INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Saturday, October 31, 2015

Wala Sijapotea Nipo Najipanga.

MWIGIZAJI wa kike katika tasnia ya filamu Bongo Nuru Nassor ‘Nora’ anasema hajapotea katika tasnia ya filamu bali ni kujipanga na kufanya kazi zake zaidi kuliko za kushirikishwa kwani mara nyingi filamu ili ung’are lazima uwe mtayarishaji.

Davina Ahamasika Kugombea Ubunge Uchaguzi Ujao.

HALIMA Yahya ‘Davina’ amehamasika na mambo ya kisiasa hivyo, kujiandaa kwa kujifua vyema kwa ajili ya msimu ujao wa uchaguzi (2020).
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Davina ambaye ni msanii wa filamu Bongo, alisema kufuatia kupata fursa ya kushiriki kampeni kwa nafasi yake, maeneo mbalimbali ya nchi, amejikuta akishawishika kuwa kiongozi na kwamba baada ya miaka mitano, endapo Mungu atamjaalia uzima, atagombea nafasi ya ubunge, mkoani Iringa.

Dr.Cheni Aiomba Serikali Ya Magufuli Kutimiza Ahadi Ya Wasanii Kufaidika Na Kazi Zao.

Mahsein Awadh Said ‘Dk Cheni’ hivi karibuni ametoa ya moyoni kwa kusema kuwa serikali
ijayo iache mambo ya blabla bali itimize ahadi ambazo imekuwa ikitoa kwa wasanii ikiwa ni pamoja na kulinda haki
na masilahi yao.

Saturday, October 24, 2015

Kifo Cha Deo Filikunjombe Kimenihuzunisha Sana: Cathy Rupia

Muigizaji wa muda mrefu, Sabrina Rupia ‘Cath wa Mambo Hayo’,  amekiri kuumia vibaya kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe kutokana na ukaribu wao na jinsi alivyokuwa na moyo wa kuwajali wengine.
Akizungumza kwa uchungu na mwandishi wetu kwa njia ya simu kutoka Ludewa alikohudhuria mazishi ya mbunge huyo, Cath alisema maumivu aliyonayo kamwe hayasimuliki na kwamba itamchukua muda mrefu kumsahau Deo na kwamba ataendelea kumuombea kwa Mungu, ampumzishe kwa amani.

Picha: Wema Sepetu, Odama, Batuli, Nyamayao Katika Kuhitimisha Kampeni Za CCM Zanzibar.

Zanzibar ilishuhudia wasanii wakihitimisha kampeni za CCM visiwani humo, hizi ni picha....

Rais Wa TAFF Simon Mwakifwamba Awavaa Wasanii Wa Filamu.

RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba amewatemea cheche wasanii na kuwataka kuachana na kuendekeza kupokea fedha za wanasiasa tu bila kutetea masilahi yao.

Odama, Stan Bakora, Ali Choki, Batuli Na Wasanii Wengine Waiteka Mbeya Kumnadi Magufuli.

Mkoa wa Mbeya ulishuhudia wasanii mbalimbali wakimuombea kura Magufuli kupitia CCM. hizi ni baadhi ya picha...

Thursday, October 22, 2015

King Majuto Hafanyi Tena Filamu Za Aina Hii Baada Ya Kutoka Hijja.

Muigizaji na mchekeshaji maarufu nchini, Alhaj Athumani King Majuto, amesema baada ya kwenda kuhiji Mecca, atakuwa hafanyi tena filamu ambazo ndani yake kutakuwa na matendo ya kumchukiza Mungu.

Natamani Sana Kupata Mtoto: Jackie Pentezel

Msomaji: Mbali na sanaa unafanya shughuli gani?
Jack Chuz: Nina saluni yangu Sinza na duka la nguo. Pia ni mtaalam wa kusuka na make up.
Msomaji: Nasikia bila ndumba huwezi kukubalika kwenye sanaa, unaliongeleaje hilo?
Jack Chuz: Si kweli, uzuri wa kazi zako ndiyo uchawi wako.
Msomaji: Mumeo (Gadner) ni Muislam na dini inamruhusu wake wanne akitaka kuoa tena utafanyaje?

Tuesday, October 20, 2015

Lugha Ya Kiingereza Ni Tatizo Kwa Wanafunzi: Jokate

Miss Tanzania namba mbili 2006 na mmiliki wa kampuni ya ‘Kidoti’, Jokate Mwegelo aka Jojo, siku chache zilizopita alifanya ziara yake katika shule za secondari jiijini Dar es Salaam kama Jangwani, Azania, Benjamini Mkapa nk na kupokelewa vizuri na Waalimu pamoja na Wanafunzi. Je ziara yako ilifanikiwa kwa kiasi gani na changamoto ipi umeiona kwa wanafunzi?

Rayuu Asema Maisha Yake Mitandaoni Ni Tofauti Na Nyumbani.

Mrembo anayetikisa kiwanda cha filamu nchini, Rahma Rayuu ‘Rayuu’ amesema maisha yake halisi na maisha anayoonyesha kwenye mitandao ya kijamii ni tofauti hivyo watu wanaodhani ndivyo alivyo wanakosea.

Friday, October 16, 2015

Hizi Ndio Sifa Za Mwanaume Anayemtaka Rose Ndauka.

MSANII wa Filamu za kibongo, Rose Ndauka, ameibuka na kudai kwamba yeye si mwanamke anayependa wanaume wenye uwezo mkubwa kama tuhuma dhidi yake zinavyoeleza.

Picha: Wasanii Wakiwa Shinyanga Kumnadi Magufuli Na Samia Suluhu.

Hapa wasanii mbali mbali wanaoiunga mkono CCM wakiwa mkoani Shinyanga kumuombea kura Magufuli na Samia Suluhu....

Wanaume Hukimbia Nikiwatajia Suala La Ndoa: Nora

MSANII wa Filamu za Bongo, Nuru Nasoro ‘Nora’ amefunguka kwamba wanaume wengi wanaomtaka kimapenzi humkimbia anapowataka wasubiri hadi watakapofunga ndoa.
Nora alisema ameweka sharti hilo ili ampate mwanamume wa kweli, lakini anaona kama amejiwekea gundu kwa kuwa wengi waliojitokeza kwake hukimbia anapowaeleza masuala ya kusubiri hadi ndoa.

Picha: Davina, Odama, Wema Sepetu Ndani Ya Geita Kumpigia Kampeni Magufuli.

Geita iliwashuhudia mastaa wa filamu na muziki wanaoipigia kampeni CCM kumnadi magufuli. Hizi ni baadhi ya picha............

Monday, October 12, 2015

Tatizo La Umeme Linasababisha Tasnia Ya Filamu Kuzorota: Dr.Cheni

Msanii wa filamu, Dr Cheni amesema kuwa biashara ya filamu kwa sasa imeshuka kutokana na tatizo la umeme linaloendelea.
Dr Cheni ameambia Bongo5 kuwa mawakala wanalalamika kushindwa kuuza kazi za filamu kama walivyotarajia kutokana na tatizo la umeme.

Kayumba Ajinyakulia Mil.60 Za Bongo Star Search.

Shindano la kusaka vipaji vya waimbaji wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Star Search limemalizika huko kijana mdogo toka Temeke Kayumba Juma akijinyakulia zawadi ya kitita cha Tsh.Mil.60. Shindano hilo lilikuwa na ushindani mkali akiwemo Naseeb Fonabo toka Arusha aliyeshika nafasi ya pili ambapo yeye na Kayumba walionyesha uwezo mkubwa tangu awali.

Picha: Odama, Wema Sepetu, Batuli, Wellu Sengo Katika Kampeni Za CCM Mwanza

Hizi ni picha za wasanii wa filamu na muziki akiwemo Odama, Wema Sepetu, Wellu Sengo, Batuli na wengineo wakati walipokuwa Mwanza katika kampeni za CCM..

Thursday, October 8, 2015

Shamsa Ford Amuacha Mtoto Kwa Bibi Yake Ili Kufanya Kampeni

MTOTO wa staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford aitwaye Terry, analelewa na mama yake mzazi wakati yeye akiwa bize na kampeni kuelekea uchaguzi mkuu.
Shamsa akithibitisha jambo hilo, aliliambia gazeti hili kuwa amelazimika kumuacha mwanaye kwa bibi yake ili aende na kasi ya kampeni, lakini hujitahidi kuzungumza naye kwa simu kila siku ili kumfanya ajisikie vizuri.

Bonge La Nyau Adatishwa Na Uzuri Wa Irene Paul.

Urembo na uchapakazi wa mwanadada anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu, Irene Paul umemdatisha msanii wa muziki, Bonge La Nyau aka Nyauloso.
Nyauloso ameiambia Nje ya Box ya kipindi cha Planet Bongo cha EATV, kuwa anatadishwa mno na miondoko ya mwanadada huyo.

Tuesday, October 6, 2015

Filamu Zinalipa Kuliko Siasa

MKURUGENZI wa Jerusalem Film Company, Jacob Stephen ‘JB’ ameweka wazi kuwa kamwe hafikirii kuwa mwanasiasa kwani sanaa inamlipa zaidi.
Akizungumza na mwanahabari wetu katika mahojiano mafupi, JB alisema kipindi cha nyuma ziliibuka tetesi kuwa huenda anaweza kuwa mwanasiasa lakini ukweli kutoka moyoni, sanaa inamlipa.

Honeymoon Aljabri Afanya Filamu Nchini Marekani.

MWONGOZAJI bora wa filamu mwenye tuzo ya ZIFF 2015, Honeymoon Aljabri, yupo mbioni kukamilisha filamu yake ya pili ya ‘Forgotten Hero’ mwishoni mwa mwaka huu.
Mwongozaji huyo Mtanzania anayeishi Houston, Marekani, aliliambia MTANZANIA kwamba ameandika na kuiongoza filamu yake hiyo nchini Marekani, huku akidai kwamba ujumbe katika filamu hiyo unaonyesha uhusiano wa wapendanao ambao mmoja wao aliwahi kushiriki vita.

Sikia Point Ya Hemedy Kwa Wasanii Juu Ya Uchaguzi Mkuu.

Hemed Suleiman ‘Phd’ ametoa rai kwa masanii wengazke kutoa elimu juu ya upigaji kura katika Uchaguzi Mkuu wa badaye mwezi huu badala ya wenyewe kuwa mashabiki wa vyama.

Monday, October 5, 2015

Picha: Odama Na Kina Wema Sepetu Ndani Ya Butiama.

Odama na wasanii wenzake bado wapo katika kampeni za CCM na hivi majuzi walikuwa Butiama. hizi ni picha wakiwa huko....

Aunty Ezekiel Akana Kugombana Na Nape Nnauye.

"Ndugu zangu,
Naomba niwakumbushe jambo moja kubwa na la msingi ambalo labda mmelisahau. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na inaruhusu kila mtanzania kuwa na imani yake ya kisiasa, kwani ni haki yake ya msingi.

Riyama Ally Awaasa Wasanii Kutosahau Kupigania Haki Zao Kisa Siasa.

Habari wapendwa wangu Leo naomba kuongea na wewe MTANZANIA mwenzangu rafiki yangu unae Like na ku comment katika ukurasa wangu (kwenye mtandao wa Instagram) naamini wewe ndio balozi wangu utake nifikishia ujumbe wangu Kwa jamii inayo tuzunguka.

Wastara Na Bond Watarajia Kufunga Ndoa Baada ya Uchaguzi Mkuu.

SASA imethibitika kuwa ndoa kati ya muigizaji nyota wa filamu Wastara Juma na Mtangazaji Bond Suleiman itafanyika mara baada ya uchaguzi mkuu ujao.
There was an error in this gadget