INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, July 24, 2014

FILAMU YA INSIDE SASA INAPATIKANA SOKONI


MWANADADA BATULI ATESWA NA DAWA ZA KULEVYA

  MWANADAFADA kutoka Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amefunguka kuwa anaumia kuona listi ndefu ya Wabongo wanaosubiri kunyongwa nchi mbalimbali kwa kukutwa na dawa za kulevya.

Mwanadada kutoka Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ akipozi.


Batuli alisema kinachowaponza vijana wengi ni kupenda fedha za chapuchapu, matokeo yake wanaambulia kifungo cha maisha na wengine kunyongwa katika nchi zenye misimamo mikali.
“Inashangaza sana wasichana wanaingia katika biashara hii haramu, mbaya zaidi wanapoingiza madawa ya kulevya wanaharibu kizazi kilichopo, inaniuma sana maana vizazi na vizazi vinaendelea kuangamia,’’ alisema Butuli.

MWANADADA BATULI ATESWA NA DAWA ZA KULEVYA
MWANADAFADA kutoka Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amefunguka kuwa anaumia kuona listi ndefu ya Wabongo wanaosubiri kunyongwa nchi mbalimbali kwa kukutwa na dawa za kulevya.


Mwanadada kutoka Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ akipozi.


Batuli alisema kinachowaponza vijana wengi ni kupenda fedha za chapuchapu, matokeo yake wanaambulia kifungo cha maisha na wengine kunyongwa katika nchi zenye misimamo mikali.
“Inashangaza sana wasichana wanaingia katika biashara hii haramu, mbaya zaidi wanapoingiza madawa ya kulevya wanaharibu kizazi kilichopo, inaniuma sana maana vizazi na vizazi vinaendelea kuangamia,’’ alisema Butuli.

Sunday, July 13, 2014

KWANINI UKOSE UTAMU WA FILAMU HII MPYA YA "INSIDE"?

Sina maneno mengi juu ya filamu hii yenye kufundisha na kuona vituko vinavyofanyika maofisini na baadhi ya wafanyakazi na maboss wao.
kama ilivyo ada, kampuni ya J-Film 4 Life imehakikisha video inaonekana katika ile quality bora yenye kiwango cha kimataifa. Maudhui yake ni yenye kuelimisha jamii na kugeuza fikra potovu za watu juu ya vituko vya maofisini.

Baadhi ya waliohusika katika filamu hii ya kimataifa ni:-


MAHOJIANO KATI YANGU NA MWANDISHI WA HABARI WA GLOBAL JUU YA UJAUZITO WANGU NA MAENDELEO YA J-FILM 4 LIFEWIKI
iliyopita tuliyaanza makala haya kwa kujua baadhi ya hatua ambazo mwigizaji, Jenifer Kyaka ‘Odama’ amepitia katika maisha yake.

Jenifer Kyaka ‘Odama’
Tuliona alikotokea, vikundi ambavyo amepitia kabla ya kufanikiwa kufungua kampuni yake ya J Film 4 Life na kuanza kuzalisha sinema zake mwenyewe.
 Leo tunaendelea na hatua nyingine ambazo amepitia katika maisha yake likiwemo suala la mchumba wake wa kwanza walivyokutana:
Mwandishi: Wasomaji wanataka kujua ulikutana wapi na mchumba wako wa kwanza na ikiwezekana umtaje jina.

Odama: Mh! Hilo ni swali gumu lakini pia ni rahisi kwa sababu jibu lake ninalo. Ukweli ni kwamba boyfriend wangu wa kwanza tulikutana maeneo ya Posta jijini Dar lakini jina siwezi kumtaja na sipendi kumuongelea sana sababu ilishakuwa na sasa hivi kila mtu ana maisha yake.
Mwandishi: Siku hizi katika mitandao ya kijamii kuna timu zinazoanzishwa kwa lengo la kumsapoti msanii flani lakini huwa zinageuka kuwa sumu kwa kushambuliana, unazizungumziaje hizi?

Odama: Kwa upande wangu sioni kama kuna tatatizo kukiwa na Timu Odama lakini tatizo linakuja kama zitageuka na kuanza kumshambulia mtu kwa matusi, zikitumika vizuri zina manufaa makubwa.

Mwandishi: Kwenye maisha yako ulishawahi kusemwa vibaya, kutukanwa hadi ukamwaga machozi?

Odama: Aaa kwangu mimi haijawahi kunitokea na haitakaa itokee maana najiamini, siwezi kuyumbishwa na mtu nikalia bila sababu za msingi.

Mwandishi: Kwa nini sanaa ya Bongo inashindwa kupenya katika anga za kimataifa?

Odama: Tatizo ni mfumo wetu, kuanzia namna kazi zinavyoandaliwa hadi kusambazwa. Hakuna mtu wa kusimamia kwa nguvu zote ndiyo maana kila siku tunaendelea kunyonywa tu. Serikali ikilichukulia soko la filamu kama ajira, tunaweza kusonga mbele. Watuwekee utaratibu na sheria ambazo zitaleta fursa ya wasanii kuwa na mitaji mizuri na kuwekeza vifaa vikubwa vya kazi.

Mwandishi: Ulikuwa mjamzito, jamii haikujua hadi ulipokuja kujifungua, sababu hasa ilikuwa ni nini?

Odama: Watu wangu wa karibu walikuwa wanajua, lakini kwenye vyombo vya habari halikuweza kuwafikia kwa haraka labda ndiyo maana wanachi hawakujua lakini watu wote wanaonizunguka walikuwa wanajua. Hakuna sababu yoyote iliyonifanya niwe msiri lakini nahisi ilitokea tu watu wa habari wengi wao walikuwa hawajui kama mimi ni mjamzito.

Mwandishi: Au ulificha kwa sababu ulijifungua kabla ya kufunga ndoa?

Odama: Hapana bwana, mipango ya kuzaa ilikuwepo. Tulijipangia mimi na mwenzangu tukakubaliana tuzae na kisha ndoa itafuata hivyo siyo kwamba ilitokea bahati mbaya.

Mwandishi: Mashabiki wako wanataka kumjua huyo mzazi mwenzako anaitwa nani na pengine mnaishi naye au vipi?

Odama: Hilo ni swali gumu umeniletea. Watamjua muda utakapofika, wasijali, kila kitu kinakwenda na wakati.

Mwandishi: Wewe tunajua unaishi Kinondoni, je mnaishi pamoja na huyo baba mtoto au la!

Odama: Hilo nalo siwezi kulijibu bwana, uliza mengine kama kuhusu hii filamu yangu mpya ya Inside iliyotoka mwezi huu. Nimecheza vizuri kweli na marehemu Recho.
Mwandishi: Turudi kidogo katika kampuni yako, ina jumla ya wafanyakazi wangapi ambao wanategemea mshahara kutokana na mnachozalisha?

Odama: Kampuni yangu ina jumla ya watu kumi na tano ambao wote kwa pamoja tunategemea kile tunachokizalisha, tunalipana na maisha yanaendelea.
Mwandishi: Kipato mnachokipata kinawatosheleza wafanyakazi wote hao, pamoja na wewe mwenyewe kama mkurugenzi?

Odama: Yah! Kinatosha na ndiyo maana unaona tunaendelea mbele vinginevyo usingetuona tumefika idadi hiyo.

Mwandishi: Kama kampuni, mmeshazalisha filamu ngapi sokoni?

Odama: Filamu ni nyingi sana sidhani kama nitazikumbuka zote lakini kuna Un Broken Promise, Life to Life, All About Love, Loreen, Rude, House Made, Chocalate, Which Doctor, Pain Killer, Figo, Jicho Langu, Family War na nyingine nyingi tu.

Mwandishi: Mnatajwa sana katika masuala ya ushirikina ili mng’ae kisanii, kwa nini msimtegemee Mungu?
Usikose makala haya wiki ijayo kwenye gazeti hili hili.

Thursday, July 10, 2014

STEVE NYERERE AWAANDALIA 'DINNER' MASTAA NA WADAU WA FILAMU

MWENYEKITI wa Bongo Muvi, Steve Nyerere jana usiku aliwaandaia chakula cha jioni mastaa na wadau mbalimbali wa filamu Bongo ikiwa ni kuungana na wenzao waliokatika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Hafla hiyo ilifanyika ndani ya Great Wall Restaurant iliyopo Osterbay jijini Dar esa Salaam.

Waigizaji na baadhi ya waandishi wa habari wakiwa tayari kusubiri chakula cha usiku kilichoandaliwa na Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere.


Wolper na Kajala wakibadilishana mawazo wakati wa hafla hiyo.

Wanamuziki wa Kundi la Makomandoo Fred (kushoto) na mwenzake Muki aliyevaa kanzu nyeupe nao pia walikuwepo katika hafla hiyo.


Tiko na Shilole nao ndani
Profesa Jay akichati kwenye simu yake wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Steve Nyerere.

Mike Sangu na mkewe Thea wakiwa katika pozi.

Muigizaji Maria akiwa na mwenzake Rose Ndauka (kulia).

Jini Kabula, Mariam Mndeme na Isabela Mpanda wakijumuika katika hafla hiyo.

Mwanamuziki Chaz Baba, na waigizaji wa Bongo Muvi wakibadilishana mawazo.

Chaz Baba akiwa na kigogo mmoja mwenye mamlaka ya kutengeneza vitambulisho vya taifa wakitaniana na Profesa Jay.

Mhudumu wa mgawaha wa Great Wall Restaurant akiwa ameshikilia samaki aina ya kaa.

Baadhi ya wageni waalikwa wakifanya yao.

Rich na Dude wakigonga menyu.

Mtitu akiomba sahani yenye nyama za kukaanga.
Waigizaji wa kike wakifanya yao.


Mahaba niue: Mike Sangu akimlisha mkewe chakula.

Malkia wa Mipasho, Bi. Khadija Kopa akila chakula kwa kutumia vijiti maalum wanavyotumia Wachina kulia chakula.

ILE FILAMU YA INSIDE ITAKUWA SOKONI WIKI IJAO

Ule muda uliopangwa kuwepo filamu ya Inside umesogezwa mbele na sasa itakuwa  sokoni wiki ijayo. Jipange kujipatia nakala yako sasa ili uweze kuona vituko vinavyofanyika maofisi.

Monday, July 7, 2014

MSANII BAKARI MAKUKA ATUNUKIWA STASHAHADA YA UANDISHI WA HABARI

MSANII katika tasnia ya filamu nchini, Bakari Makuka ametunukiwa stashaha ya uandishi wa habari katika Chuo cha Dar es Salaam City (DACICO) kilichoko Kibamba CCM jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mwandishi wetu, amewataka wasanii wenzake kujiendeleza zaidi katika masomo ya fani mbalimbali kama yeye alivyochukua fani ya uandishi wa habari.

"Ushauri wangu wasanii wasibweteke wajiendeleze na masomo kwani vyuo ni vingi sana, unaweza kusoma fani yoyote unayoitaka". Alisema Makuka


Bakari Makuka akiwa kavalia joho.


Bakali Makuka akiwa na mhitimu mwenzake baada ya kutunukiwa stashahada.


Ndugu na jamaa wakimpongeza mpendwa wao Bakari Makuka.

Sunday, July 6, 2014

DULLAH TISHIO KATIKA FILAMU HII YA "INSIDE"

Dullah kafanya yake katika filamu, ukiangalia filamu hii hakika utasema kuna watu wana talent nyingi. Dullah mbali na utangazaji radioni na kwenye TV pia ni mwigizaji mzuri sana hapa Bongo. Usikose kununua filamu itakayotoka Julai 10.2014. Nadni ya filamu hii utakutana na King Majuto, Beny, marehemu Rachel Haule, Davina, na wengine wengi.


MAHOJIANO KATI YA ODAMA NA WAANDISHI WA HABARI AKIELEZEA ALIVYO KUTANA NA MAREHEMU RECH

Makala: Erick Evarist
MTOTO mzuri mwenye asili ya Kihaya, Jenifer Kyaka ‘Odama’ aliyesoma shule ya msingi mkoani Kigoma kisha kuhamia jijini Dar na kupitia kozi tofautitofauti kabla kutupa karata yake katika anga la filamu ndiyo tupo naye leo katika Exclusive Interview.

Mtoto
mzuri mwenye asili ya Kihaya, Jenifer Kyaka ‘Odama’ akiwa na marehemu Recho Haule enzi za uhai wake.
Awali, hakuwahi kuwaza kama siku moja anaweza kuwa mwigizaji, lakini baadaye upepo ulibadilika na kujitengenezea jina la kazi, Odama. Kwenye makala haya amefunguka mambo mengi kuhusiana na safari yake ya uigizaji, twende pamoja:
Mwandishi: Wasomaji wetu wangependa kujua historia yako kifupi?
Odama: Nilianzia masomo yangu kule Kigoma baadaye nikahamia Shule ya Msingi Mburahati, sekondari nikamalizia Moshi mwaka 2000.
Mwandishi: Nini kilifuata baada ya kumaliza masomo yako ya sekondari?
Odama: Nilisoma kozi mbalimbali za kompyuta kisha ndipo nikajikuta nimekita nanga katika masuala ya filamu.
Mwandishi: Ulianzaje na nani ambaye alikuunganisha na fani hiyo?
Odama: Nilivutiwa na uigizaji ghafla, nikajiunga na Kikundi cha Kidedea, nikafanya mazoezi lakini bahati mbaya mmiliki wa kikundi hicho, Peace alifariki kikasambaratika hivyo nikawa nimepoteza uelekeo wa kisanaa.
Mwandishi: Ulifanya nini baada ya kundi hilo kufa?
Odama: Nilikaa kwa muda kisha baadaye nilikutana na ‘camera man’ mmoja anaitwa Musa Banzi ambaye alinikuta Holliday Inn, Posta nikiwa na rafiki yangu ndipo wakaniomba kushuti katika kipande cha wimbo wao baada ya mtu waliyekuwa wamempanga aje kuchelewa, baada ya kumudu uhusika vizuri katika video hiyo, kila mtu aliyekuwepo hotelini hapo aliguswa na mimi. Wakanishauri nijikite katika uigizaji.

Jenifer Kyaka ‘Odama’
Mwandishi: Wazazi wako walikupokeaje ulipoanza kujishughulisha na sanaa?
Odama: Nashukuru Mungu walinipokea vizuri, walinitia moyo na kuamini kwamba naweza kujiingizia kipato kupitia sanaa.
Mwandishi: Ugumu gani ulipitia kwenye sanaa?
Odama: Kujifua kwenye mazoezi pasipo kujulikana na watu kwa muda mrefu ndiyo changamoto kubwa niliyopitia. Kidogo nilianza kuona mwanga wa mafanikio nilipokutana na wasanii wenzangu kina Riyama, Shumileta na wengineo katika Kundi la White Elephant ambalo lilikuwa chini ya Banzi.
Mwandishi: Katika upande wa filamu, muvi gani ilikuwa ya kwanza wewe kuigiza?Odama: Sikuwa muhusika mkuu katika muvi ya kwanza kuigiza lakini ilikuwa ni Shumileta ambayo ilimpa jina mwenzangu Jenifer Mwaipaja, kila mtu akamtambua kwa jina la Shumileta.
Mwandishi: Kwa nini majina ya umaarufu zamani yalikuwa yanazalishwa na jina la filamu?
Odama: Basi tu ilikuwa inatokea hivyo, mashabiki walikuwa wakipenda kutumia jina la filamu hususan ile ambayo umecheza vizuri na kukubalika ndiyo maana hata mimi jina langu lilizaliwa mwaka 2005 nilipocheza filamu ya Odama.
Mwandishi: Ulianza lini  kujitegemea mwenyewe rasmi na kusimama katika soko la filamu?
Odama: Ilikuwa ni mwaka 2009 baada ya kufanikiwa kuanzisha kampuni yangu ya filamu, J Film 4 Life.
Mwandishi: Ulipata wapi mtaji wa kuanzisha kampuni?
Odama: Nilikuwa nafanya biashara zangu tu ambazo zilinipa mtaji wa kwenda kununua vifaa vyangu na kufungua ofisi.
Mwandishi :Inasemekana mapedeshee ndiyo ambao walikupa mtaji wa kufungua kampuni ya filamu, ni kweli?
Odama: Sijawahi kupewa mtaji na pedeshee, sina pedeshee aliyeniwezesha na wala sitakuja kuwa naye.
Mwandishi: Mlikutana wapi na marehemu Recho (Sheila Haule).
Odama: Recho nilikutana naye kipindi f’lani nilipokuwa nikifanya kazi na Bajomba (prodyuza) ambapo nilikutana na Lamata (muongozaji), tukakutana na Recho na kuanza kufanya naye kazi.
Mwandishi: Unakumbuka muvi ya kwanza kucheza na marehemu Recho?
Odama: Nakumbuka, ilikuwa ni muvi iliyofahamika kwa jina la Candy.
Mwandishi: Hebu tuambie mlikutana wapi na boifrendi wako wa kwanza?
Odama: Heeee! Swali gumu…anyway ni hivi….
Usikose wiki ijayo ili kujua Odama alikutana wapi na ‘boyfriend’ wake wa kwanza.