INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Tuesday, September 18, 2012

WASEMAVYO WADAU WANGU: "ODAMA APATA SHAVU UINGEREZA NA MALAYSIA"

 

Jennifer Kyaka ‘Odama’.

SISTADUU wa tasnia ya filamu za Kibongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amekula shavu la kufanya ziara ya kikazi nchini Malaysia na Uingereza.
Rafiki wa karibu wa Odama aliiambia Bongowood kuwa staa huyo aliondoka nchini hivi karibuni baada ya kupata shavu kutoka kwa maprodyuza wa  Nigeria ambapo atafanya nao ziara ya kikazi katika nchi hizo mbili kisha atarejea Bongo kuleta maujuzi ya kuendeleza tasnia hiyo.

BELLA:'NICHEZEWA NYWELE NA LUTEN KALAMA NAKUA TAABANI'


MISS Ruvuma 2006/07 ambaye anasukuma maisha town kupitia uigizaji na muziki wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda ‘Bella’ ameifungukia Hot 2 Hot kuwa mwanaume wake anapomchezea nywele na maeneo nyeti na kifuani huwa habari yake inakwisha kabisa na kujikuta hoi bin taabani.
Bella anayewakilisha Kundi la Bongo Fleva la Scorpion Girls alitiririka kuwa anapokuwa kwenye sita kwa sita huwa hana ujanja pale mpenzi wake, mwanamuziki Kalama Masoud ‘Luten’ anapomchezea nywele kichwani na ‘chakula ya mtoto’ kifuani.
“Sijui huwa najisikiaje lakini nashangaa tu mizuka inanipanda, inakuwa… kaazi kwelikweli!,” alifunguka Bella.
Kuhusu kuhusishwa na skendo za kutoka na wanaume tofauti, Bella alichomoa na kudai kuwa kazi yake ya sanaa ndiyo inayomkutanisha na wadau tofauti na si kila mwanaume atakayetajwa then anavunja naye amri ya sita.

SHILOLE AHOFIA KUPORWA BWANA NA MASHOSTI ZAKE

STAA wa filamu na muziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameiambia Bongowood kuwa anaogopa kumtambulisha kwa mashosti zake bwana’ke aliyenaye kwa sasa akihofia kuporwa.
Shilole anayedaiwa kunasa kwenye penzi la mtangazaji (jina tunalo), alisema kuwa anaogopa kumweka hadharani kwani kuna baadhi ya wasichana wa mjini wakishamjua mwanaume wa mtu, huwa wanamnyemelea na kumnasa kirahisi, jambo ambalo hataki limtokee.

ROSE NDAUKA:'FILAMU ZA KIBONGO HAZIPENDWI KIMATAIFA'


 
Rose Donatus Ndauka.

SURA ya mauzo katika sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka amekiri kwenye Bongowood kuwa filamu nyingi za Kibongo hazipenyi kwenye soko la kimataifa kutokana na ukweli kwamba waigizaji wengi hawana elimu ya sanaa hiyo hivyo ni ziro kabisa.
Rose alisema kwa upande wake analitambua hilo ndiyo maana yupo kwenye hatua za mwisho za kujiunga na chuo cha sanaa ambacho hakukitaja ili kuongeza elimu katika sanaa hiyo.

DIAMOND Afunguka: "HUU NDIO UKWELI KUHUSIANA NA MAHUSIANO YANGU MIMI NA WEMA SEPETU"Baada ya msanii anae-make headlines za kutosha Diamond Platnumz weekend iliyopita kukanusha habari zilizochapishwa na gazeti la Risasi kuwa ana mahusiano mapya ya kimapenzi na binti kutoka Kenya, sasa amefunguka tena kuhusiana na yeye na Wema Sepetu kupitia website yake. 

Soma alichokiandika:


"Najua watu wengi sana mnapenda Couple hii  na furaha yenu ni kutuona wawili sisi tukiwa kwenye Mahusiano ya kimapenzi.... na mmekua mkifurahi sana na story za hapa na pale mkiskia kua wawili sisi tumekua pamoja na hata pindi mkituona tuko pamoja pia Mmekua mkishangilia na kufurahi... 

bt ukweli ni kwamba Mimi na Wema hivi sasa si Wapenzi tumekua ni kama Dada na Kaka ama marafki tu wa kawaida ambao tunashirikiana katika kazi mbalimbali za sanaa na za n'nje ya sanaa, katika harakati za kujenga Taifa Letu... Pia ni vizuri ningependa mfahamu kwamba Wema ana Mpenzi wake ambae  namfaham na tunaheshimiana kama mtu na Shemeji yake........So das' de Truth abt me and Her!... and Get ready! kwa kazi tofautitofauti ambazo soon zitadondoka....".

Habari ndio hiyo!

J-FILM 4 LIFE INAKUPA POLE STEVE NYERERE KWA KUFIWA NA MWANAOMchekeshaji aliyejizolea umaarufu nchini kwa kumuigiliza hayati Baba wa Taifa, Steve ‘Nyerere’ Mangere amefiwa na mtoto wake.

Kwa mujibu wa majirani zake, mtoto huyo wa kiume amefariki baada ya kuishi kwa siku mbili tangu azaliwe.
Huyo ni mtoto wa pili kufariki kwenye familia ya Steve na mke wake aitwaye Zawadi.
“Sababu za kifo cha kwanza sijakijua, ila huyu wanasema atakuwa alivutwa wakati wa kuzaliwa, maana mtoto alikuwa mkubwa mno, sijajua ni kilo ngapi,” kilisema chanzo hicho kilicho jirani na Steve.
“Wa kwanza alifariki, wa pili yupo na huyu wa tatu amefariki.”
Kwa mujibu wa chanzo hicho, mazishi ya mtoto huyo yalifanyika jana.
Bongo5 inampa pole Steve kwa msiba huo.

MUONEKANO MPYA WA MUINGIZAJI ELIZABETH MICHAEL 'LULU'

Muigizaji nyota wa Filamu nchini Elizabeth Michael a.k.a Lulu (17) anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie, Marehemu Steven Kanumba, aliye fariki dunia Aprili 7 mwaka huu nyumbani kwake maeneo ya Vatican Sinza Jijini Dar es Salaam. Akiwa katika muonekano mpya tokea amepelekwa lupango. Kwa sasa msanii huyu anaonekana kunenepa wakati kila mtu anaamini yuko kwenye kipindi kigumu sana pengine kuliko vipindi vyote katika maisha yake tangu azaliwe. Kingine najiulizaga siku zote ile mimba ambayo ilikua ikiongelewa sana imepotelea wapi?


Monday, September 10, 2012

NDOA YA MTITU YAGHARIMU 25 MIL

 
 William Mtitu.

MSANII wa kiwanda cha filamu Bongo, William Mtitu anayetarajia kufunga ndoa Jumamosi ijayo, ametoa ripoti kuwa, bajeti ya harusi yake itakula kiasi cha  Sh. milioni 25 za Kitanzania.
Akichezesha taya na paparazi wetu, jana Jumatano jijini Dar, Mtitu alisema mpaka sasa kamati ya harusi yake imefanikiwa kukusanya mkononi Sh. milioni 16 huku watu mbalimbali wakiendelea kuahidi na kutoa.
Alisema ndoa yake hiyo itakayofungwa katika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph lililopo Posta, Dar, itafuatiwa na sherehe ya kukata na mundu kwenye Ukumbi wa Urafiki-Ubungo ambapo mavazi yatakayovaliwa na waalikwa ni ya kawaida.

SINTAH NI MENEJA MPYA WA CHIDY BEENZ


List ya managers wanaowasimamia wasanii wa bongo flava inazidi kuongezeka baada ya Sintah kutagaza kum-sign Chidy Beenz kuwa chini yake.
Hatujui deal hilo lina thamani ya kiasi gani lakini inaonekana kama Chidy ameamua kutumia experience aliyoko nayo Sintah pamoja na elimu yake ili ku-boost his public image na mziki wake pia.
Education is power and that is why Chidy kawaacha wote na kunitafuta mimi, sasa mambo ndo yameanza“, alihollar Sintah ambapo Chidi Beenz chini ya usimamizi wake atafanya show ya kwanza at New Maisha Club on 30 September.
Aliongeza kuwa Chidi Benz will be dressed by Kidoti Fashion which is owned by Jokate ambaye ndiye anayewavalisha maceleb kibao kwa sasa hapa nchini.

SNURA AJUTA 'KUMDISS' WEMAMUDA mchache umepita tangu msanii wa filamu bongo, Snura, kutangaza kuachana na rafiki yake kipenzi Wema Sepetu, sasa anaonekana kujirudi na kudai kuwa kuna vitu ameanza kuvimisi kutoka kwa mwanadada huyo ingawa anaona aibu kumuomba msahama na arudi tena kundini.

Mtandao huu  
ulimtafuta Snura kuzungumzia kwa ufupi kuhusiana na urafiki wake wa awali na Wema, ndipo alipofunguka kuwa vipo vingi na anaona haya kumuomba msamaha ili arundi tena kundini kwani anaamini akifanya hivyo watu watapata la kusema.

“Kuna vitu nimevimisi kuvifanya ambavyo nilikuwa nafanya pindi nilipokuwa na Wema, nilikuwa na hamu ya kuzungumza naye lakini naona kama nitawapa watu ncha kusema kitu ambacho sioni kama ni kizuri kwa wakati huu,”
alidai.

Hata hivyo mtandao huo ulitaka kujua ni vitu gani alivyovimisi kutoka kwa Wema ambavyo yeye mweneywe hawezi kuvifanya, na alidai kuwa kutoka usiku na kuingia sehemu viwanja vikubwa vikubwa vya starehe ambazo huingia watu wazito ni moja ya kitu ambacho anahisi atavikosa kwa muda mrefu.

JACK WA CHUZI NA JINI KABULA WAFUMWA NDIVYO SIVYO
Kwa muda mrefu waigizaji wa kike wa Bongo Movies, Jack Pentzel na Miriam Jolwa aka Jini Kabula wamekuwa wakisakamwa na skendo ya usagaji kutokana na picha iliyosambaa kwenye mtandao inayowaonesha wakibusiana.


Hata hivyo wote wameendelea kukanusha kutojihusisha na vitendo hivyo kwa kudai kuwa walikuwa kazini.

Akiongena na kipindi cha Tagz Weekly cha DTV, Jack amesema hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Miriam kwakuwa zile ni picha zilizochukuliwa wakati wakishoot movie.


“Mi mwenyewe nimezisikia kama wewe ulivyozisikia, lakini ukweli ni kwamba mimi ni msanii, ni msanii wa filamu nafanya kazi za kuelimisha jamii, kwamba jamii ntaifundisha kwamba ifanye hivi ntaikosoa ifanye hivi.  

Kwahiyo zile ni picha ambazo zilipigwa wakati tupo location, na sio kwamba zile picha walizoziona wao ndio kile kitu sisi tulichokuwa tunakifanya. Sisi tulikuwa tunaigiza, hakuna uhalisia wowote wa kitu tulichokuwa tunakifanya”, alisema.

“Mimi nina mtu wangu, mimi nina mpenzi wangu, kwanza siwezi kuwa na mahusiano na mwanamke mwenzangu, kwasababu atanifanya nini mpaka mimi niridhike?”.Aliongeza
 

Kwa upande wake Miriam, naye alikanusha kuwa na uhusiano na mwanamke mwenzake na kusisitiza kile alichokisema mwenzie.

“Ni kweli hizo picha zipo, lakini sio kama namaanisha mimi na Jack Pentzel tulikuwa tunafanya huo uchafu. Hiyo ni movie tulikuwa tunacheza, mimi nilikuwa kama namuapproach Jack, yaani mimi ndio yule mwanamke msagaji halafu yeye ndio demu wangu. Na hiyo movie sijui kwanini inachelewa kutoka,” alisisitiza Miriam.

HEMED AND GELLY WA RHYMES NDANI YA TWO IDIOT


No doubt Comedy  is nowadays doing good here in Tanzania.
Kufuatia hili singer wa “Ninachotaka“, “Alcohol” ambaye pia signs zake ziko kwenye movies za “Green Light” na “Crazy Love” is read to team up with Gelly wa Rhymes to do  comedy.
Hemedy Suleiman aka Pretty Huge Dude, ambaye ni movie star ataungana na Gelly whose real name is George ambaye ni hit maker wa nyimbo za “Kikuku“, “I Love You” na “Barafu wa Moyo Wangu” kuingia location kwa ajili ya ku-shoot a their first romantic comedy movie to be called “Two Idiots“.
Ni kweli mimi na PHD tuko tayari kufanya movie ya comedy ambayo roughly ita-cost seven million kuitengeneza chini ya E Media Company“- Gelly wa Rhymes told BK.
 Hemedy alipoulizwa utofauti wa movie hiyo yao ya comedy na comedy nyingine zilizopo hapa nchini this is what he said, “Wengi wamekuwa wakidhani kuwa comedy ni kukunya sura na kuanza kuigiza, but sisi tutatupia romantic issues na bado watu wacheke bila kulazimishwa“.
Project hii haitaishia hapa kwani baada ya Two Idiots tuna mipango ya kuanza kuvuka borders na kwenda kutafuta comedians wa kimataifa ili kuipeleka sector hii anga a mbele zaidi“-Hemedy.

Sunday, September 2, 2012

"BONGO MOVIE IMENIFUNDISHA UHUNI. NILIPOKUWA KIJIJINI SIKUWA HIVI"....RECHOMSANII anayetokea mkoani Ruvuma ambaye kwa sasa a ametengeneza jina kupitia tasnia ya filamu Rachel Haule ‘Recho’, amebainisha kuwa tasnia hiyo ndiyo iliyombandilisha kimavazi tofauti na alipokuwa anatoka kijijini kwao Songea.

Mwandishi wa mtandao huu alitaka kujua anazungumzia vipi juu ya skendo kadhaa zilizokuwa zinaelekezwa kwake kuwa anavaa mavazi ya kichokozi, ambapo alidai kuwa baada ya kuingia mjini kitambo kidogo alijikuta akitekwa na mji lakini alikuja kucharuka zaidi baada ya kuanza kujuana na wasanii wa bongo muvi ambao mara zote walimshauri kuvaa nguo fupi ili kuleta mvuto zaidi.

Aliongeza kuwa inawezekana yeye akajiona hana matatizo lakini kwa sababu tasnia hiyo ya bongo muvi inaonekana kuwa na matatizo mengi basi hata yeye watu wanamuona ana matatizo hayo ya watu wengine na hawezi kukataa kwa sababu tayari yupo kwenye chungu hicho kimoja.

“Si kwamba nilitaka kuharibiwa hapana yani nilijikuta tu napenda kuvaa mavazi ambao rafiki zangu wanavaa na kadri siku zilivyokuwa zinaenda nilizidi kuzoea” alisema.

Hata hivyo msanii huyo kwa upande wa filamu alidai kuwa zimeweza kumtangaza kwa namna moja ama nyingine na anaamini ataweza kufika mbali zaidi na kujitangaza kimataifa.

Source mpekuz

DUDE AKANA KUONEKANA KWA MGANGA TANGA


Kulwa Kikumba ‘Dude’.

STAA wa filamu za Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’, hivi karibuni alionekana kwa mganga, Pangani Tanga ambako inadaiwa alikwenda kwa ajili ya kurejesha mali zake zilizoibwa.
Dude alipotafutwa kwa njia ya simu na kupatikana alikuwa na haya ya kusema:
 “Mh! Nyie ni wambeya sana, mimi nimekuja Tanga kwa shughuli zangu za kikazi, hayo mengine ni kama ziada tu.”

JOKATE AMPONDA SNURA KWA KUJIFANYA MPAMBE WA WEMA SEPETU


MWANAMITINDO maarufu nchini Jokate Mwengelo, amedai kuwa msanii Snura asijifanye kuwa ameacha urafiki na best yake wa karibu Wema Sepetu kwani awali alikuwa kama mpambe ambaye alisahau kufanya kazi zake kwa kushindwa kusoma alama za nyakati.

Snura
amefunguka hivi karibuni na kudai kuwa eti ameamua kuachana na Wema Sepetu kwa madai kuwa alikuwa anakosa muda wa kufanya kazi zake, na badala yake muda mwingi alikuwa akifanya biashara za Wema huku akiwa
kama amsimamizi, na kazi zake zikiwa hazifananikiwi na kusonga mbele.Jokate
alipotafutwa na mwandishi wa mtandao huu ili kutoa kauli yake juu ya Snura kuachana na best yake wa karibu Wema, alidai kuwa kikubwa alichoharibu Snura ni kujifanya mpambe kwani alishindwa kufanya ishu zake badala yake alijiona kama mpambe wa Wema kwa kumfuata kokote anapokuwa.

“Unajua Snura alikuwa kama mpambe wa Wema na alishindwa kusoma alama za nyakati na sasa anadai kuwa ameachana na Wema amepoteza muda kweli mi sioni kama atakuwa ni mkweli zaidi ya uongo alionao,”
alidai.

Source: Vituko vya Mtaa
There was an error in this gadget