INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, October 22, 2015

Natamani Sana Kupata Mtoto: Jackie Pentezel

Msomaji: Mbali na sanaa unafanya shughuli gani?
Jack Chuz: Nina saluni yangu Sinza na duka la nguo. Pia ni mtaalam wa kusuka na make up.
Msomaji: Nasikia bila ndumba huwezi kukubalika kwenye sanaa, unaliongeleaje hilo?
Jack Chuz: Si kweli, uzuri wa kazi zako ndiyo uchawi wako.
Msomaji: Mumeo (Gadner) ni Muislam na dini inamruhusu wake wanne akitaka kuoa tena utafanyaje?

Jack Chuz: Nitakubali sababu dini inaruhusu ila asije kwa pupa huyo mwanamke tutakosana.
Msomaji: Nilisikia mumeo kakupa talaka tatu, ni kweli?
Jack Chuz: Hakuna kitu kama hicho ni uzushi tu.
Msomaji: Kwa nini mastaa hampendi kuwasaidia chipukizi?
Jack Chuz: Mbona nawasaidia sana tu. Lakini wakati mwingine utakuta mtu anaandaa filamu yake na kuweka chipukizi watupu na hapohapo anahitaji nishiriki katika filamu yake ambayo staa ni mimi peke yangu na hapo nitokee kwenye kava na huwa nafanya hivyo.
Msomaji: Kwa nini kila kukicha unazushiwa ndoa yako kuvunjika na nini siri ya kudumu?
Jack Chuz: Watu wenye chuki ndiyo wanazusha na siri ya kudumu ni maelewano tu, watu wamezoea  kuwa mastaa wengi hawatulii kwenye ndoa.
Msomaji: Tangu umeanza sanaa, umepata mafanikio gani?
Jack Chuz: Kikubwa umaarufu ila kwa maendeleo bado.
Msomaji: Nilisikia hutaki kuzaa na mumeo eti kwa sababu bado unakula ujana na ukipata mimba unatoa?
Jack wa Chuz: Si kweli, natamani kuzaa na mume wangu hata leo. Hakuna kitu kinachoniumiza kila siku kama hicho na kama ipo hospitali inayoweza kunisaidia nitashukuru sana.
Msomaji: Ukikumbuka skendo zako za nyuma unajisikiaje?
Jack Chuz: Huwa naumia sana na kuna kipindi natamani hata nizaliwe upya. Kwa sasa ni Jack mpya kabisa si wa zamani.
Chanzo:GPL

1 comment:

  1. Mungu ni mweza yote, swali la mtoto ni ndogo sana,jiweke mikononi mwake kila kitu kitafunguliwa bila Shaka, Mungu atakujibu!

    ReplyDelete