INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Wednesday, December 4, 2013

MTUNIS:WHO'S BAD NDIO FILAMU YANGU YA KUFUNGIA MWAKA 2013

Mtayarishaji na Muigizaji wa filamu Nice Mohamed ‘Mtunis’amesema kwamba filamu yake ya Who’s Bad itakuwa kazi yake ya kufungia mwaka kwa kuzima kazi nyingine za filamu zilizoingia pamoja na filamu hiyo ambayo inafanya vizuri sokoni baada ya kuingia mitaani hivi karibuni.

“Kama ambavyo wengi wamenizoea ninapotoa kazi inakuwa ni bora na lazima ikimbize sokoni, sinema yangu ya Who’s Bad itafunga mwaka kama kazi bora nakuwa makini sana katika utengenezaji wa filamu na ndio kilichofanyika katika filamu hiyo wasanii wamekamua sana na kuonyesho uwezo wa hali ya juu,”anasema Nice.

Filamu hiyo imeshirikisha wasanii kama Patcho Mwamba na washiriki wengine wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu, Mtunis amekuwa akifanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo kazi alizofanya ni kama Bar mead, Who’s Bad,Clinic Love na kusambazwa na kampuni ya Steps Entertainment.

No comments:

Post a Comment