MSANII anayetokea mkoani Ruvuma ambaye kwa sasa a ametengeneza jina kupitia tasnia ya filamu Rachel Haule ‘Recho’, amebainisha kuwa tasnia hiyo ndiyo iliyombandilisha kimavazi tofauti na alipokuwa anatoka kijijini kwao Songea.
Mwandishi wa mtandao huu alitaka kujua anazungumzia vipi juu ya skendo kadhaa zilizokuwa zinaelekezwa kwake kuwa anavaa mavazi ya kichokozi, ambapo alidai kuwa baada ya kuingia mjini kitambo kidogo alijikuta akitekwa na mji lakini alikuja kucharuka zaidi baada ya kuanza kujuana na wasanii wa bongo muvi ambao mara zote walimshauri kuvaa nguo fupi ili kuleta mvuto zaidi.
Aliongeza kuwa inawezekana yeye akajiona hana matatizo lakini kwa sababu tasnia hiyo ya bongo muvi inaonekana kuwa na matatizo mengi basi hata yeye watu wanamuona ana matatizo hayo ya watu wengine na hawezi kukataa kwa sababu tayari yupo kwenye chungu hicho kimoja.
“Si kwamba nilitaka kuharibiwa hapana yani nilijikuta tu napenda kuvaa mavazi ambao rafiki zangu wanavaa na kadri siku zilivyokuwa zinaenda nilizidi kuzoea” alisema.
Hata hivyo msanii huyo kwa upande wa filamu alidai kuwa zimeweza kumtangaza kwa namna moja ama nyingine na anaamini ataweza kufika mbali zaidi na kujitangaza kimataifa.
Source mpekuz
No comments:
Post a Comment