INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Tuesday, September 18, 2012

J-FILM 4 LIFE INAKUPA POLE STEVE NYERERE KWA KUFIWA NA MWANAO



Mchekeshaji aliyejizolea umaarufu nchini kwa kumuigiliza hayati Baba wa Taifa, Steve ‘Nyerere’ Mangere amefiwa na mtoto wake.

Kwa mujibu wa majirani zake, mtoto huyo wa kiume amefariki baada ya kuishi kwa siku mbili tangu azaliwe.
Huyo ni mtoto wa pili kufariki kwenye familia ya Steve na mke wake aitwaye Zawadi.
“Sababu za kifo cha kwanza sijakijua, ila huyu wanasema atakuwa alivutwa wakati wa kuzaliwa, maana mtoto alikuwa mkubwa mno, sijajua ni kilo ngapi,” kilisema chanzo hicho kilicho jirani na Steve.
“Wa kwanza alifariki, wa pili yupo na huyu wa tatu amefariki.”
Kwa mujibu wa chanzo hicho, mazishi ya mtoto huyo yalifanyika jana.
Bongo5 inampa pole Steve kwa msiba huo.

No comments:

Post a Comment