INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Saturday, January 30, 2016

Idris Na Wema Sepetu Wanena Mazito Kuhusu Uhusiano Wao.

Usiku wa jana Mastaa Wema Sepetu na Idris Sultan walidhibitisha kwa mara ya kwanza kwenye kipindi cha Ala Za Roho na mtangazaji Diva Loveness kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kwamba wana tarajia kupata mtoto wao wa kwanza.
‘’Unajua kuna kipindi nilikuwa siamini nikawa namtuma mdogo wangu akaninunulie ‘pregnancy test’nyingi ili niwe na’test’ kila siku,nilikuwa natakiwa kwenda kufanya ‘process’ ya kusafisha kizazi,nikamwambia daktari wangu kuwa natakiwa kusafisha kizazi ila nikamwambi kuwa nime’miss’ period zangu,akaniambia kabla sijasafisha kizazi nipime kwanza kama nina ujauzito,’’Wema.

Wema Sepetu Awekwa Chini Ya Ulinzi.

Mama kijacho Wema Abraham Sepetu ‘Madam’ kwa mara nyingine ametengeneza kichwa cha habari, safari hii amewekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa kosa la kuendesha gari aina ya Range Rover Evogue bila kuwa na vibali, Risasi Jumamosi lina ‘full’ stori.
Tukio hilo lililodumu kwa takriban saa tatu lilijiri Jumanne iliyopita maeneo ya Aficana, Mbezi Beach jijini Dar wakati mrembo huyo alipokuwa ‘kiguu na njia’ kwenda kwenye bethidei ya rafiki yake aliyefahamika kwa jina la Kibadude.

Tukumbuke Kuna Maisha Baada Ya Duniani: Wolper

"Kuna wakati tunatatakiwa tujue na tukumbuke kuwa haya maisha ya duniani ni ya kupita kuanzia binadamu pamoja na vitu vya duniani. Binadam tunajisahau sana tunawaza kutafuta mapesa na magari ya kifahari na majumba ya kifahari lakini hatujipangi kutafuta maisha ya huko tuendako yani kaburini😢😢.
Wengine wanagombaniana maviwanja na kudhurimiana viwanja lakini siku ya kuzikwa tunachimbiwa kasehemu kadogo tu na ndo mwisho wetu unaishia hapo😭😭😭Ee Mungu najua mm ni mkosefu na ninajua na kukwaza na kuishi kinyume cha amri zako wakati mwingine ila naomba uzidi kunitia hofu yako na maisha ninayoelekea na kila siku nijue hapa duniani sio kwangu kabisa na pia nijue mbinguni hakuna ustar wala uraisi,haya ya ustar na mengine ni mapito ya dunia kwako haya mambo hakuna😭Yanii hakuna kabisa kwa sababu ww hukuumba mtu wa kumzidi mwenzie ww ulitumia wote sawa ingawa duniani tunakosoana mwingine anamuona mwenzie sie yeye ndo anajiona ndie lakini mwisho wa siku wote tunaishia sehemu moja daaah.

Sunday, January 24, 2016

Nisha Na Mzee Majuto Waja Na KIBOKO KABISAAA.

Muigizaji Maarufu Wa Filamu nchini Nisha tarehe 29 mwezi huu anaingiza sokoni filamu yake mpya inayoitwa KIBOKO KABISAAA akiwa na King Majuto na Ben Branco na wasanii wengine. filamu hiyo inahusu maisha ya matron, mpishi na wanafunzi wa shule ya secondary ya boarding.

Davina Amtolea Uvivu Mwandishi Wa Habari Wa Gazeti La Udaku Kwa Kumwandika Kwa Habari Ya Uongo.

Gazeti la habari za burudani la Wembe limendika habari kuhusu Davida kubeba mimba nje ya ndoa...lakini msanii huyo ameonekana kuchukizwa na habari hiyo aliyoiita ya uongo

Nora Arudi kwa Kasi Na Kumshukru Mungu.

STAA aliyekuwa akitingisha kwa wasanii Bongo kutoka Kundi la Kaole, Nuru Nassoro ‘Nora’ amefunguka kuwa Mungu amemuona baada ya kukaa benchi kwa takriban miaka mitano bila kurekodi sinema.

Thursday, January 14, 2016

Bado Nipo Na Ray Hatujaachana: Chuchu Hans

Msanii wa filamu nchini, Chuchu Hans amesema bado yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na Vicent Kigosi aka Ray licha ya hivi karibuni baadhi ya watu kudai wawili hao hawapo tena pamoja.
Akizungumza katika kipindi cha Take One cha Clouds TV Jumanne hii, Chuchu alisema toka aanze kutoka kimapenzi na staa huyo mengi yamezushwa juu yake.

Bond Nusu Ajiue Kwa Sumu Kisa Wastara Kuolewa na Mbunge Sadifa.

DAR ES SALAAM: Zikiwa zimepita siku chache tangu staa wa filamu, Wastara Juma kufunga ndoa na Mbunge wa Jimbo la Donge,  Zanzibar, Sadifa Juma aliyekuwa mpenzi wake, Bond Suleiman nusu afe, Risasi Mchanganyiko lina mkanda kamili.
Wakizungumza na gazeti hili, ndugu wa karibu wa kijana huyo ambaye pia ni muigizaji (jina linahifadhiwa) alisema siku moja kabla ya ndoa ya Wastara, Bond alitaka kujiua kwa kunywa sumu, lakini kaka yake aliyeingia chumbani kwake ghafla, akamuwahi kabla hajaibugia.

Tuesday, January 12, 2016

Naweza Kuuza Filamu Zangu Mwenyewe Bila Kumtegemea Mhindi: Gabo

Msanii wa filamu aliyetamba kwenye Bado Natafuta, Gabo Zigamba amesema filamu yake mpya ‘Safari ya Gwalu’ aliyoisambaza mwenyewe kupitia kampuni yake ya D Entertainment, imemfanya agundue kuwa kusambaza mwenyewe filamu kuna manufaa zaidi kuliko kupeleka kwenye makampuni binafsi ya usambazaji.

Faiza Ally Aelezea Kuhusu Mavazi Yake Na Kutoa Ushauri Huu.

Inawezekana kuvaa nguo fupi au bikini ni tatizo hasa ktk upande wa imani zetu kutokana na maamrisho ya vitabu.
Lkn Lkn hakuna tatizo kubwa kuliko kumtangazia mtu sifa mbaya – unapo sema maneno mabaya unatengeneza sumu mbaya sana kwenye mioyo na fikra za watu…tofauti na yale mavazi maana akisha vaa anavua mwisho wa siku ni mavazi tu ambayo hayamzuru mtu yoyote kwa namna yoyote lkn maneno mabaya na sifa mbaya yana haribu fikra za watu na mioyo ya watu nakupelekea kuharibu watu na kudumu kwenye vizazi na vizazi.

Nitafuta Tattoo Za Shilole Nikipata Mwanamke Wa Kuziba Pengo Lake: Nuh Mziwanda


Chanzo cha ugomvi kati ya Shilole na Nuh Mziwanda kilichopelekea penzi lao kuvunjika kimeendelea kubaki kuwa siri yao, kutokana na wote kutotaka kukisema licha ya Shishi kuweka wazi kuwa Nuh ndiye mkosaji.
“Sipaswi kusema kitu gani kimetokea au kipi ambacho kimefanya mimi na bibie tuweze kutengana kwasababu ni maisha. Katika maisha kuna kupata na kukosa kwahiyo unaweza ukampata mtu na ukamkosa mtu, so kuachana ni kitendo cha kawaida tu ambacho kipo katika maisha yetu ya kila siku.” Alieleza NUh.

Saturday, January 9, 2016

Wasanii Fake Kukiona Cha Mtema Kuni.

KATIKA kile kinachoelezwa ni kuhakikisha heshima ya wasanii wa filamu inarejea nchini, Chama cha Wasanii wa Filamu Tanzania, kimelazimika kutunga sheria ya kuwataka wasanii, maprodyuza na wapiga picha wote kujisajili kwenye chama hicho na mtu hatoruhusiwa kufanya kazi bila kujisajili
Akizungumza jana na MTANZANIA, Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Maprodyuza Tanzania, William Mtitu, alisema kuwa kuanzia sasa ni kosa la jina filamu yoyote kuingizwa sokoni iliyochezwa na wasanii wasiojisajili na itaondolewa bila wahusika kufidiwa gharama waliyopoteza wakati wa kuiandaa.

Serikali Inatuangusha Wasanii: Dr.Cheni

Msanii mkongwe wa filamu nchini, Dr Cheni amesema wasanii wengi wa filamu bado wapo kwenye kigugumizi kwenye kuwekeza pesa nyingi katika filamu zao kwa kuwa bado serikali haijatoa kauli yoyote kuhusu ulinzi wa kazi zao.
Dr Cheni ameiambia Bongo5 kuwa hali hiyo bado inawafanya waendelee kusita kuwekeza pesa nyingi kwenye kazi zao.

Tattoo Yangu Inaonyesha Jinsi Nilivyoumizwa Katika Mapenzi: Amanda

STAA wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amesema tattoo yake aliyojichora mgongoni yenye maneno ‘Mapenzi yanauma’ ni kama inasema kwani mwanaume yeyote atakayekuwa naye kimapenzi, akiiona itampa kitu cha kujifunza.

Monday, January 4, 2016

Nikipata Tatizo Team Diamond Watahusika: Esha Buheti

Chokochoko! Msanii wa filamu za Kibongo, Esha Buhet amefunguka kuwa endapo atakumbwa na tatizo lolote basi timu ya Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Team Diamond itahusika.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Esha alisema kuwa chokochoko zilianza alipoposti picha za Ali Kiba mtandaoni ambapo Team Diamond walianza kumtukana na kumwambia watamfanyia kitu mbaya

Maggie Vampire Kuwa Tishio Kwa Kina Uwoya, Odama, Lulu, Wolper Na Wema Sepetu !

SINEMA mpya ya kimataifa ya Homecoming imekuja na vipaji vipya katika sinema za Kibongo, huku Magdalena Munisi akiibuka na kuwatishia amani madiva wa Bongo Muvi wanaotesa katika tasnia hiyo.
Mastaa wanaoonekana kufanya vizuri zaidi Bongo Muvi kwa sasa ni pamoja na Elizabeth Michael ‘Lulu’, Irene Uwoya, Wema Sepetu, Rose Ndauka, Shamsa Ford na Aunt Ezekiel.

Steve Nyerere Kutoa Filamu Kubwa Mwaka Huu.

Steve Nyerere amesema baada ya kukaa kimya kwa miaka minne bila kutoa filamu, mwaka 2016 atawapa raha mashabiki wake.
“Nina miaka minne sijatengeneza wala kutoa sinema na si kwamba siuzi,” aliandika kwenye Instagram.
“Kwa mwaka nitakuwa natoa sinema 1 tu ila itakuwa zaidi ya vile tunavyofikiria, ni ubora wa hali ya juu sio kwa mwezi sinema 5, duu ni kumvuruga mteja. Maisha ni kujipanga na kujitambua unataka nini.”

Friday, January 1, 2016

Picha: Odama Alipofanya Special Appearance Wakati AY Na Bob Junior Wakitumbuiza.

Odama juzi alikuwa na special appearance wakati AY na Bob Junior wakitumbuiza katika party flani ya kijanja. Hizi ni picha,,,

TV Zimeua Tamthilia Za Kitanzania: Mzee Chilo

Msanii wa filamu, Mzee Chilo amedai wamiliki wa runinga nchini ndio waliosababisha kupotea kwa tamthilia za nyumbani kwa kuzikwepa na kuonesha za kigeni.
Muigizaji huyo ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ya Pilipili Entertainment, ameiambia Bongo5 kuwa hali hiyo imesababisha wazalishaji wa filamu nchini kukaa na kazi zao ndani bila kuwa na sehemu za kuzipeleka.

TAFF Na Bongo Movie Waondoa Tofauti Zao.

BIFU kubwa lililokuwepo kati ya wasanii wa fi lamu wanaounda Bongo Movie na wale wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘Taff ’ limeyeyuka baada ya viongozi wa pande zote mbili kukutana na kuona kuna ulazima wa kuwa kitu kimoja.
There was an error in this gadget