INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Wednesday, January 28, 2015

PROF. LIPUMBA NA BAADHI YA WANACHAMA WAKE WAKAMATWA NA POLISI


Prof. Lipumba akihutubia.

TAARIFA zilizotufikia ni kwamba Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba na wanachama wake wamekamatwa na kupigwa na Jeshi la Polisi.


Wananchi wakiwa eneo la tukio.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeeleza kushtushwa na tukio hilo la kupigwa na kukamatwa Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA Prof. Lipumba.

Uongozi wa juu wa Chadema pamoja na mawakili wa chama hicho wameelekea Kituo Kikuu cha Polisi, Dar kwa ajili ya tukio hilo walilofanyiwa viongozi hao wa CUF na wanachama.


Polisi wakiwatawanya wananchi baada ya kuandamana.

Juhudi za Mtandao huu kumpata Kaimu wa Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Kova, Afande Sirro zinaendelea baada ya kumpigia simu hapo awali na kuomba kupigiwa baadaye kutokana na kikao alichokuwa nacho.

No comments:

Post a Comment