INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Saturday, October 24, 2015

Rais Wa TAFF Simon Mwakifwamba Awavaa Wasanii Wa Filamu.

RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba amewatemea cheche wasanii na kuwataka kuachana na kuendekeza kupokea fedha za wanasiasa tu bila kutetea masilahi yao.

Akistorisha na paparazi wetu, Mwakifwamba alisema kwa sasa tasnia ya filamu imekufa kabisa hivyo wasanii wanaopata nafasi ya kuzunguka na wagombea urais wawe wanawaambia na matatizo waliyonayo kuliko kuishia kuchekelea fedha wanazopewa na kusahau kazi yao ilivyo na changamoto nyingi.
“Kama wanalipwa ni jambo zuri sana lakini pia watumie fursa hiyo kutetea masilahi ya tasnia wasijisahau kutokana na fedha wanazopata kwani uchaguzi utaisha na maisha yataendelea,” alisema Mwakifwamba.
Chanzo:GPL

No comments:

Post a Comment