INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, March 20, 2014

NI MATUMIZI MABOVU YA AKILI KWA MSANII KUWA BUSY NA SKENDO BADALA YA KAZI

Swahiliworldplanet ilipata nafasi ya kuzungumza machache na star wa filamu nchini Salim Ahmed "Gabo Zigamba" kuhusiana na kazi zake za filamu na maisha binafsi hivi juzi kati. Gabo ambaye kipaji chake cha kuigiza hakijifichi huku akiwa tayari amejizolea mashabiki wengi alitiririka kama ifuatavyo katika interview hii ndogo.

SWP: Nani alikushawishi kuingia kwenye sanaa ya uigizaji?

GABO: Ni msukumo wa maisha baada ya plan A na mtazamo wa ndugu jamaa na marafiki

SWP: Umefaidika na nini mpaka sasa tangu uanze kuigiza filamu?

GABO:  Kwa upande wa mafanikio bado naidai sanaa

SWP:  Kitu gani huwa kinakukera zaidi unapokuwa location?

GABO: Kero kubwa ni mijadala ya pre-production ndani production....

SWP: Baadhi ya waigizaji nchini wapo busy kutengeneza skendo ili kuandikwa kwenye media huku kazi zao zikiwa chache na bado haziridhishi je unalizungumziaje hilo?

GABO:  .Ni matumizi mabovu ya akili huwezi kuwa busy na skendo ikiwa huna kaz miliki.....

SWP:  .Umeoa au una mchumba?

GABO:  Nina mke na mtoto mmoja

SWP:  Nini matarajio yako ndani ya miaka 3 ijayo kuanzia sasa?

GABO: Kufanya sanaa kimataifa

  Kwa upande mwingine filamu mpya ya JICHO LANGU aliyoigiza Gabo, Odama na Thadeo Alexernder itaingia sokoni tarehe 31 mwezi huu wa tatu hakikisha unanunua nakala yako hali ya filamu hii mpya kali.

No comments:

Post a Comment