INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, September 10, 2012

SNURA AJUTA 'KUMDISS' WEMAMUDA mchache umepita tangu msanii wa filamu bongo, Snura, kutangaza kuachana na rafiki yake kipenzi Wema Sepetu, sasa anaonekana kujirudi na kudai kuwa kuna vitu ameanza kuvimisi kutoka kwa mwanadada huyo ingawa anaona aibu kumuomba msahama na arudi tena kundini.

Mtandao huu  
ulimtafuta Snura kuzungumzia kwa ufupi kuhusiana na urafiki wake wa awali na Wema, ndipo alipofunguka kuwa vipo vingi na anaona haya kumuomba msamaha ili arundi tena kundini kwani anaamini akifanya hivyo watu watapata la kusema.

“Kuna vitu nimevimisi kuvifanya ambavyo nilikuwa nafanya pindi nilipokuwa na Wema, nilikuwa na hamu ya kuzungumza naye lakini naona kama nitawapa watu ncha kusema kitu ambacho sioni kama ni kizuri kwa wakati huu,”
alidai.

Hata hivyo mtandao huo ulitaka kujua ni vitu gani alivyovimisi kutoka kwa Wema ambavyo yeye mweneywe hawezi kuvifanya, na alidai kuwa kutoka usiku na kuingia sehemu viwanja vikubwa vikubwa vya starehe ambazo huingia watu wazito ni moja ya kitu ambacho anahisi atavikosa kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment

There was an error in this gadget