INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, March 20, 2014

MAPAPARAZI WAAPA KULA SAHANI MOJA NA ODAMA KUPATA PICHA ZAKE AKIWA MJAMZITO
Odama
Chanzo cha uhakika kikizungumza na swahiliworldplanet jana kimesema kuwa mapaparazi bado hawajakata tamaa katika kupata picha za star mkubwa anayekimbiza sokoni na movies kibao, Odama Jennifer Kyaka ambaye kwasasa ni mjamzito akitarajiwa kuitwa mama. Wiki iliyopita tuliripoti kuwa mapaparazi wanadaiwa kumshawishi Odama wapate picha zake hata pesa watampa lakini star huyo asiyependa skendo amekataa katakata kwani anaona haina faida kwake zaidi ya kujichafua mbele za jamii.


Sasa chanzo chetu kimetoa habari mpya kuwa Odama bado anasakwa ili apigwe picha huku mapaparazi wakimshawishi mtu mmoja aliye karibu na Odama ampige picha na kuwapa mapaparazi na wao kumpa pesa, lakini chanzo hicho kimekataa pia kwa madai kama mwenyewe hataki hata yeye hataki kufanya hivyo isitoshe shilingi laki 1 wanayotaka kumpa ni ndogo kwani wao wataingiza pesa nyingi wakazipata picha za Odama akiwa mjamzito. "mapaparazi bado wanazitaka picha za Odama wananisumbua kwenye simu kila mara ili nimpige picha halafu niwape wanipe laki moja, siwezi kufanya hivyo hata kwa dawa, hata Odama mwenyewe hayuko tayari, wao wataingiza pesa nyingi kuliko laki moja wanayotaka kunipa" kilisema chanzo hicho.

Ukiachilia mbali chanzo hicho star mmoja wa filamu aliye rafiki wa Odama amesema kuwa Odama kwasasa anaishi kwa machale sana kuogopa kupigwa picha huku muda mwingi akiwa ndani. "Odama yupo kimachale sasa unajua wa...(akiitaja kampuni) wanataka picha zake wanamuwinda wapate picha akiwa mjamzito ila yeye kawachunia"

Ukiachana na habari hizo Odama kwasasa yupo likizo ya uzazi ila filamu yake mpya ya JICHO LANGU kutoka J-Film 4 Life itaingia sokoni tarehe 31 mwezi huu wa tatu, jiandae kununua nakala yako halisi.

No comments:

Post a Comment