INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Saturday, February 22, 2014

WATU WAMUUA MCHEKESHAJI KING MAJUTO ANGALI HAI....HUU HAPA USHAIDI

JAMANI tunaombwa tunapotumiwa messege tujifunze kuisoma mpaka mwisho na sio kusoma juu tu nakuanza kuwapigia watu simu kuwapa habari zisizo za kweli.


Hivi karibuni kumekuwa na uzushi kuwa Msanii nguli wa vichekesho hapa nchini mzee King Majuto eti amefariki, Kwakweli sisi wasanii tulipata tabu sana kwa kupigiwa simu na kuulizwa eti kuna nini kimetokea huko?.. Mzee Majuto yupo?.. Mbona tunasikia kafa? Ukimuuliza mtu nani kakwambia eti nimetumiwa messege?.. Jamani tumechoka na uzushi huu jamani kwanza mzee majuto ni msanii mkubwa haiwezekani akafa ikapita wiki TV na Radio zisitangaze eti messege ndio ziungurume tuuuuuuuu...! tena kibaya zaidi messege yenyewe imetungwa na mtu tu hamna cha filamu ya majuto yenye matukio hayo wala nini.. HEBU cheki upuuzi wenyewe huu hapa chini..





King Majuto

Hamza King Majuto

MTOTO wa Mzee King Majuto ameongea kwa uchungu sana na kwa hasira sana kupitia kitendo hicho cha watu wanaoutumia muda wao kuandaa messege za ajabu za kuwazushia watu kifo aliiambia masainyotambofu kuwa swala la baba yake kuzushiwa kifo kwa kisingizio kwamba matukio hayo ni katika filamu mpya ya King Majuto huo ni uzushu mtupu.

Aliongeza kusema kuwa filamu za Baba yake zilizopo mbioni kutoka niWHY THIS ROOM, CHUNGU KIMOJA, RCO n.k. Hio iliyoandikwa katika messege ya kumzushia Baba yake kifo yeye haitambui kabisa ukweli ndio huo na Mzee Majuto yuko hai na afya nyema anaendelea na shughuli zake za sanaa kama kawaida.
HII HAPA CHINI NI MESSEGE YA MTOTO WA MAJUTO ALIOMTUMIA MWANDISHI WA WEBSITE YA Masai Nyotambofu.




Masainyotambofu