama Zakaria.

Mkwe Imezingatia Nini Mashabiki Wanataka: Odama

Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Jennifer Kyaka ‘Odama’ ametambulisha ujio wa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la MKWE ambapo ameleza kuwa imezingatia maoni ya mashabiki zake.
Kupitia ukurasa wake mtandaoni, Odama ameandika haya mara baada ya kuweka picha ya kasha la filamu yake hiyo hapo juu.

Steve Nyerere Amtaka Paul Makonda Kuangalia Tasnia Ya Filamu.

MSANII wa filamu Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ameshikilia bango la kutaka filamu za nje zizuiwe hapa nchini kwa kuamini kuwa, soko la filamu za Kibongo litazidi kutanuka na kufanya vizuri.
Akipiga stori na paparazi wetu alisema, kila anapofikiria masuala ya filamu jambo hilo huwa linazidi kumnyima raha na kumtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kulishughulikia kwa kuwa yeye ni kiongozi wa serikali kuhakikisha wasanii wa filamu za Kibongo wanakuwa na amani katika kazi zao.