INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Friday, March 14, 2014

AKIONGEA NA GAZETI LA IJUMAA - LULU NAE:"NIKO TAYARI KUOLEWA NA KUZAA MTOTO"-LULU MICHAEL

STAA wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa kama siku yoyote atapata ujauzito kwa bahati mbaya, hatafanya kosa tena, atazaa tu. Katika mahojiano maalum na gazeti hili juzikati, Lulu alisema kwa sasa yuko tayari kuolewa ili awe na familia yake ila si kwa sharti la mwanaume husika kumwambia amzalie kisha ndiyo amuoe.

Ijumaa: Kwani kwa sasa si una mpenzi? Lulu: Ndiyo ila bado sijapanga swala la kufunga naye ndoa. Ijumaa: Kwa hiyo umesema ukipata mimba kwa bahati mbaya hutofanya misteki lazima uzae, unaweza kuniambia ni misteki gani? Lulu: Nadhani maswali yako uliyoniuliza nimekujibu kiufasaha kabisa hilo siwezi kulijibu. Ijumaa linahisi kosa ambalo Lulu hatalirudia tena ni la kutoa mimba, kitu ambacho hataki kukizungumzia

No comments:

Post a Comment