INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, December 26, 2013

HATIMAYE CHUCK NORRIS AJIBU MAPIGO YA VAN DAMME KWA KUTENGENEZA TANGAZO LA KUSIMAMA JUU YA NDEGE 2 LENYE MFANO WA MTI WA CHRISMASMara ya kwanza muigizaji mkongwe Jean-Claud 'Van Damme' alipotengeneza tangazo la Volvo kusimama katikati ya magari mawili makubwa ya Volvo juu ya side mirrors,mguu wa kushoto ukiwa kwenye gari moja na wa kulia kwenye lingine habari iliwashangaza watu wengi sana huku wengi wakijiuliza maswali.

VIN DIESEL ATANGAZA RASMI TAREHE YA KUACHIA FILAMU MPYA 'FAST AND FURIOUS 7'

Baada ya kusimamisha shughuli za maandalizi ya muendelezo wa saba ya Filamu ya Fast and Furious kutokana na kifo cha muigizaji 'Paul Walker aliyefariki mwishoni mwa mwezi uliopita kwa ajali ya gari.

Leo Desemba 23 Muigizaji na mkuu wa filamu ya Fast na Furious,Vin Diesel ametangaza rasmi tarehe ya kutoka kwa muendelezo wa saba wa filamu hiyo yenye mafanikio makubwa.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Diesel ameweka picha akiwa na Paul Walker na kuandika kuwa hiyo ilikuwa scene yao ya mwisho kuwa na staa huyo na kutangaza rasmi kuwa Fast and Furious sehemu ya 7 itatoka April 10 mwaka 2015.
“The last scene we filmed together…

There was a unique sense of completion, of pride we shared… in the film we were now completing… the magic captured… and, in just how far we've come… Fast and Furious 7 will be released… April 10th 2015! P.s. He'd want you to know first…,” ameandika Diesel.

Tuesday, December 17, 2013

BIFU KATI YA HEMED NA MLELA GUMZO JIJINI DARHemed (kushoto) akimtishia bastola Mlela

Hemed na Mlela wakiwa wamelazwa hospitalini baada ya kuumizana huku mama yao akiwaangalia kwa huzuni


Kasha la filamu mpya ya bifu la kina Mlela na PHD inayotarajiwa kuingia mtaani keshokutwa Jumatano. LILE bifu lililowahi kufukuta kwa kasi mithiri ya moto wa kifuu baina ya ‘tozi’ wawili ndani ya tasnia ya filamu, Hemed Suleiman ‘PhD’ na Yusuf Godfrey Willard Mlela ‘Mlela’ linadaiwa kuibuka upya na kuzidisha uhasama baina ya wasanii hao. Aidha, alisema bifu hilo lilidhihirika hivi karibuni wakati wawili hao walipokutanishwa kuigiza filamu moja, kwani mara kwa mara walijikuta wakifanya kweli kwenye baadhi ya vipande vya ugomvi na mapigano jambo lililompa wakati mgumu muongozaji wa filamu hiyo inayotarajiwa kuingia sokoni kuanzia Desemba 18 mwaka huu iliyopewa jina la I Know You. “Walikuwa na muda mrefu sana bila kukutana, tukadhani bifu lao halipo tena, lakini hivi karibuni walikutana kwenye filamu iliyoandaliwa na Mtitu Game 1st Quality, wakawa wanafanya kweli kwenye baadhi ya sehemu za majibizano na mapigano huku wakifanyiana fujo mbalimbali huku kupigana vijembe vya wazi,” alisema rafiki huyo. “Ni kweli tulikuwa na utofauti, ule mvutano wa zamani bado ulikuwepo, kila mmoja hakutaka kuwa dhaifu kwa mwenzake, utaona baadhi ya vipande tulivyofanya kweli,” alisema Mlela ambapo simu ya Hemed iliita bila kupokelewa licha ya mwandishi wetu kuipiga mara kwa mara. Naye Meneja matayarishi wa Kampuni ya Game st Quality Ltd, Noel Amani ‘Futo’ alisema filamu ya I know You iliwapa wakati mgumu sana kutokana na bifu la wasanii hao kuonekana waziwazi. “Walitumbua sana, kuna wakati walifokeana kweli, kukunjiana ngumi hata hivyo kuna baadhi ya vipande walivyofanya kweli tumelazimika kuviacha ili kuleta uhalisia zaidi. Kila mmoja anaamini yuko juu ya mwenzake,” alisema Futo.

Wednesday, December 4, 2013

MTUNIS:WHO'S BAD NDIO FILAMU YANGU YA KUFUNGIA MWAKA 2013

Mtayarishaji na Muigizaji wa filamu Nice Mohamed ‘Mtunis’amesema kwamba filamu yake ya Who’s Bad itakuwa kazi yake ya kufungia mwaka kwa kuzima kazi nyingine za filamu zilizoingia pamoja na filamu hiyo ambayo inafanya vizuri sokoni baada ya kuingia mitaani hivi karibuni.

“Kama ambavyo wengi wamenizoea ninapotoa kazi inakuwa ni bora na lazima ikimbize sokoni, sinema yangu ya Who’s Bad itafunga mwaka kama kazi bora nakuwa makini sana katika utengenezaji wa filamu na ndio kilichofanyika katika filamu hiyo wasanii wamekamua sana na kuonyesho uwezo wa hali ya juu,”anasema Nice.

Filamu hiyo imeshirikisha wasanii kama Patcho Mwamba na washiriki wengine wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu, Mtunis amekuwa akifanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo kazi alizofanya ni kama Bar mead, Who’s Bad,Clinic Love na kusambazwa na kampuni ya Steps Entertainment.

There was an error in this gadget