INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, December 26, 2013

HATIMAYE CHUCK NORRIS AJIBU MAPIGO YA VAN DAMME KWA KUTENGENEZA TANGAZO LA KUSIMAMA JUU YA NDEGE 2 LENYE MFANO WA MTI WA CHRISMASMara ya kwanza muigizaji mkongwe Jean-Claud 'Van Damme' alipotengeneza tangazo la Volvo kusimama katikati ya magari mawili makubwa ya Volvo juu ya side mirrors,mguu wa kushoto ukiwa kwenye gari moja na wa kulia kwenye lingine habari iliwashangaza watu wengi sana huku wengi wakijiuliza maswali.

VIN DIESEL ATANGAZA RASMI TAREHE YA KUACHIA FILAMU MPYA 'FAST AND FURIOUS 7'

Baada ya kusimamisha shughuli za maandalizi ya muendelezo wa saba ya Filamu ya Fast and Furious kutokana na kifo cha muigizaji 'Paul Walker aliyefariki mwishoni mwa mwezi uliopita kwa ajali ya gari.

Leo Desemba 23 Muigizaji na mkuu wa filamu ya Fast na Furious,Vin Diesel ametangaza rasmi tarehe ya kutoka kwa muendelezo wa saba wa filamu hiyo yenye mafanikio makubwa.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Diesel ameweka picha akiwa na Paul Walker na kuandika kuwa hiyo ilikuwa scene yao ya mwisho kuwa na staa huyo na kutangaza rasmi kuwa Fast and Furious sehemu ya 7 itatoka April 10 mwaka 2015.
“The last scene we filmed together…

There was a unique sense of completion, of pride we shared… in the film we were now completing… the magic captured… and, in just how far we've come… Fast and Furious 7 will be released… April 10th 2015! P.s. He'd want you to know first…,” ameandika Diesel.

Tuesday, December 17, 2013

BIFU KATI YA HEMED NA MLELA GUMZO JIJINI DARHemed (kushoto) akimtishia bastola Mlela

Hemed na Mlela wakiwa wamelazwa hospitalini baada ya kuumizana huku mama yao akiwaangalia kwa huzuni


Kasha la filamu mpya ya bifu la kina Mlela na PHD inayotarajiwa kuingia mtaani keshokutwa Jumatano. LILE bifu lililowahi kufukuta kwa kasi mithiri ya moto wa kifuu baina ya ‘tozi’ wawili ndani ya tasnia ya filamu, Hemed Suleiman ‘PhD’ na Yusuf Godfrey Willard Mlela ‘Mlela’ linadaiwa kuibuka upya na kuzidisha uhasama baina ya wasanii hao. Aidha, alisema bifu hilo lilidhihirika hivi karibuni wakati wawili hao walipokutanishwa kuigiza filamu moja, kwani mara kwa mara walijikuta wakifanya kweli kwenye baadhi ya vipande vya ugomvi na mapigano jambo lililompa wakati mgumu muongozaji wa filamu hiyo inayotarajiwa kuingia sokoni kuanzia Desemba 18 mwaka huu iliyopewa jina la I Know You. “Walikuwa na muda mrefu sana bila kukutana, tukadhani bifu lao halipo tena, lakini hivi karibuni walikutana kwenye filamu iliyoandaliwa na Mtitu Game 1st Quality, wakawa wanafanya kweli kwenye baadhi ya sehemu za majibizano na mapigano huku wakifanyiana fujo mbalimbali huku kupigana vijembe vya wazi,” alisema rafiki huyo. “Ni kweli tulikuwa na utofauti, ule mvutano wa zamani bado ulikuwepo, kila mmoja hakutaka kuwa dhaifu kwa mwenzake, utaona baadhi ya vipande tulivyofanya kweli,” alisema Mlela ambapo simu ya Hemed iliita bila kupokelewa licha ya mwandishi wetu kuipiga mara kwa mara. Naye Meneja matayarishi wa Kampuni ya Game st Quality Ltd, Noel Amani ‘Futo’ alisema filamu ya I know You iliwapa wakati mgumu sana kutokana na bifu la wasanii hao kuonekana waziwazi. “Walitumbua sana, kuna wakati walifokeana kweli, kukunjiana ngumi hata hivyo kuna baadhi ya vipande walivyofanya kweli tumelazimika kuviacha ili kuleta uhalisia zaidi. Kila mmoja anaamini yuko juu ya mwenzake,” alisema Futo.

Wednesday, December 4, 2013

MTUNIS:WHO'S BAD NDIO FILAMU YANGU YA KUFUNGIA MWAKA 2013

Mtayarishaji na Muigizaji wa filamu Nice Mohamed ‘Mtunis’amesema kwamba filamu yake ya Who’s Bad itakuwa kazi yake ya kufungia mwaka kwa kuzima kazi nyingine za filamu zilizoingia pamoja na filamu hiyo ambayo inafanya vizuri sokoni baada ya kuingia mitaani hivi karibuni.

“Kama ambavyo wengi wamenizoea ninapotoa kazi inakuwa ni bora na lazima ikimbize sokoni, sinema yangu ya Who’s Bad itafunga mwaka kama kazi bora nakuwa makini sana katika utengenezaji wa filamu na ndio kilichofanyika katika filamu hiyo wasanii wamekamua sana na kuonyesho uwezo wa hali ya juu,”anasema Nice.

Filamu hiyo imeshirikisha wasanii kama Patcho Mwamba na washiriki wengine wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu, Mtunis amekuwa akifanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo kazi alizofanya ni kama Bar mead, Who’s Bad,Clinic Love na kusambazwa na kampuni ya Steps Entertainment.

Monday, November 25, 2013

ILE FILAMU MLIYOKUWA MKISUBIRI YA JICHO LANGU ITAKUWA SOKONI TAREHE 24.12.2013. JIPATIE NAKALA YAKO

Tunafunga mwaka na filmu mpya ya JICHO LANGU kutoka katika kampuni ya J-Film 4 Life. Ikifika tarehe 24.12.2013 jisogeze taratibu katika duka lililo karibu nawe ujipatie nakala yako ya JICHO LANGU. 

Thursday, November 21, 2013

PICHA NYINGINE ZA MUONEKANO MPYA WA VICENT KIGOSI "RAY"s

 


KAJALA KESI UPYAAA..MUMEWE AMPONZA

 

Bado bundi anamnyemelea staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja baada ya kurejeshwa kortini kwa mara nyingine huku kesi ikimjia upya.
MUME AKATA RUFAA

Pamoja na kutoa faini ya Sh. milioni 13 alizolipiwa na staa mwenzake wa filamu, Wema Isaac Sepetu, Kajala anatarajiwa kuhukumiwa tena Novemba 25, mwaka huu baada ya mumewe, Faraji Agustino Chambo kukata rufaa katika mahakama kuu.
Kwa mujibu wa jaji aliyezungumza  kuna kila dalili wawili hao wakaachiwa huru au wakafungwa tena kwa adhabu kubwa zaidi ya ile ya awali, hivyo huu ni msala mpya kwa Kajala ambaye tayari alikuwa uraiani.
Kesi iliyokuwa ikiwakabili wanandoa hao ilihusiana na utakatishaji wa fedha haramu uliofanywa na mume wa Kajala wakati akifanya kazi kwenye Benki ya NBC, Dar.
Mume wa staa huyo ndiye anadaiwa kukata rufaa wakati akitumikia kifungo cha miaka saba jela baada ya kukutwa na hatia.
 
Habari za ndani zilieleza kwamba, Kajala alisharidhika na hukumu iliyotolewa Machi 25, mwaka huu ambapo yeye  alitakiwa kufungwa mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni 13.
Katika hukumu hiyo, mume wa Kajala alifungwa miaka saba na ndipo alipoamua  kukata rufaa na akamuingiza Kajala kwa maelezo kuwa wote hawakuridhishwa na hukumu iliyotolewa mwanzoni.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Kajala, staa huyo amekuwa katika wakati mgumu na mara nyingine na kujikuta akiangua kilio hasa anapokumbuka maisha ya gerezani.

KAJALA KORTINI

Ili kuthibitisha habari hizo, juzi (Jumatatu) Kajala akiwa na shosti wake, Wema anayehaha kumnasua, alipigwa chabo na mashushushu wetu wakitinga tena katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Habari zilieleza kuwa jaji ambaye alikuwa akipitia ya hukumu ya awali ya wanandoa hao, alidai kwamba  Jaji Temba aliyetakiwa kutoa hukumu ya kesi hiyo upya alikuwa anaumwa.

HUKUMU NOVEMBA 25

Kufuatia kuumwa kwa hakimu huyo, kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 25, mwaka huu, ambayo itakuwa siku ya hukumu huku ikielezwa kuwa kila kitu kipo tayari.
Akiwa katika viunga vya mahakama hiyo, Kajala alionekana mwenye wasiwasi na woga kwa sababu hakuwa anajua kama anaweza kuburuzwa kortini kwa mara nyingine kuhusiana na suala hilo kwa kuwa aliamini alishamaliza kwa kulipa faini ya Sh. milioni 13 kisha kurejea uraiani huku mumewe akienda jela.
 
Kajala alisema anaomba Mungu ili kikombe hicho kimuepuke kwani alishasahau kama anaweza kurudi kortini.
“Sikudhani kwa kweli kama ninaweza kurudi mahakamani, Mungu anisaidie kwa kweli…” alisema Kajala.
 
Naye Wema alipigwa na mshangao baada  ya kuona kesi hiyo imeibuka tena.
“Siku ile niliuliza kilikuwa kinahitajika nini ili Kajala awe huru, nikaambiwa milioni 13, nikatoa, sasa iweje tena arudishwe mahakamani?” alihoji na kuonesha wasiwasi mkubwa baada ya kuambiwa  kuwa Kajala anaweza kufungwa kwa kuwa hukumu inapitiwa upya.
Wakili wa Kajala, Peter Kibatala alisema anapambana kunyoosha sheria kuhakikisha mteja wake anakuwa huru.


Read more: http://www.vitukovyamtaanews.com/2013/11/kajala-kesi-upyaaamumewe-amponza.html#ixzz2lINJMHYr

Tuesday, November 19, 2013

JENNIFER KYAKA (ODAMA) AFIWA NA BIBI YAKE MZAA BABA YAKE SYMPHOROSA KOKUTONA


Hiki ni kipindi cha majonzi kwa familia yetu kwa kupotelewa na mmoja wa wanafamilia  Symphorosa Kokutona ambaye alikuwa kipenzi chetu kipindi yupo hapa duniani. Amekuwa msaada mkubwa katika maisha yetu hasa kwa ushauri wake ambao umetuwezesha kufika mahali hapa tulipo. Tunasikitika sana na kifo chake kilichotokea jana huko Bukoba katika kijiji cha Kilimilile na mazishi yanafanyika leo
MUNGU AMULAZE MAHALI PEMA PEPONI...AMINA

Monday, November 18, 2013

ANITA KYAKA NA JAMES WAFUNGA PINGU YA MAISHA TAREHE 16.11.2013 KATIKA KANISA LA AICT MAGOMENI

Siku ya Jumamosi 16/11/2013 ilikuwa ni siku ya pekee kwa wapendanao, James na Anita Kyaka kufunga pingu ya maisha katika kanisa la AICT Magomeni. Wanandoa hawa walimshukuru Mungu kwa yale yote ambayo amefanya katika kufanikisha lengo lao la kuachana na ukapela na kuingia katika maisha mapya ya mume na mke. Pia waliwashukuru wazazi wao ambao wamewalea mpaka kufikia hatua hii waliyofikia. Anita na James waliwashukuru pia ndugu na jamaa zao waliowatia moyo katika kipindi walichokuwa wakipitia wakati wa uchumba wao na mpaka sasa wanaitwa Bwana na Bibi.

Shukrani zingine zilimfikia dada yake kipenzi Jennifer Kyaka (ODAMA) kwa yale yote aliyoyafanya kuhakikisha shughuli inaisha salama.

Shughuli ilianza katika kanisa la AICT Magomeni, baada ya hapo zoezi lilihamia katika viwanja vya Lamada ambapo wanandoa, jamaa na marafiki waliweza kupiga picha za kumbukumbu na mwisho wa siku gurudumu lilielekezwa katika ukumbi wa PICOLO BEACH MIKOCHENI ambapo watu waliweza kujiachia na kufurahia siku ya kipekee ya Anita na James.

Tuone baadhi ya matukio yaliyoajili.

Picha zimepigwa na RUMAFRICA +255 715 851523

KIPINDI CHA KUINGIA KANISANI
Wakiingia kanisani
James na Anita wakiingia kanisani


Fuuul kupendeza

MCHUNGAJI AKIFANYA MAOMBEZI NA KUBARIKI NDOA HII

Mchungaji akiwaombea wanandoa


 Wa pili kutoka kulia ni mzazi wa Bwana harusi James

KIPINDI CHA KUSIKILIZA NENO LA MUNGU KUTOKA KWA MCHUNGAJI
 Kutoka kulia ni wazazi wa Bibi harusi Anita Kyaka

 Anita Kyaka (Mrs James)

Kulia ni James akiwa na best man wake

 Mdogo wake na Anita Kyaka aitwae George Kyaka
 Jennifer Kyaka (Odama)
 Odama akiwa na mdogo wake wa mwisho kulia
 Odama akiwa na mdogo wake wa mwisho Albert Kyaka

 Kulia ni mjomba wake na Bwana harusi James


KIPINDI CHA MZAZI WA BWANA HARUSI KUMRUHUSU MWANAE KUMPOKEA MKE WAKE (ANITA KYAKA) RASMI...KANISANI
Mamamzazi wa Bwana harusi, James


 Bibi wa Bibi harusi Anita Kyaka

KIPINDI CHA WAZIZI WA BIBI HARUSI KUTOA NENO KWA MAHARUSI

 Wazazi wa bibi harusi, Anita Kyaka
Mchungaji akiwapa mkono wa baraka wazazi wa bibi harusi baada ya wosia wao

KIPINDI CHA KUVISHANA PETE
KIPINDI CHA KUTIA SAINI KATIKA VYETI VYAO VYA NDOA
 James akiweka saini
Anita akiweka saini
KIPINDI CHA KUTOKA KANISANI NA KUELEKEA LAMADA KWAAJILI YA PICHA ZA KUMBUKUMBU
KIPIDI CHA KUPIGA PICHA ZA KUMBUKUMBU KATIKA LANGO KUU LA KANISA


Wakiwa katika mlango mkuu wa kutokea wakipiga picha za pamoja na ndugu na jamaa zao
 Kushoto ni dada yake Anita Kyaka akiwa na mdogo wake George Kyaka
 Odama akiwa na wadogo zake..kulia ni George na kushoto ni Albert
Odama akiwa na wazazi wake


MAHARUSI  WAKIWA KATIKA ENEO LA LAMADA KWA PICHA ZA KUMBUKUMBU

 Maharusi wakiwa na wazazi pamoja na ndugu wa upande wa Anita Kyaka
 Madada na baadhi ya ndugu wa bibi harusi
 Kulia ni mdogo wake Anita Kyaka (Joan Kyaka) akiwa na rafiki yake

UKUMBINI
 Wa kwanza ni mama mzazi
Kutoka kulia ni Zungu, dada yake na Anitaka Kyaka, Joan Kyaka na rafiki yake Joan Kyaka wakiingi ukumbini


 Jennifer Kyaka (Odama) dada wa Anita Kyaka
 Joan Kyaka mdogo wake na Anita KyakaKIPINDI CHA MAHARUSI KUSALIMIANA NA NDUGU NA JAMAA

 Anita Kyaka akisalimiana na mama mzazi wa mume wake James

 James akisalimiana na mama yake mzazi.

 James akisalimiana na baba mzazi wa mke wake Anita Kyaka

KIPINDI CHA KUBURUDIKA NA MUZIKI

KIPINDI CHA KUPIGA PICHA ZA PAMOJA NA VIKUNDI MBALIMBALI
 Hawa ni ndugu wa upande wa James
 Bibi mzaa mama wa Anita Kyaka
 Bryan mtoto wa dada yake na Anita Kyaka

 Odama dada yake na Anita Kyaka


Wazazi wa Anita Kyaka wakiwashukuru wale wote waliofika na kutoa ujumbe kwa wanandoa hawa...

George Kyaka akiwa na dada yake

KIPINDI CHA KULISHANA KEKI KILIFIKA

KIPINDI CHA MISOSI KILIFIKA..WATU WEWEEEEEEE...!!!!

 KIPINDI CHA SHAPENI KILIFIKA


KIPINDI CHA KUTOA ZAWADI KILIFIKA


KIPINDI CHA KUPIGA PICHA ZA PAMOJA NA VIKUNDI MBALIMBALI, NDUGU NA JAMAA
Ndugu upawa mume


KWAHERINI JAMANI NA MUNGU AWABARIKI SANA

Picha zimepigwa na
RUMAFRICA
+255 715 851523
www.rumaafrica.blogspot.com