INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, March 21, 2016

JB Aanza Kushuti Tamthilia Yake Mpya.

Msanii mkongwe wa filamu na mtayarishaji, Jacob Stephen ‘JB’ amewataka mashabiki wa kazi zake za filamu kukaa mkao wa kula kwa ujio wa tamthilia yake mpya iitwayo ‘Kiu ya Kisasi’.
Kupitia instagram, JB ameandika:

Wapenzi wa Jerusalem nilikuwa sijawapa habari ya kazi tunayoendelea nayo sio filamu bali ni tamthilia. Inaitwa Kiu ya Kisasi. Ningependa wapenzi wangu wote muione kazi hii. Tatizo ni runinga gani mko wengi. Tayari tumeanza mazungumzo na runinga nyingi zilizoonyesha nia ya kuirusha lakini tutaangali wapi tutalipwa vizuri, na wapi wapenzi wetu mko wengi…nawapenda.
Katika post nyingine aliandika:
Ratiba yetu wapenzi wa Jerusalem Films tunaendelea kuchukua picha za tamthilia yetu ya Kiu ya Kisasi hadi mwezi tano. Lakini mwezi huo wa tano tuta achia filamu ya ‘Kalambati Lobo’ ambapo tumecheza mimi JB na Diana Kimaro. Kisha itakuja Chale Mvuvi, amecheza Shamsa Ford na Haji Adam, halafu mwezi wa tano nitaingia tena kazini kufanya ile movie yangu na King Majuto….nawapenda.

No comments:

Post a Comment