INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Saturday, January 9, 2016

Serikali Inatuangusha Wasanii: Dr.Cheni

Msanii mkongwe wa filamu nchini, Dr Cheni amesema wasanii wengi wa filamu bado wapo kwenye kigugumizi kwenye kuwekeza pesa nyingi katika filamu zao kwa kuwa bado serikali haijatoa kauli yoyote kuhusu ulinzi wa kazi zao.
Dr Cheni ameiambia Bongo5 kuwa hali hiyo bado inawafanya waendelee kusita kuwekeza pesa nyingi kwenye kazi zao.

“Tuna ari ya kufanya kazi kubwa ndani ya mwaka huu kwa sababu tayari kila mmoja anasubiri kauli ya serikali ili tuweze kuwekeza zaidi kwenye kazi zetu mpya,” amesema.
“Sasa kwakuwa bado hawajatoa kauli yoyote na sisi tunashindwa kuwekeza pesa nyingi kwenye filamu kwakuwa serikali bado ipo kimya, unaweza ukawekeza halafu mambo yakawa yale yale,” amesisitiza.
“Viongozi wetu bado wanahangaika ili kuweka mambo sawa, nadhani wakifanikiwa kila kitu kitakuwa wazi na kazi zetu zenye ubora zitaanza kumiminika kama kawaida.”
Chanzo: Bongo5

No comments:

Post a Comment