Jacqueline Wolper (kulia), akipokea cheti cha ushindi kutoka kwa DK. Cheni aliyekuwa jaji mkuu wa shindano hilo. Wolper akiwa ameshikiria cheti chake muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi. Dok. Cheni akiwa kwenye pozi na Wolper juu ya jukwaa. Msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz akiwajibika jukwaani na mnenguaji wake.
Chidy Benz akikamua jukwaani hapo.
Omm Dipoz akizungumza na mashabiki zake jukwaani.
Dogo Asley akiwajibika.
Awali jana mchana hawa ni baadhi ya watoto wakichezeshwa ukumbini hapo.
Watoto hawa wakijiandaa kushindanishwa moja ya mchezo wa kuzungucha rigi kiunoni jana mchana ukumbini hapo.
Mmoja wa watoto waliofika Dar Live mchana akikabidhiwa baiskeli baada ya kuibuka mshindi katika mchezo wa kuruka kamba.
Mchekeshaji maarufu Mtanga, akizungumza na mmoja wa watoto ndani ya Dar Live.
Sehemu ya umati uliyojitokeza ukumbini hapo.
MSANII wa chimbo la filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe, usiku wa kuamkia leo ameibuka kidedea kwenye shindano lililokuwa likiwashirikisha mastaa wa kike Bongo la Ijumaa Sexiest Girl ndani ya Ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.
Wolper amejizolea heshima lukuki na kitita cha sh. milioni 2 ikiwemo na ofa ya kulipiwa saluni kujiremba kwa mwaka mzima. Usiku wa leo pia ndani ya ukumbi huo kulikuwa na burudani kibao kutoka kwa Ommy Dimpoz, Chidy Benz, Dogo Asley, TOT Taarab na michezo kibao ya watoto iliyosindikizwa na shindano la Mkali wa Mic.