INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Friday, August 19, 2016

Zari Awapa Za Uso Wabaya Wake.

Kuna tetesi nyingi sana zimevuma kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni zikiwahusu Diamond na Zari.
Huku tetesi hizo zikimhusisha Diamond kusaliti mahusiano yake kwa kutoka na warembo wengine akiwemo Hamisa Mobetto na mrembo aliyetumika kwenye video ya wimbo wa ‘Kwetu’, Irene.

Wema Sepetu Na Petit Man Wapatana.

Kwa miezi kadhaa sasa Wema Sepetu na Petit Man walikuwa wakichuniana hadi kuwafanya mashabiki waanze kuuliza maswali kupitia mitandao ya kijamii kutaka kujua kunani!

Mapenzi Yamtesa Fid Q

AGOSTI 13, mwaka huu ilikuwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mwanahip Hop, Fid Q na kwa furaha aliyonayo kwa kutimiza miaka kadhaa, siku hiyo aliamua kuachia ngoma mbili kama zawadi kwa mashabiki wake.
Wimbo wa kwanza unaoitwa Sumu aliutoa usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita, baadaye jioni akaachia video ya ngoma nyingine ya Roho aliyomshirikisha Christian Bella.

Masanja Awaangukia Polisi Na Kuyamaliza.

Katika harusi ya Masanja Mkandamizaji iliyofanyika Agosti 14, wachekeshaji wenzake wa kundi la Orijino Komedi, walikuja wamevalia nguo zilizofanana na sare za jeshi la Polisi hali iliyowapelekea kukamatwa. Walifikishwa kituo cha Polisi kwa mahojiano na pia wakakaguliwa sehemu wanazoishi ili kuweza kufahamika kama kuna kitu kingine wanachomiliki tofauti na sare za Polisi.

Thursday, July 28, 2016

Riyama Ally Awaumbua Waliosema Hatafika Popote Na Leo Mysterio.

STAA wa filamu za Kibongo, Riyama Ally amewafunga midomo wote waliokuwa wakibeza uhusiano wake na msanii chipukizi wa muziki wa Bongo Fleva, Haji Mwalimu Mzee ‘Leo Mysterio’, baada ya kufunga naye ndoa hivi karibuni.
Minong’ono ilikuwa mingi mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kuwa Riyama yupo kwenye uhusiano na Serengeti Boy kwa vile kijana huyo ni mdogo wake kiumri kwa miaka saba zaidi.

Gabo Aishauri Serikali Kuhusu Sanaa Na Kilimo.

Msanii Salim Ahmed alimaarufu kama ‘Gabo Zigamba’ ameishauri serikali ya awamu ya tano kutolea macho kwenye sekta ya kilimo Tanzania pamoja na vipaji na kusema kuwa hivyo ndivyo vyanzo vizuri vya mapato.

Jay Moe Afunguka Kuhusu Shilole.

Mwanamuziki rapa nchini anayetikisa kwa ngoma ya ‘Pesa Madafu’, Jay Moe amekuwa akionekana karibu sana na rapa Bilnass ambaye anatikisa na ngoma ya ‘Chafu Pozi’ kitu ambacho ni njia pekee ya Jay Moe kumpata mrembo Shilole.
Baada ya kuwepo kwa tetesi za wawili hao kutoka kimapenzi na zaidi kuonekana picha wako pamoja kwenye moja ya eneo za kula bata wakati wa usiku, ENewz ilimtafuta rapa Jay Moe avunje mzizi huo wa fitna kama ni kweli anaanguka kwa Shilole lakini alikanusha nakusema ndio mara ya kwanza yeye kusikia habari hizo.

BASATA Wamfungia Na Kumpiga Faini Nay Wa Mitego.

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia kwa kipindi kisichojulikana msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kwa jina la Nay wa Mitego.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia kwa kipindi kisichojulikana msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kwa jina la Nay wa Mitego hadi hapo litakapojiridhisha kwamba ametekeleza maagizo yote aliyopewa na Baraza sambamba na yeye kubadilika katika kubuni kazi zenye maadili na zisizo dhalilisha watu wa kada mbalimbali.

Thursday, July 21, 2016

Wema Sepetu Achoshwa Na Wanaomfuatilia.

"Naomba niseme kitu na nieleweke tafadhal, Sijawahi hata siku moja kwenda kwa hata mmoja wenu na kumgongea kuomba hata hela ya chumvi…. My life concerns me…. Na hata siku nikifa nakufa mwenyewe, Majibu kwa Mungu naenda kujibu alone…. Niacheni Jamani…. Nimechoka……! Jus leave me Alone…!!! Kama nakukera na maisha yangu basi usiyafatilie… Sio lazima….. Nisiheme sasa…. Naomba tafadhal kama mapungufu ni ya kwangu mimi na mimi mwenyewe sasa midomo

Wema Sepetu Bado Anataka Kuzaa Na Idris.

LICHA ya madai kuwa wapenzi wawili, Idris Sultan na Wema Sepetu wamemwagana, muigizaji huyo nyota na Miss Tanzania 2006, amesema anataka kuzaa na mshindi huyo wa Big Brother Hotshots 2014 kutokana na jinsi anavyojali na mwenye huruma nyingi.

Ali Kiba Na Baraka Dah Prince Wavamiwa Na Majambazi South Afrika.

“Wote Alikiba na Barakah the Prince walikuwa pamoja na timu kwaajili ya mkutano wa utayarishaji kwenye ofisi zilizopo maeneo ya katikati za kampuni maarufu ya Afrika Kusini wanayofanya nayo kazi,” yamesema maelezo rasmi kutoka uongozi wa Rockstar4000.
“Wakati wakiendelea na mkutano, watu sita waliokuwa na bunduki walivunja kuta za jengo la ofisi hiyo na kuingia walipokuwa Alikiba, Barakah The Prince na wengine,” yamesema.

Thursday, July 14, 2016

Filamu 25 Za ZIFF Kutumika Kufundishia Mashule.

MKURUGENZI wa Tamasha la Ziff, Profesa Martin Mhando, amesema kwamba baadhi ya filamu katika tamasha la mwaka huu zitatumika kwa ajili ya kufundishia.

Shilole Ampata Mrithi Wa Nuh Mziwanda.

STAA anayebeba fani mbili kwa mpigo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, juzikati alimwanika bwana’ake mpya huku akijinadi kuwa ndiye mrithi halali wa aliyekuwa mpenzi wake wa kitambo, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’

Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni baada ya kubambwa kwenye Ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar es Salaam ilipokuwa ikifanyika Shoo ya Black Tie, Shilole alisema ameamua kubadili upepo na kuachana na mapenzi ya vijanahivyo ameangukia kwa mwanaume huyo ambaye ni mtu wa rika lake.
“Kusema kweli leo sitaki hata kupaparika maana nimekuja na mheshimiwa hivyo sitaki tena kuonekana kama mtoto mdogo humu ukumbini, angalia hata meza niliyokaa utagundua kuwa hapa ishu zote ni za kiutu uzima, siwezi tena kupaparika, ifikie muda tuheshimiane kwani njia pekee ya kujiheshimu ni kutoka na watu wenye msimamo wao nawatu wazima kama huyu.

Roma Mkatoliki Asema Babu Tale Alimchimba Mkwara.

Msanii Roma Mkatoliki ambaye leo ameachia ngoma yake mpya ‘Kaa tayari’ amefunguka na kusema moja ya mstari uliopo kwenye wimbo wake huo unamuhusu meneja wa Diamond Platnumz ambapo unamchana kuwa saizi anamganda sana Diamond Platnumz mpka amelisahau kundi lake na Tip Top Connection.

Siasa Ipo Kwenye Damu Yangu: Irene Uwoya

STAA mkali Bongo Muvi, Irene Uwoya amefunguka kuwa bado hajakata tamaa ya kuwa mwanasiasa japokuwa mwaka jana alishindwa lakini hiyo imempa nguvu ya kujipanga zaidi na kwamba kwa sasa akili yake yote akilala, akiamka ni kuwaza siasa tu.

Saturday, July 9, 2016

Mose Iyobo Ataka Aunty Ezekiel Achore Tattoo Ya Jina Lake.

Moses Iyobo ‘Moze’ ambaye ni mzazi mwenza wa staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson, amemwambia mpenzi wake huyo kuwa na yeye ajichore ‘tatuu’ ya jina lake kama ilivyokuwa kwa msanii Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kwa Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kabla ya kumwagana.

Mr.Blue Aikubali Couple Ya Diamond Na Zari.

Mr Blue amesema Diamond na Zari ndiyo couple anayoikubali zaidi.
“Ukinitoa mimi na Wahyda couple ambayo naipenda, naielewa ni Zari na Diamond,” Blue alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM.
“Yaani wanapendeza unajua eeh, na Mungu amewajaalia wamepata mtoto, wanashirikiana kama marafiki kwenye biashara, wanajua kucheza na akili za raia, wanaitengeneza couple yao ya kimapenzi, wanaifanya pia inakuwa kibiashara, yaani very nice,” aliongeza.

Mtitu Awachana Viongozi Wa Shirikisho La Filamu Tanzania.

DAIREKTA mwenye jina kubwa nchini, William Mtitu amefunguka kuwa kitu kinachoiangusha tasnia ya filamu Bongo ni uongozi wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), ambao umeshindwa kuwasimamia wasanii wake vizuri pamoja na kutengeneza mazingira mazuri ya kuwafanya wadau mbalimbali kuvutiwa na tasnia hiyo hata kuwekeza.

Bodi Ya Filamu Yahimiza Wasanii Wachanga Wasaidiwe.

Wito huo umetolewa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi.Joyce Fissoo jijini Dar es Salaam wakati akimkabidhi Bi Wakonta Kapunda Shilingi laki tano kwa ajili ya Safari ya kwenda Zanzibar kushiriki mashindano ya uandishi wa Muswada (Script).
“ Napenda kutoa wito kwa wadau wa sanaa kusaidia wasanii wanaochipukia kwani ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya sanaa nchini” Alisema Bi Joyce.

Sunday, July 3, 2016

Mimi Ni Dhahabu Kila Mtu Anataka Kuishika: Wema Sepetu

Wema  Sepetu, amesema yeye ni dhahabu inayogombewa na watu hivyo hajali hata kama atachafuliwa namna gani katika mitandao ya kijamii.

Wema aliliambia MTANZANIA kwamba, hana mpango wa kujibu vibaya vinavyoongelewa kuhusu yeye kwa kuwa yeye bado ni dhahabu inayotamaniwa kushikwa na kila mtu.