Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka hivi karibuni amedaiwa kutwangana makonde na mchumba wake aitwaye Maliki Bandawe, chanzo kikidaiwa ni safarisafari za Rose,
Mtoa habari wetu ambaye alishuhudia mtiti huo alisema, tukio la wawili hao ‘kuzibuana’ lilitokea katika baa moja iliyopo pande za Manzese jijini Dar.
Alisema, akiwa maeneo hayo alimuona Rose akishuka kwenye gari kisha kuingia kwenye baa hiyo na kuungana na wenzake ambapo haikufahamika kama walikuwa na kikao au walikuwa ‘wakila bata’ zao tu.
“Baada ya Rose kuingia pale, wakati wanaendelea kupata moja baridi, moja moto ghafla akaingia jamaa mmoja (Malick) na kumfuata Rose ambapo tuliona wakirushiana maneno kabla ya timbwili la aina yake kutokea.
“Yule jamaa alimpiga Rose kwa maelezo kuwa, alimuaga anakwenda kwa ndugu zake Sinza lakini cha ajabu akamuona maeneo hayo, lilitokea varangati, walichapana vibao hadi watu wakawaamulia,” alisema mtoa habari huyo.
Katika kupata ukweli zaidi wa tukio hilo, waandishi wetu walimsaka Malick bila mafanikio lakini Rose alipopatikana alikiri mtiti huo kutokea na kusema aliyempiga ni mchumba wake na ugomvi ni sehemu ya mapenzi.
“Ni kweli tukio hilo lilitokea lakini kaa ukijua kuwa, wivu na ugomvi ni sehemu ya mapenzi, msipogombana wala kuoneana wivu basi hamna mapenzi ya dhati,” alisema Rose.
No comments:
Post a Comment