INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Wednesday, November 4, 2015

Faiza Ally Kuja Na Filamu Ya Baby Mama Drama.

Baada ya kushambuliwa na baadhi ya watu kuhusu malezi ya mtoto wake Sasha, aliyekuwa mke wa zamani wa Sugu, Faiza Ally ameamua kuweka wazi mpango wake wa kuachia filamu iitwayo ‘Baby Mama Drama’.
Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, Faiza ambaye amedai ni mama kijacho, amesema ameamua kufanya filamu hiyo ili kupeleka ujumbe sahihi kwa jamii kuhusu malezi ya mtoto huyo.
“Unajua mimi mama ambaye nimekuwa na drama nyingi toka nipate mtoto. Hii ni historia katika maisha yangu, watu wana-judge muonekano wa mtu ndio malezi. Kwahiyo katika filamu hii mimi nitacheza kama mhusika mkuu pamoja na mwanangu Sasha na baba wa familia atakuwa Gabo,” amesema Faiza.
“Kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula, mipango yote ipo tayari na leo hii naenda kuonana na director ili tuanze kushoot,” ameongeza.
Bongo 5

No comments:

Post a Comment