INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, April 4, 2016

Mkwe Imezingatia Nini Mashabiki Wanataka: Odama

Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Jennifer Kyaka ‘Odama’ ametambulisha ujio wa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la MKWE ambapo ameleza kuwa imezingatia maoni ya mashabiki zake.
Kupitia ukurasa wake mtandaoni, Odama ameandika haya mara baada ya kuweka picha ya kasha la filamu yake hiyo hapo juu.

Ndugu Zangu, Jamaa, Mashabiki, Team Pamoja Na Wapenzi Wa Filamu Nchini Tanzania Leo Ni Siku Maalumu Ya Kutambulisha Cover Na Poster Maalum Inayotambulisha Filamu Yangu Mpya Ya “MKWE” Iliyoandaliwa na Kampuni Ya J-FILM4LIFE Itakayotoka Rasmi Tarehe 18.04.2016. Filamu Hiyo Ni Kwa Ajili Yako Na Kutokana Na Maoni Ya Wengi Nimeiandaa Kwa Umakini Na Katika Mazingira Ambayo Kila Mwanajamii Ataifurahia Kwani Imechunguzwa Na Wahusika Maalum Na Kuhakikisha Kua Inaangaliwa Na Rika Zote Ili Kila Mmoja Atakayeipata Aweze Kupata Kitu Ambacho Roho Yake Inaridhika. Usiikose Pindi Ifikapo Kitaani Kwako. Tag Rafiki Yako Akumbuke Tarehe Hii…. Tag, Share, Repost Kwa Rafiki Zako Ujumbe Huu… Nawapenda Sana.

No comments:

Post a Comment