INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, November 26, 2015

Wasanii Wa Filamu Hawana Ubunifu Kama Wasanii Wa Bongofleva: Lulu

MWIGIZAJI wa kike wa filamu aghari Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kuwa wasanii wengi wa filamu hawana mawazo ya maana wala kufikiria mambo makubwa kuhusu wanachokifanya bali ufanya tu kwa sababu wapo na jamii inawaona jambo ambalo anahisi Bongo fleva wamewazidi kuwaza.

“Unawaza kwanza kisha unatenda wasanii wa filamu hawana mawazo mazuri zaidi ya ubishoo tu, hatuoni mbali hatuna wivu wa kimaendeleo, leo unakuta wasanii wa Bongo fleva wanatoka nje wanarudi na tuzo lakini sisi tumekaa tu,”anasema Lulu.
Lulu anasema kuwa mwaka huu atapigana hadi ahakikishe kuwa anatoka kimataifa na kufanyakazi kubwa ambayo inaweza kumpatia tuzo kubwa kama Diamond na kufungua njia kwa wasanii wa filamu waliobweteka na kulidhika na soko la ndani ambalo halieleweki.
FC

No comments:

Post a Comment