INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Wednesday, July 29, 2015

Mimi Tayari Nimepata Kitambulisho Changu Cha Kupiga Kura, Kajiandikishe Pia Tuchague Viongozi Bora Kuleta Maendeleo Nchini.

Mimi tayari nimeenda kujiandikisha kupiga kura na nimepata kitambulisho changu. ukiwa kama kijana na mtanzania nenda kajiandikishe tuungane kuchagua viongozi sahihi ili kuleta mabadiliko nchini kupitia viongozi bora....

Keysher Ang'ara Kura Za Maoni Ubunge Viti Maalum Dodoma.

Msanii wa muziki wa Bongofleva Khadija Shaban maarufu kama Keysher Ameibuka kidedea kura za maoni ubunge wa viti maalum kundi la walemavu mkoani dodoma. Kwa upande mwingine wasanii wa filamu nchini Wastara Juma na Wema Sepetu wao wameshindwa kutamba ubunge wa viti maalum mkoani Morogoro na Singida.

Monday, July 27, 2015

Zari Na Diamond Waiteka Mitandao Ya Kijamii Na Hizi Picha Zao Mpya.

Zari anakaribia kujifungua muda sio mrefu, Jana Diamond na mpenzi wake huyo waliachia picha hizi matata ambazo zimekuwa zikitrend katika blogs na mitandao ya kijamii. Angalia Picha zaidi..........

Wednesday, July 15, 2015

Filamu Ya Big Surprise Bado Inaendelea Kufanya Vizuri Sokoni, Pata Nakala Yako Halisi Sasa.

Filamu kali ya Big Surprise toka kampuni ya J-Film-4 Life bado inaendelea kuchangamkiwa sokoni na mashabiki wa filamu za kitanzania. Wahi sasa kununua nakala yako halisi upate uhondo.

Kama Wewe Ni Kijana Chini Ya Miaka 40 Soma Alichoandika Ray.

"Watu wengi hawajui kwa nini wazungu huwa wanasema LIFE BEGINS AT 40. Yaani maisha yako ya kweli yataanza ukifika umri wa Miaka 40. Wakati ambapo unatakiwa uwe na elimu uliyoihitaji.. Uwe na familia yako tayari.. Uwe na kwako tayari siyo umepanga bado.. Uwe na usafiri binafsi.. Uwe na kitu chako cha kukuingizia pesa na si kutegemea ajira peke yake. At 40!

Monday, July 13, 2015

Nina Wasiwasi Kama Tutapata Rais Bora Kama Kikwete: Ray

"Napata kigugumizi na mgagasuko mkubwa sana ndani ya kilindi cha moyo wangu, kama tutaweza kumpata Rais atakaye tuthamini kama wewe baba yetu, Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Saturday, July 11, 2015

Snura Adaiwa Kufunga Ndoa Kwa Siri Na DJ Hunter.

Staa wa Bongo Fleva alieanzia uigizaji, Snura Mushi amedaiwa kufunga ndoa ya siri na mchumba wake wa siku nyingi ambaye pia ni mzazi mwenziye,DJ maarufu mjini Mbeya,Hunter.
Habari zinasema kuwa katika sherehe ya ndoa hiyo walialikwa watu wachache kutoka kwenye pande mbili za familia ya wanandoa hao na ilifungwa kwa siri jijini Dar.

Friday, July 10, 2015

Wasanii Wanapodai Hakutatokea Rais Kama Kikwete !

Naipenda sana sanaa but bado sijawaelewa baadhi ya wasanii wa Tanzania wanavyoshupalia eti hawadhani kama atatokea Rais kama Kikwete ! kisa tu walikuwa wanapiga nae picha na kualikwa ikulu mara kadhaa. Hivi hatuoni uchumi wa Tanzania ulivyodhorota na maisha kupanda sana katika utawala wa Rais Kikwete na mengine kibao. Yes ana mazuri yake machache na udhaifu wake kama binadamu wengine but To me Benjamin Mkapa was better than Kikwete coz yeye pia nimeshuhudia utawala wake tayari nikiwa najitambua ingawa sanaa wakati wa mkapa haikuwa katika kizazi cha leo , time changes and changes are inevitable in any society.

Odama Ameremeta Katika Picha Mpya.

Star wa filamu nchini Jennifer Kyaka Odama ametoa picha mpya akiwa katika style matata ya rasta na kuonekana kupendeza vilivyo kama anavyoonekana katika picha mbalimbali........
There was an error in this gadget