INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, November 9, 2015

Tasnia Ya Filamu Nchini Imeyumba Mwaka Huu: Johari.

Muigizaji wa filamu, Johari Chaula amesema kuwa mwaka 2015 haukuwa mzuri kwa wasanii wa filamu.
Johari ameiambia Bongo5 kuwa wasambazaji wa filamu wamezidiwa na kazi zinazozalishwa na wasanii.
“Mwaka huu si mzuri sana kiukweli kwa sababu wasanii wa filamu wamekuwa wengi na tunazalisha sana filamu mpaka wasambazaji wanazishindwa na wao wanasema soko haliko vizuri,” amesema.

“Kwahiyo msanii kama mimi nashindwa kutoa filamu nyingi kutokana na hali hiyo, ni hivyo hivyo haukuwa mzuri sana. Lakini nadhani mwaka 2016 utakuwa mzuri zaidi kwa sababu binafsi nitajipanga mapema kuhakikisha naenda na hali hiyo ili mambo yawe mazuri,” aliongeza.
Bongo5

No comments:

Post a Comment