INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, September 10, 2012

JACK WA CHUZI NA JINI KABULA WAFUMWA NDIVYO SIVYO
Kwa muda mrefu waigizaji wa kike wa Bongo Movies, Jack Pentzel na Miriam Jolwa aka Jini Kabula wamekuwa wakisakamwa na skendo ya usagaji kutokana na picha iliyosambaa kwenye mtandao inayowaonesha wakibusiana.


Hata hivyo wote wameendelea kukanusha kutojihusisha na vitendo hivyo kwa kudai kuwa walikuwa kazini.

Akiongena na kipindi cha Tagz Weekly cha DTV, Jack amesema hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Miriam kwakuwa zile ni picha zilizochukuliwa wakati wakishoot movie.


“Mi mwenyewe nimezisikia kama wewe ulivyozisikia, lakini ukweli ni kwamba mimi ni msanii, ni msanii wa filamu nafanya kazi za kuelimisha jamii, kwamba jamii ntaifundisha kwamba ifanye hivi ntaikosoa ifanye hivi.  

Kwahiyo zile ni picha ambazo zilipigwa wakati tupo location, na sio kwamba zile picha walizoziona wao ndio kile kitu sisi tulichokuwa tunakifanya. Sisi tulikuwa tunaigiza, hakuna uhalisia wowote wa kitu tulichokuwa tunakifanya”, alisema.

“Mimi nina mtu wangu, mimi nina mpenzi wangu, kwanza siwezi kuwa na mahusiano na mwanamke mwenzangu, kwasababu atanifanya nini mpaka mimi niridhike?”.Aliongeza
 

Kwa upande wake Miriam, naye alikanusha kuwa na uhusiano na mwanamke mwenzake na kusisitiza kile alichokisema mwenzie.

“Ni kweli hizo picha zipo, lakini sio kama namaanisha mimi na Jack Pentzel tulikuwa tunafanya huo uchafu. Hiyo ni movie tulikuwa tunacheza, mimi nilikuwa kama namuapproach Jack, yaani mimi ndio yule mwanamke msagaji halafu yeye ndio demu wangu. Na hiyo movie sijui kwanini inachelewa kutoka,” alisisitiza Miriam.

No comments:

Post a Comment