INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, November 26, 2015

Wolper Aweka Wazi Jinsi Anavyompenda mchumba Wake.

Muigizaji wa filamu za Bongo, Jacqueline Wolper baada ya kuvalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake miezi miwili iliyopita, jana amemwandikia ujumbe mzuri wa siku yake ya kuzaliwa kuonesha jinsi anavyompenda.

Wasanii Wa Filamu Hawana Ubunifu Kama Wasanii Wa Bongofleva: Lulu

MWIGIZAJI wa kike wa filamu aghari Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kuwa wasanii wengi wa filamu hawana mawazo ya maana wala kufikiria mambo makubwa kuhusu wanachokifanya bali ufanya tu kwa sababu wapo na jamii inawaona jambo ambalo anahisi Bongo fleva wamewazidi kuwaza.

Picha Odama Alipokutana Na Team Odama Inayomsapoti Katika Kazi Zake.

Hivi Juzi star wa filamu nchini Odama alikutana na watu wa Team Odama ambao humsapoti katika mambo mbalimbali hususani katika kazi zake , hizi ni baadhi ya picha.....

Sunday, November 22, 2015

Shilole Auza Nyumba Aliyokuwa Akijenga Huko Kimara

Msanii Shilole aliwai kuingia kwenye headlines baada ya ku-post kwenye instagram picha ya nyumba yake ambayo alikua bado anaijenga. Caption ya picha hiyo ilikua inasomeka hivi, “Mungu nisaidie nimalize hii kitu ili watoto wangu wasije kupata tabu”.
Eneo ambalo alilokua anajenga nyumba hiyo ni Kimara jijini Dar es Salaam lakini Shilole amesema kwamba ameuza nyumba hiyo ambayo ilikua bado haijaisha vizuri.

JB Anatafuta Script Ya Filamu Acheze Na Mzee Majuto, Changamkia Fursa.

"Tasnia yetu ya filam inakabiliwa na changa moto mbalibali lakini kwangu mimi changa moto kubwa kuliko zote inayo ninyima usingizi ni waandishi wa miswaada(script).
Hili kwangu ndio tatizo kubwa kuliko yote, mfano natarajia kufanya filam yangu na King Majuto, tangu mwaka jana mwezi wa 8 mpaka leo kati ya script 10 nilizoletewa hakuna inayo faa.
Mko wapi waandishi? niko tayari kununua kwa bei yoyote.Lakini ukiniletea kituko tarajia ngumi kama malipo ya usumbufu, ndiyo maana tangu nitoe mzee wa swaga mwezi wa 2 mpaka leo 20-11 sijatoa nyingine...mali ghafi(script) hamna." ameandika JB katika Instagram

Irene Uwoya Arudi Kwenye Filamu Kwa Kishindo Baada Ya Siasa.

Baada ya mikikimikiki ya uchaguzi kuisha, Staa mrembo wa Bongo Movies ambate alikuwa akiwania nasi ya Ubunge kupitia viti maalum , Irene Uwoya amerudi tena kwenye fani yake na sasa yupo kwenye maadalizi ya kazi yake mpya.
Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram Uwoya ameandika

Saturday, November 14, 2015

Wolper Kujikita Kwenye Siasa ?

 Jacqueline Wolper Massawe ameweka pembeni masuala ya uigizaji kwa muda usiojulikana kwa kile alichodai ni kujipa muda wa kupumzika na kujikita zaidi kwenye mambo ya siasa.
Rafiki wa karibu na Wolper aliyeomba hifadhi ya jina lake mwanzoni mwa wiki hii, aliliambia gazeti hili kuwa Wolper kwa sasa amekolea sana kwenye mambo ya siasa na kuona kama amekuwa akipoteza muda mwingi kwenye mambo ya uigizaji.

Alichokisema Masanja Baada Ya Kushindwa Kupeta Kura Za Maoni Huko Ludewa.

List ya mastaa wa Bongo Tanzania ambao walijitosa na kujipanga kwenye foleni ya kuusaka Ubunge iliongezeka baada ya mchekeshaji kutoka Kundi la Orijino Komedi, Masanja Mkandamizaji nae kujitosa kwenye foleni hiyo.

Filamu Ya Going Bongo Inahitaji Tuzo Zaidi: Mzee Chilo

Mwigizaji wa filamu, Chilo ametaja sababu tatu zinazoweza kuifanya filamu ya Going Bongo kushinda tuzo zaidi, ambazo ni maandalizi ya muda mrefu, kuona mbali na waigizaji kutambua kazi yao.
Mwigizaji huyo, ambaye jina lake halisi ni Ahmed Olutu, alisema inawezekana mambo mengine yamo ndani ya maandalizi, lakini kiuhalisia kila jambo linajitegemea, kwa sababu unaweza kuandaa kila kitu lakini waigizaji wakawa hawatambui thamani ya ulichokiandaa na kufanya mzaha katika kazi.
Chilo ni miongoni mwa wasanii walioigiza kwenye filamu ya Going Bongo iliyoshirikisha waigizaji kutoka nchi sita na ambayo imejishindia tuzo kadhaa.

Monday, November 9, 2015

Tasnia Ya Filamu Nchini Imeyumba Mwaka Huu: Johari.

Muigizaji wa filamu, Johari Chaula amesema kuwa mwaka 2015 haukuwa mzuri kwa wasanii wa filamu.
Johari ameiambia Bongo5 kuwa wasambazaji wa filamu wamezidiwa na kazi zinazozalishwa na wasanii.
“Mwaka huu si mzuri sana kiukweli kwa sababu wasanii wa filamu wamekuwa wengi na tunazalisha sana filamu mpaka wasambazaji wanazishindwa na wao wanasema soko haliko vizuri,” amesema.

Wema Na Diamond Walipuana

BAADA ya muigizaji nyota Wema Sepetu ‘kumtusi’ mpenziwe wa zamani, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kwa kudhihaki zawadi ya bei chee ya gari aliyowahi kumnunulia, rais huyo wa lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), juzikati aliibuka na kumjibu kuwa amefanya mambo ya ‘Kiswahili’.
Akizungumza ofisini kwake Sinza Mori jijini Dar es Salaam, Diamond alisema katika maisha kila mmoja ana ndoto zake, hivyo ni jambo jema kwamba amefanikisha, lakini hata hivyo, akasema hatua aliyofikia yeye siyo ya kufanya mashindano na mtu, badala yake ni kuchapa kazi kusaka mafanikio zaidi ya maisha yake.

Lulu Awambwatukia Wanaohoji Urembo Wake.

STAA asiyekaukiwa matukio Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amewacharukia watu wanaohoji kwa nini anapendeza angali mwanafunzi kwa kuwaambia, ‘kwani akiwa mwanafunzi ni mwiko kupendeza?’
Akizungumza  na mwandishi wa habari hii hivi karibuni,  Lulu alisema amekuwa akiona maoni ya watu wengi mtandaoni wakihoji anapata wapi fedha za kupendeza wakati yeye ni mwanafunzi hoja ambayo ameiona haina mashiko kwani yeye hatumii fedha nyingi katika urembo wake.

Wednesday, November 4, 2015

Nilitamani Diamond Platnumz Awe Mume Wangu: Wema Sepetu

Jina la Nasib Abdul bado halijatoka kichwani mwa Wema Sepetu!
Nasib Abdul ni jina halisi la Diamond Platnumz.
Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 na muigizaji wa filamu alikuwa akijibu swali kwenye kipindi cha Hitzone kupitia kituo cha redio cha Jembe FM cha jijini Mwanza alipoulizwa ni mwanaume gani ambaye alitamani awe mume wake wa ndoa.

Mume Asema Bado Anampenda Shamsa Ford.

ALIYEKUWA mzazi mwenziye na staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford, Dickson Matoke amesema kuwa ndani ya moyo wake bado anampenda sana na kumthamini mkewe huyo kama mama wa mtoto wake siku zote za maisha yake.

Faiza Ally Kuja Na Filamu Ya Baby Mama Drama.

Baada ya kushambuliwa na baadhi ya watu kuhusu malezi ya mtoto wake Sasha, aliyekuwa mke wa zamani wa Sugu, Faiza Ally ameamua kuweka wazi mpango wake wa kuachia filamu iitwayo ‘Baby Mama Drama’.

Tuesday, November 3, 2015

Picha Kutoka Royal Birthday Ya Wema Sepetu.

Wema Sepetu alianda party ya birthday yake iliyohudhuriwa na masataa na watu wake wa karibu. Hizi ni picha.......

Sitaacha Muziki Licha Kuchaguliwa Kuwa Mbunge Wa Mikumi. Professor Jay

Joseph Haule "Prefessor Jay" amabye ni msanii maarufu wa hip hop nchini amesema kuwa hataacha muziki hata kama amechaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Mikumi. Professor Jay alisema kuwa muziki ndio umefasnya wengi wamjue yeye na harakati zake za kuipigania jamii. Hivyo atawatumikia wananchi wa jimbo la Mikumi kuleta maendeleo lakini pia muziki atafanya kama kawaida kufikisha ujumbe kwa jamii.

Magufuli Awashukuru Wasanii Kwa Kumpigia Kampeni.

HAIKUWA kazi rahisi katika kuusaka urais kwa awamu ya tano kila chama kilitumia mbinu katika kuhakikisha kinaibuka kidedea, na hatimaye Dr. John J Pombe Magufuli kuteuliwa kuwa rais wa awamu ya tano, mh. Rais mteule amewashukru wasanii kwa support yao wakati wa kampeni.