INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, September 10, 2012

NDOA YA MTITU YAGHARIMU 25 MIL

 
 William Mtitu.

MSANII wa kiwanda cha filamu Bongo, William Mtitu anayetarajia kufunga ndoa Jumamosi ijayo, ametoa ripoti kuwa, bajeti ya harusi yake itakula kiasi cha  Sh. milioni 25 za Kitanzania.
Akichezesha taya na paparazi wetu, jana Jumatano jijini Dar, Mtitu alisema mpaka sasa kamati ya harusi yake imefanikiwa kukusanya mkononi Sh. milioni 16 huku watu mbalimbali wakiendelea kuahidi na kutoa.
Alisema ndoa yake hiyo itakayofungwa katika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph lililopo Posta, Dar, itafuatiwa na sherehe ya kukata na mundu kwenye Ukumbi wa Urafiki-Ubungo ambapo mavazi yatakayovaliwa na waalikwa ni ya kawaida.

No comments:

Post a Comment