INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Wednesday, January 28, 2015

WILL SMITH, JADA KUSHEREHEKEA MIAKA 20 YA UHUSIANO WAO FEBRUARI 2015Will Smith akiwa na familia yake.

STAA wa filamu Will Smith na mkewe Jada Pinkett wanataraji kusherehekea miaka 20 katika uhusiano wao mbali na kuwa wanandoa hao walisherehekea miaka 17 ya ndoa yao Desemba 31, mwaka jana.


Will Smith na mkewe Jada Pinkett.

Jada mwenye umri wa miaka 43, aliandika katika ukurasa wake wa Facebook kuhusu uhusiano wake na Will huku akielezea matunda ya mahusiano hayo wakiwemo watoto wao
Willow na Jaden Smith na jinsi walivyoweza kudumu katika upendo na kuvumiliana.

Aliandika hivi: Desemba 31, mwaka jana, nilisherehekea miaka 17 ya ndoa. Mwezi Februari mwaka huu nitatimiza miaka 20 tangu nilipoamua kuanza maisha na Will. Nimejifunza kuwa muungano wa watu wawili ni muujiza wa kweli na watoto ndiyo matunda ya muujiza huo.

Kwa jinsi ninavyoendelea kuupanda mlima huu wa upendo na muungano, ninahamasika kuona yote ambayo yeye na mimi tumetengeneza tukiwa kileleni mwa mlima huo. Aliandika Jada katika sehemu ya ujumbe huo.

No comments:

Post a Comment