INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, October 10, 2013

BAADA YA NORA KUACKIKA...SASA AANDAA KIPINDI CHAKE CHA TV ....NDIO FASHION SIKU HIZI BONGO MOVIE KUANZISHA VIPINDI VYA TV!



UHUSIANO wa wasanii wawili wa filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ na Geofrey Kusila umeota mbawa baada ya kumwagana na kila mmoja kuendelea na maisha yake.
Chanzo makini kilicho karibu na wasanii hao kimepenyeza habari kuwa uhusiano wao umevunjika bila kufahamika chanzo.

“Nora na Geofrey wameshaachana na kila mtu ana maisha yake hata kazi hawafanyi tena pamoja, tangu walipoachana Nora anaandaa kipindi chake cha kwenye runinga na hayupo tena na Geofrey,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Nora ili kuujua ukweli, akafunguka:
“Mimi ninafanya kazi zangu mwenyewe na Geofrey kivyake kwa sababu tumeachana na kampuni ambayo tulikuwa ndiyo kwanza tumeianzisha nayo imekufa na baada ya hapo kila mmoja akashika njia yake na kuangalia jinsi gani atakavyofanya kazi hivyo hatupo pamoja tena.”

Source: Vituko vya Mtaa

No comments:

Post a Comment