INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Wednesday, January 28, 2015

DOTNATA AMWAGA CHOZI ‘LOKESHENI’

Stori: Mwandishi wetu/Risasi Mchanganyiko
MKONGWE wa filamu Bongo, Illuminata Posh maarufu kama Dotnata, amesema alitoa machozi wakati akirekodi sinema inayohusu unyanyasaji wanaofanyiwa watoto wadogo, hasa alipobaini ukweli kuwa wanakosa mtetezi hata wa kuweza kuhisi mateso wanayokutana nayo.


Mkongwe wa filamu Bongo, Illuminata Posh 'Dotnata'.

“Watoto wanapata mateso sana kutoka kwa jamii inayowazunguka, wakipoteza wazazi au familia ikifarakana, wanaoumia zaidi ni wao kwani huingia mitaani na kuwa ombaomba, wanajiingiza kwenye wizi, ukahaba na ushoga. Wanafanya haya yote ili wapate mlo tu kwani hawana akili yoyote ya maisha yao ya mbele, jamii inapaswa kubadilika na kujadili vyanzo vya watoto wa mitaani badala ya kufikiri kuhusu misaada katika vituo vyao,” alisema Dotnata.

Filamu iliyomtoa machozi ni C.P.U ambayo yeye ameigiza kama wakala wa kuwauza wasichana kwenye madanguro ikiwahusisha wasanii wengine kama Kulwa Kikumba ‘Dude’, Richard Mshanga ‘Mzee Masinde’, Hashim Kambi ‘Ramsey’, Sauda Simba, Subira Wahure, Steve Sandhu, Nkwabi Juma, Mohamed Funga Funga ‘Mzee Jengua’ Mobby Mpambala na chipukizi kibao.a

No comments:

Post a Comment

There was an error in this gadget