INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Friday, July 10, 2015

Wasanii Wanapodai Hakutatokea Rais Kama Kikwete !

Naipenda sana sanaa but bado sijawaelewa baadhi ya wasanii wa Tanzania wanavyoshupalia eti hawadhani kama atatokea Rais kama Kikwete ! kisa tu walikuwa wanapiga nae picha na kualikwa ikulu mara kadhaa. Hivi hatuoni uchumi wa Tanzania ulivyodhorota na maisha kupanda sana katika utawala wa Rais Kikwete na mengine kibao. Yes ana mazuri yake machache na udhaifu wake kama binadamu wengine but To me Benjamin Mkapa was better than Kikwete coz yeye pia nimeshuhudia utawala wake tayari nikiwa najitambua ingawa sanaa wakati wa mkapa haikuwa katika kizazi cha leo , time changes and changes are inevitable in any society.
Utasema rais anaipenda sanaa na ameweka msingi mzuri wa sanaa nchini wakati hata Television ya taifa haiwalipi vizuri wasanii wala kupromoti vizuri sanaa ya Tanzania badala yake imekalia kutafsiri kazi za China na Korea na kuzionyesha kwa kiswahili. Je hapo utasema ni kukuza sanaa ya Tanzania au kukuza sanaa za mataifa mengine na kupromote tamaduni zao badala ya sisi kuwekewa msingi mzuri to promote tamaduni zetu za kimasai na kihadzabe kupitia filamu zetu ili mataifa mengine yavutiwe kutafsiri kazi zetu kwa lugha zao na kutangaza taifa, urithi na utamaduni wetu.
Wasanii mtambue kuwa bila uchumi imara na uongozi imara hata hiyo sanaa kupiga hatua kama mataifa makubwa ya wenzetu ni vigumu sana. Ukuaji wa sanaa unategemeana kwa ukaribu na sectors nyingine nyingi tu so kama hizo sectors zimepuuzwa au hazijawekewa mikakati imara hata huyo rais akiwa mpenda sanaa ni kazi bure kwani atafanya mambo mdo mdo not systematically and strategically kama tulivyoshuhudia mara leo katoa studio, mara leo kamsaidia msanii yule mara kesho yule lakini wakati huo huo serikali yake ikiwa imeshindwa kuweka msingi imara wa sector ya sanaa nchini.
Chuo kama UDOM kimeanzishwa katika utawala wake kilitakiwa angalau kiwe mfano wa kuigwa katika ukuzaji wa sanaa nchini but msanii ku-shoot tu pale ni ndoto kama kuingia Hollywood na bado eti kinafundisha sanaa !. Vyuo vya sanaa bado ni vichache sana, Vifaa vya kutosha na vya kisasa hakuna walimu na wakufunzi bobezi hakuna waliokuwepo wanagusagusa tu tena kwa theory but practical na kutengeneza movie au muziki wa kimataifa hawajui.
Angalau walimu/wakufunzi waliokuwepo nao wangepelekwa huko Hollywood, Bollywood wakeongeze ujuzi kwa vitendo halafu warudi ili sasa kufundisha kwa kuakisi maisha na mazingira halisi ya mtanzania na mwafrika badala ya kuwaleta mastaa wachache wa marekani kuja kusalimia na kuhutubia siku moja na kisha kwenda kutalii katika mbuga za wanyama kwa kuwagharamia mabilioni ambayo yangetumika kuongezea ujuzi wa walimu wa sanaa na kuongeza vyuo. Wenzetu waliopiga hatua katika sanaa wamewekewa misingi mizuri ya kulinda na kunufaika na kazi zao za kisanaa na pia kuyaingizia mataifa yao pesa nyingi kupitia sanaa tofauti na ilivyo hapa nchini.
Rais Kikwete amewekeza mabilioni ya pesa katika soka la Tanzania but imeshindikana kupiga hatua because hakukuta msingi imara wa soka la Tanzania na yeye pia akasahau na kushindwa kuweka msingi huo kwa kuwaanzisha vyuo na academies za soka tangu watoto na vijana wakiwa wadogo wakulie katika taasisi hizo kama ilivyo kwa wenzetu walioendelea.

Imeandikwa na Trim Saleem

No comments:

Post a Comment

There was an error in this gadget