INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Saturday, October 24, 2015

Kifo Cha Deo Filikunjombe Kimenihuzunisha Sana: Cathy Rupia

Muigizaji wa muda mrefu, Sabrina Rupia ‘Cath wa Mambo Hayo’,  amekiri kuumia vibaya kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe kutokana na ukaribu wao na jinsi alivyokuwa na moyo wa kuwajali wengine.
Akizungumza kwa uchungu na mwandishi wetu kwa njia ya simu kutoka Ludewa alikohudhuria mazishi ya mbunge huyo, Cath alisema maumivu aliyonayo kamwe hayasimuliki na kwamba itamchukua muda mrefu kumsahau Deo na kwamba ataendelea kumuombea kwa Mungu, ampumzishe kwa amani.
“Nina maumivu makali, moyo wangu umegubikwa na simanzi isiyo na kifani, kama unavyojua, Deo alikuwa mpambanaji wa kweli, hakusita kutetea maslahi ya wananchi wa Ludewa na taifa kwa ujumla, itanichukua muda mrefu kumsahau, familia zetu ni za karibu mno,” alisema Cath.
Chanzo:GPL
23.10.2015 -  Tags: 

No comments:

Post a Comment