INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Tuesday, October 29, 2013

FIGO...!!! FIGO...!!! FIGO..!!! SASA IKO MADUKANI.


Hatimaye ile siku iliyokuwa ikisubiriwa na watu wengi kujipatia nakala ya filamu mpya ya FIGO imefika. J-FILM 4 LIFE sasa imeachia kitu chake cha FIGO kwaajili yako wewe mdau wa filamu. Filamu hii ya FIGO yenye ubora wa kimataifa na ujumbe malidadi sana katika jamii yetu,  itakubadilisha kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine, mawazo yako yatabadilika na kuwa yenye mtazamo mwingie wa kimaendeleo.

Filamu hii imetengezewa katika kampuni ya J-FILM 4 LIFE iliyo chini ya Mkurugenzi Jennifer Kyaka (ODAMA) kwa kiwango cha juu sana.

JIPATIE NAKALA YAKO

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA WAKIWA KWENYE MSIBA WA BABA WA WEMA SEPETU.Leo hii rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria msiba wa Balozi Abrahamu Sepetu (Baba mzazi wa Wema Sepetu) uliotokea hapo juzi jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa kiwete amefika msibani akiongozana na mkewe hapo kutoa pole kwa familia hiyo kwa kuondokewa na Balozi Sepetu ambaye hapo alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye serikali nchini ikiwemo ya kuwa waziri wa mambo ya nje kwenye miaka ya sabini (70) kabla ya kuwa balozi wa urusi kwenye kipindi cha miaka ya 80. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

JINI KABULA AAMUA "KUOKOKA"...ASHINDA NA BIBLIA

MWANADADA anayefanya vizuri kunako gemu la filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ameamua kubadili mfumo wa maisha kwa kusoma Biblia kila wakati.

Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’. Paparazi wetu alimnasa Jini Kabula nyumbani kwake Sinza akiwa anasoma Biblia na alipoulizwa kulikoni amekuwa mtu wa kushinda nyumbani na siyo kupiga misele kama alivyozoeleka, alitiririka:
“Nimeamua kubadili mfumo wa maisha yangu niliyokuwa nikiishi zamani ya kuendekeza starehe, nimemrudia Mungu wangu na mara nyingi nashinda ndani kwangu nikisoma Biblia kwa sababu Mungu ndiye rafiki wa kweli,” alisema Jini Kabula.

Sunday, October 27, 2013

KINACHOENDELEA MSIBANI KWA BABA’KE WEMA MAREHEMU BALOZI SEPETUMama mzazi wa Wema akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mumewe mzee Sepetu.


Wema Sepetu akiwa katika hali ya majonzi baada ya kufiwa na baba yake mzazi.


Kajala Masanja (kushoto), Wema Sepetu (katikati) na Zamaradi Mketema (kulia) wakiwa katika hali ya majonzi nyumbani kwao Wema Sepetu, Sinza - Mori jijini Dar
.Kajala Masanja (kushoto) na Wema Sepetu (katikati) wakiangua vilio. Kulia Zamaradi akijaribu kumtuliza Wema.


Ndugu wa karibu wa marehemu akiwa na simanzi nzito.
Wema Sepetu akibubujikwa na machozi baada ya kuondokewa na baba yake mzazi.


STAA wa sinema za Kibongo na Miss Tanzania 2006 Wema Isaac Sepetu, bado yuko kwenye wakati mgumu baada ya leo asubuhi kupatwa na msiba mkubwa wa kuondokewa na baba yake mzazi Balozi Isaac Abraham Sepetu aliyefariki asubuhi ya leo.

Kwa sasa kuna watu wengi wamefika kumjulia hali maeneo ya Sinza, Mori jijini Dar, rafiki yake wa karibu Kajala Masanja na Zamaradi Mketema wapo bega kwa bega kuwa naye karibu na vilio vimetawala kila kona ya familia ya marehemu Balozi Sepetu.

Bado haijafahamika mazishi yanafanyika lini maana wanasubuliwa watoto wa Marehemu Tunnu Sepetu na Sunna Sepetu ambao wanaishi nchini Marekani, lakini kuna tetesi kuwa huenda mazishi hayo yakafanyika siku ya Ijumaa.

Mama mzazi wa Wema bado yuko kwenye hali ya huzuni baada ya kufiwa na mume wake ambaye amedumu nae kwa miaka mingi kabla ya kupatwa na mauti asubuhi ya leo katika hospitali ya TMJ jijini Dar. Mpaka mauti yanamfika, marehemu alikuwa akisumbuliwa na kisukari pamoja na kiharusi.

J-FILM 4 LIFE inatoa pole kwa familia yote ya marehemu Sepetu.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe!

Saturday, October 26, 2013

DIAMOND ATOA SIRI 5 ZA KURUDIANA WEMA SEPETU.....AKANUSHA KUWEPO KWA FILAMU YA YEYE KUIGIZAA NA WEMA SEPETU..

Habari na Vituko Vya Mtaa
MKALI wa songi linalotamba runingani na redioni ndani na nje ya Bongo la Number One, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ amefunguka na kuanika siri tano za kurudiana na Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Wiki mbili zilizopita, wakiwa Hong Kong, China, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii viliripoti kurudiana kwa Diamond na Wema waliomwagana takriban mwaka mmoja uliopita ambapo staa huyo wa Bongo Fleva aliibuka na kukanusha vikali akidai kuwa picha zinazomwonesha yuko na Wema ni za Filamu ya Temptations.
Akizungumza  kwa dakika ishirini katika mahojiano maalum jijini Dar mara tu baada ya kutua kutoka China Jumatano iliyopita, Diamond alikiri kufaidi penzi la Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006.
Diamond alisema kuwa, Wema ndiye aliyetangulia kwenda China ambapo yeye aliungana naye siku kadhaa baadaye akitokea kwenye shoo nchini Malaysia.
SIRI YA KWANZA
Akianika siri za kujikuta mikononi mwa mwigizaji huyo mwenye mashabiki wengi zaidi katika tasnia ya filamu za Kibongo, Diamond alisema kwanza ni ukarimu aliopewa na mrembo huyo.

Alisema kuwa alipotua Hong Kong alishangaa kukutana na mapokezi ya Wema kwenye uwanja wa ndege jambo ambalo hakulitegemea.
“Alinionesha ukarimu wa hali ya juu mno. Wakati tulipokuwa hapa Bongo tulikuwa hatusalimiani.
“Kuna vitu vingi vya ajabu vilitokea huko nyuma kati yangu na Wema. Sikufikiria wala kuwaza kama anaweza akawa mkarimu kwangu kiasi kile.

Akaongeza: “Kwa mazingira yalivyokuwa, kwa namna yoyote lazima mwanaume aliyekamilika arudishe moyo nyuma na kuacha mambo mengine yaendelee.
“Kiukweli nisema tu kuwa hata tungekutana Morogoro au Dodoma kwa ukarimu ule mwisho wa siku tungerudisha uhusiano wetu.” SIRI YA PILI
Diamond alisema baada ya mapokezi ya nguvu, Wema alimpeleka kwenye hoteli ya nyota tano (five stars) ambapo huko alipatiwa huduma ‘klasiki’ na kujiona kama yupo kwa mama Nasibu vile.

SIRI YA TATU
Alifunguka kuwa kitendo cha Wema kuwa mwenyeji wake China ambako alikuwa mgeni hadi akapazoea nacho ni siri nyingine iliyochangia wao ‘kukumbushiana’.

SIRI YA NNE
Alisema kuwa mwanadada huyo alimuonesha mapenzi mazito (yaani kutekwa kimapenzi) hivyo haikuwa rahisi kumchomolea kwani waliishi kama ndiyo penzi jipya linachipuka, akajikuta akiogelea naye.

SIRI YA TANO
Diamond alisema kuwa bado ana ndoto ya kupata mtoto kupitia kwa Wema ambaye anajua kuwa alishamwambia lengo lake juu ya kupata naye uzao hivyo katika nyakati za kukutana kwao anaamini ndoto itatimia.

HAKUNA CHA FILAMU
Alipoulizwa juu ya madai kuwa walikuwa wakirekodi filamu, Diamond alifunguka kuwa hakuna cha filamu wala sinema na kama kuna mtu anasubiri filamu atakaa sana.

“Naomba nikiri kuwa kweli zile picha hazikuwa za filamu wala nini bali ndivyo hali halisi ilivyokuwa kati yangu na Wema kule China.
“Pia naomba niseme kuwa uhusiano wetu wa kimapenzi uliishia China na sasa hivi tumebaki kama kaka na dada na ni ruksa kila mtu kumtumia mwenzie katika kazi mbalimbali kama ataona kuna ulazima wa kufanyika hivyo,” alisema Diamond.
Hii ni mara ya kwanza kwa Diamond au Sukari ya Warembo kukiri kuwa kweli alirudisha penzi lake kwa Wema walipokuwa nchini humo wakijiachia.

PENNY HANA CHAKE?
Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Diamond, ukifuatisha simulizi hiyo ya mapenzi kati ya msanii huyo na Wema, ni dhahiri kuwa mpenzi wa sasa wa jamaa huyo, Penniel Mungilwa ‘VJ Penny’ hana chake kufuatia usaliti huo.

Hata hivyo, jitihada za kumtafuta Penny ziligonga mwamba kufuatia simu yake kuita bila kupokelewa lakini juzi wanahabari wetu walipofika nyumbani kwa Diamond, Sinza-Mori, Dar waliambiwa mrembo huyo alilala hapo na kuondoka asubuhi.

Friday, October 25, 2013

MSANII WA BONGO MOVIE ANUSURIKA KULIWA KIBOGA...AZIDISHA KUNYWA POMBE NA KUJIKUTA YUKO CHOONI UCHIMuigizaji wa filamu za kibongo anayejulikana kwa jina la Danny Cloud maarufu kama Danny mtoto wa mama ambaye alipata umaarufu wa jina hilo kupitia filamu ya mtoto wa mama amenusurika kubakwa ( kuliwa kiboga )

Akizungumza na mwandishi wetu, rafiki wa karibu wa msanii huyo alidai kwamba Danny alikuwa maeneo ya Bilcanas ambapo alipewa ofa ya pombe na jamaa zake...

Rafiki huyo alidai kuwa, baada ya kupewa ofa hiyo adimu, msanii huyo alianza kuiparamia pombe mfano wa mtu mwenye kiu kali ya maji, hali iliyomfanya asijitambue na kuanza kuvua nguo...

"Kuna wakati Danny alinyanyuka na kuelea chooni huku akipepesuka...Alipofika huko alidondoka na kulala huko huko chooni, hali iliyowafanya vibaka watake kumla kiboga"...Alisema huyo rafiki yake na kuongeza:

"Baada ya kimya kirefu, ilibidi tukamwangalie ambapo tuliwakurupusha vijana watatu wakiwa wameshamvua nguo"

Source: Vituko Vya Mtaa

MAMA KANUMBA ALIA NA MCHUNGAJI KAIRUKI KWA KUDAI KANUMBA YUKO HAI

Source: Vituko vya Mtaa

Baada ya hivi karibuni kuibuka tena kwa yule nabii na Mchungaji George Kaiuruki na kudai kuwa Marehemue Steven Kanumba bado yu hai, FROLA Mtegoa - mama mzazi wa aliyekuwa mwigizaji nyota filamu wa Bongo marehemu Steven Kanumba amesikitishwa na tabia ya mtu anayejiita Nabii George Kairuki kwa kutumia jina na kifo cha marehemu mwanaye kama njia ya kujitengenezea fedha na umaarufu, mama Kanumba anasema kuwa awali Kairuki alitumia msiba wa mwanaye katika kuongelea vitu ambavyo hata familia haivijui isipo kuwa yeye pekee yake.

Mama Kanumba anadai kuwa hivi karibuni Kairuki alijitokeza kwa kudai kuwa Kanumba hajafa na amemtumia fedha katika simu yake, na kusema kuwa karibu atamrudisha duniani na kuendelea na maisha yake jambo ambalo mama wa marehemu anapingana nalo kwa kusema kuwa yeye kwa imani yake anaamini kuwa mwanaye amefariki na hakuna miujiza mingine.

“Huyu mtu anayeitwa Nabii George Kairuki sijui anatafuta nini katika familia yangu, Kanumba alikuwa ni kipenzi cha watu na sisi sote tumeshuhudia hilo kama kweli yeye ana uwezo wa kumfufua amfufue watu wote watafurahi kipenzi chao kurudi kama anavyosema yeye, mimi simjui hata sura zaidi ya kumuona katika picha,”anasema mama Kanumba

Mama Kanumba anasema kuwa iwapo Kairuki ataendelea na tabia hiyo itabidi afanye utaratibu wa kumfungulia mashitaka na hata ikibidi kumfungulia mashitaka na kumfunga endapo ataendelea na tabia ya kutumia sana jina la Kanumba katika kujitafutia fedha na kutangaza maneno ya ajabu ajabu.

Monday, October 21, 2013

WARIDI ALIA NA MAADILI KATIKA FILIMU ZA KIBONGO..


Muigizaji wa siku nyingi Anna Costantine maarufu kama Waridi ambaye alitamba sana mwishoni mwa miaka ya tisini amesema kuwa maadili ya kitanzania na kiafrika yameshuka sana katika filamu zetu mpaka ni aibu kutokana na kuiga sana uzungu ambao hata wazungu wenyewe hawafanyi hasa kwa waigizaji wa kike. Akizungumza na Mwananchi Waridi alisema "maadili yameshuka, hatuendani na maadili ya mwafrika, wanaiga sana umagharibi, tunaiga mpaka inakuwa aibu, hata wazungu hawafanyi hivyo"

Waridi ambaye alitamba enzi hizo na kina Monalisa, JB, Bishanga na Aisha alipoulizwa kuwa anategemea kurudi lini katika filamu alisema "mwanzoni mwa mwaka ujao nitarejea, nimejipanga vilivyo, ni lazima nifanye vizuri, nina kipaji, nimesomea kazi hii(chuo cha sanaa Bagamoyo), pia nina karama ya uigizaji, nitarudi kwa kasi, nitatingisha kama awali"

Sunday, October 20, 2013

HEMEDY NDANI YA PENZI ZITO NA ZUHURA GORA ....


Hemedy na Zuhura Hemedy Suleiman ambaye ni star anayetamba Swahiliwood na pia katika muziki wa Bongofleva anatoka kimapenzi na Zuhura Gora ambaye ni model na pia mwigizaji wa filamu akiwa ameigiza filamu kama vile The Beauty Fools. Chanzo makini kilicho karibu na wawili hao kiliiambia Swahiliworldplanet juzi kuwa ni muda kidogo wawili hao wapo katika penzi zito ingawa wengi wakiwemo mashabiki wao hawajui."sikia nikuambie lakini usinitaje, Hemedy na Zuhura ni wapenzi na muda wowote wakitangaza ndoa msijemkashangaa" kilisema chanzo hicho

Hata hivyo mtoa habari huyo alisema kuwa Hemedy bado kama anajifichaficha kumuweka hadharani Zuhura ili kila mtu ajue kuwa ni wapenzi huku Zuhura akijisikia huru kuwa na Hemedy kama boyfriend wake. " but unajua bado Hemedy kama hajawa tayari kumuweka hadharani Zuhura kama mtu wake lakini Zuhura yuko peace sana na relationship yao" kilimwaga data chanzo hicho. Zuhura alipotafutwa leo na Swahiliworldplanet ili kudhibitisha habari hizo alikubali kuwa ni wapenzi yeye na Hemedy kwa kujibu kwa ufupi "Yeah ni boyfriend wangu"

Zuhura ambaye ni model mwenye vigezo vyote vya kuwika kimataifa katika tasnia hiyo tayari ameonekana kwenye video za wasanii wakubwa wa Bongofleva kama vile Kamili Gado ya Profesor Jay.


-CHANZO:Swahili wold Planet

NISHA AFUNGUKA KUWA ANAJUTA KUINGIA KWENYE FANI YA KUIMBA MUZIKI..WASANII WENGINE WA FILAMU MUIGE KUTOKA KWAKE


STAA wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amesema kuwa katika maisha yake hakuwahi kufikiria kujihusisha na masuala ya muziki, isipokuwa aliingia katika fani hiyo kwa kufuata mkumbo.
Akipiga stori na paparazi wetu, Nisha alisema imekuwa ni aibu kubwa kujikita kwenye fani hiyo na kukaa kimya kwa kipindi kirefu kwa kuwa hana mapenzi ya dhati na fani hiyo kama ilivyo kwenye filamu.
“Niliona waigizaji wanaingia kuimba na mimi nikaingia, nilivamia fani tu ndiyo maana najuta, nimeamua nikae chonjo kwanza na mambo hayo nijikite zangu kwenye filamu,” alisema Nisha.

WEMA AFUNGUKA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA DIAMOND...!! SOMA HAPA..Wema Sepetu mwenyewe anajua kwamba watu wengi wanafikiri yeye anawaza kuwa na Diamond hivi sasa, lakini ametoa majibu ya hayo mawazo kwenye hii picha. Maana ya hii picha ni kwamba watu wengi wanafikiri kwamba muda wote Diamond yupo kwenye kichwa cha Wema, lakini yeye mwenyewe anasema kwamba muda wote anafikiria pesa. Unaionaje hiyo
picha?

Friday, October 18, 2013

J-FILM 4 LIFE KUACHIA FILAMU MPYA YA FIGO HIVI KARIBUNI…

Kampuni ya J-Film 4 Life iliyo chini ya mkurugenzi wake  Jennifer Kyaka (Odama) baada ya kuachia filamu nyingi  kitaani sasa inakuletea filamu nyingine yenye kiwango kingine kabisa iitwayo FIGO. Katika filamu hii utajifunza mengi sana ambayo yatakuweka katika ulimwengu mwingine.  Utapata kujua  ni kitu gani kinafanyika katika jamii yetu. Kama mdau wa J-Film 4 Life na umekuwa ukiangalia filamu zetu nyingi kama vile Pain Killer, Witch Doctor, Family War, Life 2 Life, The Avenger, Loreen na nyingine nyingi usiwaze wala kupanga kukosa kujipatia nakala yako hii ya FIGO....!!!

|
Haya ni baadhi ya matukio  yaliyoajili Location wakati wa maandalizi ya filamu hii ya FIGO.There was an error in this gadget