INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Tuesday, October 6, 2015

Honeymoon Aljabri Afanya Filamu Nchini Marekani.

MWONGOZAJI bora wa filamu mwenye tuzo ya ZIFF 2015, Honeymoon Aljabri, yupo mbioni kukamilisha filamu yake ya pili ya ‘Forgotten Hero’ mwishoni mwa mwaka huu.
Mwongozaji huyo Mtanzania anayeishi Houston, Marekani, aliliambia MTANZANIA kwamba ameandika na kuiongoza filamu yake hiyo nchini Marekani, huku akidai kwamba ujumbe katika filamu hiyo unaonyesha uhusiano wa wapendanao ambao mmoja wao aliwahi kushiriki vita.

“Nimeiandika na kuiongoza filamu hii kupitia kampuni yangu ya Motion Art Production na sasa nimeshanza kuisambaza matangazo yake, natumaini itafanya vizuri na kuwa mwongozo bora tena na wa kuigwa na waongozaji wengine wenye hofu ya kuwaongoza wasanii maarufu, wakiwemo kutoka Marekani kama nilivyofanya katika filamu hii,’’ alieleza Honeymoon.
Honeymoon alishikilia tuzo ya muongozaji bora wa filamu na filamu yake ya ‘Daddy’s Wedding’ ikatunukiwa tuzo ya filamu yenye picha bora mwaka 2015, wakati wa tamasha la filamu za nchi za majahazi (ZIFF).
Chanzo: Mtanzania

No comments:

Post a Comment