INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

MAZISHI YA MAREHEMU ROSE THOMAS WA BONGO MOVIE

Marehemu Rose Thomas alikuwa mwigizaji wa filamu za Kitanzania (Bongo Movie) kwa kipindi kirefu sana. Kuna baadhi ya filamu ambazo amecheza na wasanii wengine kama Jennifer Kyaka (Odama). Filamu hizo ni Roleen, Rude, House Maid, na pia Chocolate ambayo haijaingia sokoni. Marehemu Rose alikuwa anahusika na maswala ya "make up" wakati wa maandalizi ya kutengeneza filamu.

Marehemu alikuwa anasumbuliwa na tumbo kwa muda mrefu mapaka mauti ilipomkuta siku ya Jumamosi 5 Agosti 2012 katika hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam Tanzania. Marehemu ameacha mtoto mmoja Loveness mwnye umri wa miaka 11.

Mbali na uigizaji Marehemu Rose Thomas alikuwa akifanya kazi  Salon.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI

Rose Thomas enzi za uhai wake

Ndugu na jamaa wakiwa Muhimbbili mochwari


 Kutoka kulia ni Jacquiline Wolper, Odama na Roda wakiwa katika mawazo wakati wa kusubiria mwili wa marehemu mochwari Muhimbili
 Ndugu na jamaa wakisubiriya mwili wa marehemu Rose Thomas
Mdogo wa marehemu, Happy Thomas (aliyekaa) akiwa katika majonzi
 Dada wa marehemu, Pilly (katikati) akipelekwa mahali pa kupumzika wakati akisubiri mwili wa marehemu.
 Wasanii wa Bongo Movie kutoka kushoto ni Slim, Yusuph Mlela wakisubilia mwili wa marehemu.
 Jeneza la Marehemu Rose Thomas, nyumbani kwa Baba yake mkubwa Mabibo-DSM tayari kwa kuagwa
 Kutoka kulia wa pili ni msanii wa Bongo Movie, Recho Haule, akimkumbuka rafiki yake kwa majonzi makubwa.
 Mchungaji akitoa neno la mwisho Mabibo Dar es Salaam
 Katikati ni msanii wa Bongo Movie, Jennifer Kyaka-Odama akishuhudia mwili wa rafiki yake mpenzi Rose Thomas wakati wa kuuaga.
 Kutoka kulia ni Odama, Roda na Mainda (Wasanii wa Bongo Movie)

 Roda akiwa katika masikitiko wakati wa kumuaga rafiki yake.

 Pumzika kwa amani mwanangu, tulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi.
 Mdogo wa Marehemu Happy akiwa ameshikiliwa baada ya kuaga mwili wa dada yake mpendwa.
 Msanii wa Bongo Movie, Odama akishindwa kutembea baada ya miguu yake kufa ganzi kutokana na uchungu aliokuwa nao kwa kupotelewa na rafiki yake mpenzi ambaye amecheza naye filamu mbalimbali.
 Odama akitoa machozi na kutoamini kuwa kweli rafiki yake hatamuona tena dunia.
 Msanii wa Bongo Movie, Hashim Kambi akimshikilia Odama baada ya kuaga mwili wa rafiki yake mpenzi Rose Thomas.
 Marehemu Rose Thomas akiwa katika nyumba yake ya milele.

 Rafiki yake na marehemu mama Bryan akitoa heshima zake za mwisho kabla ya mazishi kufanyika..

 Mwili wa marehemu Rose Thomas ukipelekwa katika nyumba yake ya kupumzika milele.

 Mama mzazi wa marehemu Roda Thomas katikati akimlilia mwanae Roda Thomas

 Mdogo wake marehemu, Happy akiweka shahada katika kaburi la dada yake.


 Mtoto wa marehemu, Loveness akiliweka shahada katika nyumba ya mama yake kama ishara ya upendo na kuagana.

3 comments: