INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, March 27, 2014

HII NDIYO FILAMU YA TANZANIA INAYOSUBIRIWA KWA HAMU KULIKO ZOTE

Filamu mpya ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa kwasasa ni JICHO LANGU toka kampuni ya J-Film 4 Life inayomilikiwa na Odama Jennifer Kyaka. Filamu hiyo inadaiwa ni moto wa kuotea mbali kiasi cha wamachinga kuisubiri kwa hamu kubwa. Odama, Salim Ahmed(Gabo), Thadeo Alexander na Grace Wapunda wameonyesha uwezo mkubwa humo ndani yenye funzo kubwa kwa jamii. JICHO LANGU itaingia sokoni rasmi tarehe 31 mwezi huu wa tatu. usikose kununua nakala yako halisi.

MUONEKANO MPYA WA LULU WAFANANISHWA NA MTUMISHI WA MUNGU

Actress mwenye jina kubwa Elizabeth Michael "Lulu" ameshangaza watu kadhaa wakiwemo mashabiki wake kutokana na muonekano wake mpya katika jarida la Vibe Magazine Tanzania ambalo litatoka muda si mrefu. Lulu anaonekana kama mtumishi wa Mungu wa dini ya kikristu katika picha hiyo huku ikiambatana na maneno" can you judge me".

BONGO MOVIE UNIT YATOA MSAADA KATIKA HOSPITALI YA MWANANYAMALA


Kundi la Bongo Movie Unit ambalo linaundwa na baadhi ya wasanii wa filamu Swahiliwood leo limetoa msaada wa vitu mbalimbali katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam. Kundi hilo lilitoa msaada huo kwa ushirikiano wa kampuni ya Mabibo Beer(wauzaji wa vinywaji vya Windhoek na Climax) ambayo inadhamini maadhimisho ya miaka mitatu tangu kuundwa kwa kundi hilo ambalo kwasasa mwenyekiti wake ni Steve Nyerere.
Saturday, March 22, 2014

PICHA 8:WASTARA AKIWA GYM AKIPUNGUZA UNENE
“nimenenepa sana naitaji kupungua ndio maana nafanya mazoezi“wastara

MFAHAMU ZAMARADI MKETEMA WA TAKE ONE:HUU NDIO UASALI JUU KUCHANGANYA UTAIFA,JE ALIWAHI KUSHIRIKI U-MISS NA AMESHATENGENEZA MOVIE YAKE INAITWA ?...SOMA ZAIDIKumekuwa na rumors nyingi zikienea hapa town kila mtu akisema lakwake juu ya uchanganyiko wa utaifa wa Zamaradi kutokana tu na muonekano wake ,huku wengi wakiotea kuwa ana asili ya usomali,ila ukweli ni kwamba ,Baba yake mzazi Zamaradi ni Mmanyema kutoka Kigoma, wakati mama yake mzazi ndiye mwenye asili ya kinyarwanda,kwahiyo Zamaradi ni Mmnanyema kabisa kutoka huko Kigoma.

Alishawahi kushiriki U-miss akiwa bado mwanafunzi wa chuo cha St.Augustine ya Mwanza,ingawa haikuwa kazi rahisi kwake kuweza kukubali mara moja,kuingia katika mashindano hayo,ila kutokana na ushauri wa rafiki zake wakaribu ,akiwemo mama yake mzazi, kumshawishi ,ndipo alipoamua kuingia katika mashindano hayo.Mbali na kuchelewa kuingia kambini na kuanza mazoezi na kupitia harakati nyingi za mawazo za kukubali mwisho wa siku alifanikiwa kushika nafasi ya kwanza na kuchukua taji la Miss Mwanza mwaka 2007.

Kutokana na imani kali ya kidini aliokuwa nayo baba yake ,ile baada tu ya kushinda U-miss,alipokea simu kali sana kutoka kwa baba yake mzazi na kugombezwa sana,cause hakuwa na taarifa juu ya ushiriki wa mwanaye katika maswala ya urembo ,na kutokana na kile kwamba baba yake wakati wa uhai wake alikuwa ni mtu wa dini sana.
Ingawa akiwa bado mdogo, alitamani sana aweze kukua mapema nakuanza maisha yake mwenyewe,baada ya mama yake mzazi kufariki dunia, Zamaradi Mketema akiwa bado ni msichana tu,aliachiwa mzigo mkubwa wa kumlea mdogo wake wa pekee aitwaye Ummy,yeye akiwa kama ndiye dada ,mama na baba wa pekee nyumbani hapo,hadi hivi sasa kuweza kufika mahali anajitegemea mwenyewe na cha zaidi kujaliwa mtoto wake wa kiume aliyempa jina la Junior.

Hekaheka za mitaani kwenye kipindi cha Leo tena cha cloudsFm,ndiyo iliyoweza kumpa mawazo ya ubunifu ya kufanya movie yake ya Kigodoro,katika kukaa na kusikiliza matukio mengi yanayotokea sana mtaani kupitia section ya hekaheka za mitaani,aliweza kupata wazo lililoweza kumuweka chini na kutunga story ambayo mwisho wa siku ,ndio imeweza kuzaa movie ya Kigodoro, movie iliyogharimu shilingi milioni 18 hadi kuingia sokoni.Kigodoro moja kati ya movie ambayo ,imeleta mapinduzi makubwa katika tasnia nzima ya Bongo Movie,kutokana na ubora katika uigizaji,uwezo wa hali ya juu wa wasanii waliocheza ndani ya movie hiyo na ubora wa utengenezaji mzima wa hiyo movie, ndicho kinachofanya Kigodoro iwe gumzo hapa town.

HEMEDI ATANGAZA KUOA

BRAZAMENI mwenye swaga za utozi kwenye soko la filamu Bongo, Hemed Suleiman ‘PHD’ amewataka wanawake wanaommendea kukaa naye mbali kwani tayari anajiandaa kumuoa mpenzi wake aliyemtaja kwa jina la Muna.

Hemed Suleiman ‘PHD’.

Kuonesha msisitizo, Hemed alifunguka:
“Mambo ya ujana nimeyaweka kando, nimeamua kuoa kabisa maana ukiendekeza mambo ya ubachela siyo mazuri sana, vidosho viniache.”

MASOGANGE AKIWA LOCATION AKIIGIZA MUVI...ANGALIA HAPA


Thursday, March 20, 2014

NI MATUMIZI MABOVU YA AKILI KWA MSANII KUWA BUSY NA SKENDO BADALA YA KAZI

Swahiliworldplanet ilipata nafasi ya kuzungumza machache na star wa filamu nchini Salim Ahmed "Gabo Zigamba" kuhusiana na kazi zake za filamu na maisha binafsi hivi juzi kati. Gabo ambaye kipaji chake cha kuigiza hakijifichi huku akiwa tayari amejizolea mashabiki wengi alitiririka kama ifuatavyo katika interview hii ndogo.

SWP: Nani alikushawishi kuingia kwenye sanaa ya uigizaji?

GABO: Ni msukumo wa maisha baada ya plan A na mtazamo wa ndugu jamaa na marafiki

SWP: Umefaidika na nini mpaka sasa tangu uanze kuigiza filamu?

GABO:  Kwa upande wa mafanikio bado naidai sanaa

SWP:  Kitu gani huwa kinakukera zaidi unapokuwa location?

GABO: Kero kubwa ni mijadala ya pre-production ndani production....

SWP: Baadhi ya waigizaji nchini wapo busy kutengeneza skendo ili kuandikwa kwenye media huku kazi zao zikiwa chache na bado haziridhishi je unalizungumziaje hilo?

GABO:  .Ni matumizi mabovu ya akili huwezi kuwa busy na skendo ikiwa huna kaz miliki.....

SWP:  .Umeoa au una mchumba?

GABO:  Nina mke na mtoto mmoja

SWP:  Nini matarajio yako ndani ya miaka 3 ijayo kuanzia sasa?

GABO: Kufanya sanaa kimataifa

  Kwa upande mwingine filamu mpya ya JICHO LANGU aliyoigiza Gabo, Odama na Thadeo Alexernder itaingia sokoni tarehe 31 mwezi huu wa tatu hakikisha unanunua nakala yako hali ya filamu hii mpya kali.

MAPAPARAZI WAAPA KULA SAHANI MOJA NA ODAMA KUPATA PICHA ZAKE AKIWA MJAMZITO
Odama
Chanzo cha uhakika kikizungumza na swahiliworldplanet jana kimesema kuwa mapaparazi bado hawajakata tamaa katika kupata picha za star mkubwa anayekimbiza sokoni na movies kibao, Odama Jennifer Kyaka ambaye kwasasa ni mjamzito akitarajiwa kuitwa mama. Wiki iliyopita tuliripoti kuwa mapaparazi wanadaiwa kumshawishi Odama wapate picha zake hata pesa watampa lakini star huyo asiyependa skendo amekataa katakata kwani anaona haina faida kwake zaidi ya kujichafua mbele za jamii.


Sasa chanzo chetu kimetoa habari mpya kuwa Odama bado anasakwa ili apigwe picha huku mapaparazi wakimshawishi mtu mmoja aliye karibu na Odama ampige picha na kuwapa mapaparazi na wao kumpa pesa, lakini chanzo hicho kimekataa pia kwa madai kama mwenyewe hataki hata yeye hataki kufanya hivyo isitoshe shilingi laki 1 wanayotaka kumpa ni ndogo kwani wao wataingiza pesa nyingi wakazipata picha za Odama akiwa mjamzito. "mapaparazi bado wanazitaka picha za Odama wananisumbua kwenye simu kila mara ili nimpige picha halafu niwape wanipe laki moja, siwezi kufanya hivyo hata kwa dawa, hata Odama mwenyewe hayuko tayari, wao wataingiza pesa nyingi kuliko laki moja wanayotaka kunipa" kilisema chanzo hicho.

Ukiachilia mbali chanzo hicho star mmoja wa filamu aliye rafiki wa Odama amesema kuwa Odama kwasasa anaishi kwa machale sana kuogopa kupigwa picha huku muda mwingi akiwa ndani. "Odama yupo kimachale sasa unajua wa...(akiitaja kampuni) wanataka picha zake wanamuwinda wapate picha akiwa mjamzito ila yeye kawachunia"

Ukiachana na habari hizo Odama kwasasa yupo likizo ya uzazi ila filamu yake mpya ya JICHO LANGU kutoka J-Film 4 Life itaingia sokoni tarehe 31 mwezi huu wa tatu, jiandae kununua nakala yako halisi.

Tuesday, March 18, 2014

FILAMU YA JICHO LANGU KUTOKA MWISHONI MWA MWEZI MACHI 2014

Anza mwezi Aprili na burudani kupitia  filamu mpya ya JICHO LANGU kutoka katika kampuni ya J-Film 4 Life. Tarehe 31.03.2014 ikifika jisogeze taratibu katika duka lililo karibu nawe ujipatie nakala yako ya JICHO LANGU.Ndani ya filamu hii utajifunza mengi kupitia mwigizaji maarufu nchini Tanzania Jennifer Kyaka (ODAMA) na wasanii wenzake. Hakika JICHO LANGU itakufungua mambo mengi ambayo ulikuwa hujui na hujawahi kuyaona yakitokea katika jamii yetu.

AWEKA WAZI UMRI WAKE:SANDRA AWASHUKIA WASANII WENZAKE WANAOJIONA WADOGO NA KUDANGANYA UMRI WAO

Mwigizaji wa Bongo, Salama Salmin ‘Sandra’ (32), amesema anachukizwa na tabia ya baadhi ya wasanii wenzake wanaopenda kurudisha umri nyuma kwa kujifanya wadogo kwani haoni umuhimu wake.

Salama Salmin ‘Sandra’.

Akistorisha na gazeti hili juzikati, Sandra alifunguka kuwa ni jambo la ajabu mtu kudanganya umri tena hata kwa wasanii wenzake wakati kimuonekano inaonesha dhahiri kuwa utu uzima umemnyemelea, lakini yeye anajiweka kiutoto kwa sababu ya kula ujana. “Wanajijua hamna sababu ya kuwataja, wanashindwa kumpendeza Mungu, wanajirudisha miaka nyuma ili waonekane wadogo wakati wengine sura zao zinawaumbua, kwa nini lakini?” alihoji Sandra

Sunday, March 16, 2014

PICHA ZA WASANII WA BONGO MOVIE WAKIFANYA USAFI JIJINI DAR-ES-SALAAM


Wakitoka kwenye viwanja vya mnazi mmoja kuelekea Lumumba kuanza kazi.

Meya wa wilaya ya Ilala, Jerry Slaa akiwa kazini.

Wakiwa wanafagia.

Msanii mkongwe wa filamu, Mzee Kambi akisukuma toroli la takataka.

Kazi na dawa, wasanii wa filamu wakizungumza kidogo.

Mdogo wa Rose, Rachel Ndauka akimsapoti dada yake.

Mdau wa filamu Bongo anayewasaidia wasanii mambo mbalimbali, Mama Rolaa akiwa kazini.

Rose akionesha jiko la kisasa alilotoa kwa manispaa hiyo kwa ajili ya kuchomea takataka ambalo halina madhara kwa mazingira.

Rose Ndauka (katikati) akitoa shukurani kwa watu waliomsapoti.

Meya wa Ilala, Jerry Slaa (wa pili kushoto) akiwashukuru waliojitokeza kwenye kampeni hiyo, wa kwanza kulia ni mkurugenzi wa manispaa ya Ilala, Mwendahasara.

MSANII wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka ameibuka na jipya ambapo leo amefanya kampeni ya kusafisha jiji aliyoipa jila la Ng’arisha Tanzania ambapo wadau mbalimbali wamejitokeza wakiwemo viongozi wa serikali na wasanii wenzake.

Kampeni hiyo imefanyika katika wilaya ya Ilala ambapo walianza kufagia kuanzia maeneo ya Lumumba mpaka Mnazi Mmoja.

Friday, March 14, 2014

MAPICHA:PICHA KALI ZA ROSE NDAUKA MIEZI KADHAA BAADA YA KUJIFUNGUA


Huu ni Muonekano mpya wa Msanii Rose Ndauka ikiwa ni miezi kadhaa tu tangu ajifungue...Bado ni mrembo na yuko HOT kama zamani... |

Hili ni somo tosha kwa wasanii wa kike wenye tabia ya kuchomoa mimba zao kwa kisingizio cha kupoteza mvuto baada ya kujifungua


AKIONGEA NA GAZETI LA IJUMAA - LULU NAE:"NIKO TAYARI KUOLEWA NA KUZAA MTOTO"-LULU MICHAEL

STAA wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa kama siku yoyote atapata ujauzito kwa bahati mbaya, hatafanya kosa tena, atazaa tu. Katika mahojiano maalum na gazeti hili juzikati, Lulu alisema kwa sasa yuko tayari kuolewa ili awe na familia yake ila si kwa sharti la mwanaume husika kumwambia amzalie kisha ndiyo amuoe.

Ijumaa: Kwani kwa sasa si una mpenzi? Lulu: Ndiyo ila bado sijapanga swala la kufunga naye ndoa. Ijumaa: Kwa hiyo umesema ukipata mimba kwa bahati mbaya hutofanya misteki lazima uzae, unaweza kuniambia ni misteki gani? Lulu: Nadhani maswali yako uliyoniuliza nimekujibu kiufasaha kabisa hilo siwezi kulijibu. Ijumaa linahisi kosa ambalo Lulu hatalirudia tena ni la kutoa mimba, kitu ambacho hataki kukizungumzia

UKWELI KUHUSU BEEF LA ODAMA NA SHAMSA FORD HUU HAPA
Odama Jennifer Kyaka ambaye ni star mkubwa wa filamu nchini amekanusha habari kuwa yupo katika beef na star mwenzake wa filamu Shamsa Ford. Karibia mwezi sasa baadhi ya mitandao na magazeti yamekuwa yakiandika kuwa Odama na Shamsa hawaelewani kama mwanzo kisa kikidaiwa ni Shamsa kuchelewesha mchango wa harusi ya mdogo wake Odama kinyume na taratibu na alivyoarifiwa tangu mwanzo. Hata hivyo akichonga na Swahiliworldplanet Odama alisema hana tatizo kabisa na Shamsa na wanaelewana kama kawaida "ni uongo wanaosema hivyo, sina tatizo na Shamsa na ningependa watu wasizushie wenzao mambo ambayo hayapo na hayana ukweli" alisema Odama ambaye amejizolea umaarufu pasipo kuwa na skendo za hovyo kama baadhi ya mastaa wenzake walivyo.

Kwa upande mwingine filamu mpya ya Odama inayoitwa JICHO LANGU kutoka kampuni yake ya J-Film 4 Life itaingia sokoni tarehe 31 mwezi huu wa tatu kwa hiyo kaa tayari kununua nakala yako halisi.Saturday, March 8, 2014

FILAMU YA JICHO LANGU KUTOKA MWISHONI MWA MWEZI MACHI 2014

Anza mwezi Aprili na burudani kupitia  filamu mpya ya JICHO LANGU kutoka katika kampuni ya J-Film 4 Life. Tarehe 31.03.2014 ikifika jisogeze taratibu katika duka lililo karibu nawe ujipatie nakala yako ya JICHO LANGU.Ndani ya filamu hii utajifunza mengi kupitia mwigizaji maarufu nchini Tanzania Jennifer Kyaka (ODAMA) na wasanii wenzake. Hakika JICHO LANGU itakufungua mambo mengi ambayo ulikuwa hujui na hujawahi kuyaona yakitokea katika jamii yetu.

WASTARA ASHAURIWA NA DAVINA ASIKAKTE TAMAA

Staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma.

Stori: Gladness Mallya
BAADA ya staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma kutoa shukurani kwa wasanii wenzake zilizotafsiriwa kama anajitabiria kifo chake, msanii mwenzake, Halima Yahaya ‘Davina’ ameibuka na kumtaka asikate tamaa.


Halima Yahaya ‘Davina’.

Alisema alishtuka baada ya kuona maelezo gazetini (Ijumaa Wikienda) ambayo Wastara alimpongeza kama rafiki mwenye mchango na hakujua kama anathamini na kukumbuka vitu watu walivyomfanyia ila kikubwa amemtaka asikate tamaa kwa yote yaliyomtokea.
“Asikate tama, mitihani tumeumbiwa wanadamu, tunapaswa kuishinda,” alisema Davina.