INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, March 21, 2016

Bongo Movie Wamtenga Lulu ?

Hali hiyo ya sintofahamu ilijidhirisha Jumanne iliyopita kwenye hafla ya kumpongeza Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam iliyoandaliwa na wasanii wa Bongo Muvi chini ya uratibu wake, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ katika Hoteli ya Rodizio iliyopo Masaki, jijini Dar.

Diamond Na Zari Wanataka Mtoto Mwingine.

STAA wa Bongo Fleva asiyechuja kwa takriban miaka 7 mfululizo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameeleza mikakati yake kuwa ana mpango wa kumpa mimba nyingine malkia wake wa nguvu, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Risasi Jumamosi linakuhabarisha.

JB Aanza Kushuti Tamthilia Yake Mpya.

Msanii mkongwe wa filamu na mtayarishaji, Jacob Stephen ‘JB’ amewataka mashabiki wa kazi zake za filamu kukaa mkao wa kula kwa ujio wa tamthilia yake mpya iitwayo ‘Kiu ya Kisasi’.
Kupitia instagram, JB ameandika:

Mashauzi Na Maringo Yanawapoteza Wasanii Wengi: Diamond Platnumz

Msanii Diamond Platnumz amefunguka na kusema wasanii wengi wa Tanzania na Afrika Mashariki kiujumla wanapotea kwenye ramani ya muziki sababu kubwa ni mashauzi na starehe na kutaka kujionesha.
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Diamond Platnumz amedai kuwa mafanikio yake kimuziki na kuzidi kuendelea kufanya vizuri ni kutokana na ukweli kwamba yeye si mtu wa starehe na wala si mtu wa mashauzi kutaka kufanya vitu ili kuwaonesha watu, bali yeye amekuwa akitunza pesa anazofanya na kufanya mambo ya msingi ndiyo maana labda anazidi kufanikiwa kimaisha pamoja na sanaa.

Diamond Platnumz Apewa Ofa Kujifunza Kijerumani Bure na Ubalozi Wa Ujerumani.

Diamond amesema angependa kujifunza kijerumani, hata hivyo ngekewa ilimdondokea baada ya ubalozi wa ujerumani nchini kumpa ofa ya kusomea lugha hiyo katika chuo cha Goethea Institut kilichopo Dar es salaam. Diamond alienda ubalozi wa ujurumani juzi wakati anaenda Ujerumani kwenye show. Angalia picha zaidi...

Chid Benzi Sio Wa Kuonewa Huruma Amevuna Alichokipanda: Faiza Ally

“Kila mtu anamsikitikia Chidi kwa nini? Chidi sio mtoto ni maisha aliyo chagua, pengine unaweza kumsikitia mtoto aliye jifunza akiwa chini ya miaka 18 lakini sio mtu mzima! Kila siku mifano tunaiona jinsi gani madawa yana haribu watu inaama hawaoni ? Hawasikii ?"

Wednesday, March 9, 2016

Sabby Angel Ampindua Jokate Kwa Ali Kiba ?

Mwigizaji wa sinema za Kibongo anayefanya vyema pia kwenye Muziki wa Mduara, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ amedaiwa kumpindua mwanamitindo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ kwa mpenzi wake, Ali Kiba ‘King Kiba’, Ijumaa Wikienda limenasa vielelezo vya ubuyu kamili.
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, Sabby amevamia penzi la Jokate na kuhakikisha anampa ‘vitu adimu’ Kiba kiasi ambacho mkali huyo wa Wimbo wa Lupela kuhamishia majeshi rasmi kwa mrembo huyo ambaye jina lake linazidi kushamiri siku hadi siku mjini.

Ndoa Ya Rayuu Yavunjika Baada Ya Kufungwa Ndani Ya Wiki Moja Tu.

Baada ya uvumi kuwa staa wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ ameachika kwenye ndoa yake ambayo imedumu kwa siku nne tu huku chanzo kikiwa ni familia ya mwanaume, hatimaye mashehe wameamua kuingilia kati kuinusuru ndoa hiyo.
Februari 26, mwaka huu, Rayuu alifunga ndoa na mwanaume mwenye asili ya Kiarabu, Ahmedi Said lakini siku ya nne baadaye ulienea ‘ubuyu’ mitandaoni kuwa alitwangwa talaka tatu kwa sababu ya skendo.
Kutokana na sekeseke hilo lililoacha historia ya kipekee, mashehe mbalimbali walidaiwa kuingilia kati na kuilaumu familia ya mwanaume huyo kuwa ilienda kinyume na matakwa ya Kiislam.

Tuzo Ya Lulu Yamliza Mama Kanumba.

Tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Filamu Afrika Mashariki, iliyotwaliwa na Mbongo,
chozi mama wa aliyekuwa nyota wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa, tambaa na Risasi Mchanganyiko liujaze moyo wako.
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na mama Kanumba, muda mchache baada ya Lulu kutangazwa na waandaaji wa tuzo ambao ni African Magic Viewers Choice ‘AVCA’ kwamba yeye ni mshindi, aliwasiliana na mama yake mzazi, Lucresia Karugila, ambaye naye alimtwangia simu mama Kanumba ili kumfahamisha ushindi huo ambapo mama huyo alitoa chozi.

Soko La Filamu Bado Lipo: JB

Muigizaji Jacob Stephen ‘JB’amefungyuka haya kuhusu soko la filamu na tasnia kwa ujumla.
’Nakataa soko la filamu halijafa,limesinzia na kuna sababu kubwa sana watu wengi hawajui kwanini imesinzia,filamu sasa hivi inatakiwa ipelekwe ‘next stage’ kitu chochote kikitakiwa kitoke hapo kilipo na kwenda sehemu nyingine kinakuwa kama kinakufa mf,kuna wakati Fulani Bongo Fleva walikuwa na hali kama ya kwetu lakini walivyoanza kurekodi kwenda Sauz Afrika na video kuwa bora ikaonekana kama imefufuka,maana yake ni kwamba Bongo Fleva ilitakiwa ipelekwe ‘next stage’, Alisema JB.

Sunday, March 6, 2016

Maharamia Wa Kazi Za Wasanii Watumbuliwa Majipu Kariakoo.

UNAPOSEMA Serikali ya awamu ya tano ilichoahidi lazima kifanyike ni kweli kabisa hivi karibu Mh. Nape Moses Nnauye alisema kuwa atahakikisha kuwa wale wanaojipatia fedha kwa njia za ujanja ujanja mwisho wao umefika lazima washughulikiwe kulinda maslahi ya Wasanii wa Tanzania.
Jana ilikuwa ni siku mbaya kwa wale wauuzaji wa filamu za nje baada ya Mamlaka ya Mapato (TRA) kutinga na Polisi kwa muuzaji mkubwa wa Dvd Fake Kariakoo mwenye mtaji mkubwa ajulika naye kwa jina la Palasi na kukamata kazi fake zote na kuzipakia katika Gari.

Lulu Na Richie Watamba Tuzo Za Africa Magic Viewers Choice Awards 2016.

Usiku wa jana Tanzania imeingia kwenye headlines tena baada ya waigizaji wa Tanzania kuchukua Tuzo Africa Magic Viewer’s Choice Awards 2016 zilizotolewa Lagos Nigeria ambapo mwimbaji tokaTanzania Alikiba  alikuwa mmoja kati ya wasanii waliotumbuiza kwenye tuzo hizo.

Thursday, March 3, 2016

TAFF Yaunganisha Tasnia Ya Filamu Nchini.

SIKU za nyuma kulikuwa na malumbano makali kati ya shirikisho la filamu Tanzania (TAFF) na kundi la Bongo Movie Unity lilokuwa likiundwa na wasanii nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood na kuleta sintofahamu .
Lakini kutokana na juhudi za Mwakifwamba pamoja na makamu mwenyekiti wake Deosonga Njerekela wamefanikiwa kuwaunganisha na sasa ni kundi moja wanaongea lugha moja kufuatia vikao vya upatanishi vilivyofanyika miezi ya awali mwezi wa kwanza hadi wa pili Taff inapata nguvu zaidi baada ya kuwapa nafasi na wasanii kutoka Bongo movie kushika hatamu za uongozi na kuwa sasa ni shirikisho kamili lenye sura zote hongera.

Shamsa Ford Aendelea Kumkumbuka Lowasa.

Msanii wa filamu nchini na aliyekuwa akitoka kimapenzi na msanii Nay wa Mitego amefunguka na kusema kuwa bado aliyekuwa mgombea wa urais nchini mwaka jana kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo yupo moyoni mwake.
Kupitia Account yake ya Instgram Shamsa Ford alipost picha ya Mh Edward Lowassa na kusema ni kumbukumbu yake lakini siku zote atakuwa na nafasi moyoni mwake.