INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

INTERVIEWS

ODAMA NDANI YA HOT MIX-EAST AFRICA
Msanii wa filamu Tanzania Jeniffer Kyaka a.k.a ODAMA wiki iliyopita alifanyiwa mahojiano na EATV kuhusiana na filamu yake mpya ya RUDE inayofanya vizuri sokoni kwa sasa. Mbali na hivyo alielezea maisha yake kwa ujumla na jinsi alivyofaidika na kazi ya filamu.

Kutoka kushoto ni mtangazaji wa Hot Mix, Anna Mbanjo, akifuatiwa na msanii wa filamu, Jeniffer Kyaka (Odama) na Fatna Ramole wa Hot Mix wakiwa katika studio za EATV

 Jennifer Kyaka mbali na uingizaji pia ni Mkurugenzi wa kampuni yake ya J-FILM 4 LIFE iliyoko Biafra Kinondoni Dar es Salaam. Aliongeza kwa kusema mbali na kucheza filamu za watu wengine na pia ametengeneza filamu katika kampuni yake ya J-FILM 4 LIFE kama The Avenger, Life 2 Life, All About Love, Loreen, RUDE na filamu mpya nyingine ambayo inakuja karibuni inayoenda kwa jina la HOUSE MAID .
 Odama akiwa katika pozi baada ya kufanya interview

Odama alimaliza kwa kuwashukuru wapenzi wake wanaom-support kwa kununua filamu zake, na hasa wanaotembelea blogu yake ( www.odama1.blogspot.com) ambayo imekuwa gumzo kubwa kwa kukusanya matukio ya wasanii wa filamu Tanzania na nje ya nchi.
 Wakitokelezea ndani ya EATV

Posted: 11 June 2012

 


No comments:

Post a Comment