INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Tuesday, September 29, 2015

Picha: Odama Na Mastaa Wenzake Wakiwa Morogoro Kwenye Kampeni Za CCM.

Odama analiendeleza libeneke la kuinadi CCM katika kampeni zinazoendelea yeye na wasanii wenzake wa filamu na muziki. Hizi ni picha wakiwa Morogoro..........

Nikishinda Ubunge Nitastaafu kwanza Mambo Ya Filamu: Frank

Staa mkongwe wa bongo Movies, Mohammed Mwikongwi ‘Frank’ amesema atastaafu fani ya uchezaji wa filamu endapo atashinda kiti cha ubunge cha jimbo la Segerea, Dar es Salaam katika muchaguzi mkuu wa mwezi ujao.

Sunday, September 27, 2015

Njoo Uhudumiwe Na J-Son Production Kwa Huduma Za Kiwango Chenye Ubora Wa Hali Ya Juu.

Ukitaka Picha Nzuri, Video Zenye Quality Ya Hali Ya Juu Na Ubora Ulio Chati… 
Jibu Lako Ni J-SON Production… Tunatoa Huduma Zifuatazo:- Tunapiga Na Ku Edit Picha, Na Video Kwa Ubora Wa Hali Ya Juu Kwenye Send Off, Kitchen Party, Wedding, Komunio, Kipaimara, Filamu Na Hata Matamasha Mbalimbali… 
Ndugu Mteja Wetu Tukikufanyia Kazi Yako Pia Hua Tunatoa Ofa Mbalimbali Ikiwemo Mobile Studio Na Mengine Mengi…

Dr.Cheni Afunguka Kuhusu Madai Ya Kumuoa Lulu.

Tangu wakati ule msanii maarufu wa filamu, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ aamue kupambana kumsaidia Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwenye kesi ya mauaji iliyokuwa inamkabali, yaliibuka madai kuwa wawili hao ni wapenzi lakini leo limeibuka la ndoa, Ijumaa lina kila kitu.
Madai ya uhusiano wa Lulu na Dk. Cheni yamekuwa yakienea chinichini kiasi cha kuwafanya baadhi ya watu kuamini kuwa, huenda lisemwalo lipo na kama halipo laja.

Lowasa Anajua Njaa Zetu Wasanii Akiingia Madarakani Hawezi Kutusahau: Wolper


"Naamini hata kama UKAWA ikachukua nchi kwa navyomuona Baba Lowasa ana moyo wa imani na anaijua dini kwahiyo wewe shabiki wangu uliandika maneno haya ambayo yamenigusa nakuhakikishia kwamba Mh Lowasa ndiyo Rais nahatofanya lolote baya kwa wasanii wanaomtukana kwani pia yeye naamini anajua njaa zetu na pia anajua maneno wanafundishwa kutokana na panic zao,  maana watanzania wengi wamesanuka yani kwakifupi awajashituka wamesanuka kila mtu anataka mabadiliko na mabadiliko lazima yafanyike..Kwahyo usijali wala usiwaze nitabaki kuwa mtetezi wamaskini wenzangu paka dakika ya mwisho.

Naomba tena nirudie nanitengue kauli ukawa ikiingia madarakani aitomuonea msanii aliyedanganyika kwenda CCM kamwe itakua niwakati wawao kujutia nakutubu Ameni..." Wolper alimjibu shabiki mmoja aliyecomment kama Lowasa akiingia madarakani anaweza kuwabagua wasanii waliotimkia CCM

Wema Sepetu Amtaja mwanaume Atakayeanzisha Nae Familia, Asema Hana Uswahili Kama Kina ......

BAADA ya kupita ukimya mrefu bila kuzungumzia mapenzi, mrembo asiyepoteza ubora wake, Wema Sepetu ‘Madam’ amemtaja mwanaume anayetarajia kumzalia mtoto kuwa ni Luis Munana, raia wa Namibia.
Wema alifunguka hayo juzikati mara baada ya mwandishi wetu kutaka kujua ana mpango gani kwenye ulimwengu wa ‘malovee’ ndipo alipomwanika Luis kuwa ndiye mwanaume pekee ambaye ameshafikia hatua ya kumuamini na yuko tayari kuzaa naye kwa namna yoyote licha ya kujua ana tatizo la uzazi.

Sunday, September 20, 2015

Kijue Kilichomfanya Riyama Ally Kuishia Kidato Cha Pili.

Staa wa Filamu Bongo, Riyama Ally ameweka wazi kuwa hakumaliza elimu ya sekondari kutokana na ugumu wa masomo kwani hakuwa akiambulia chochote darasani licha ya walimu kujitahidi kufundisha kwa kiwango cha juu.

Gabo Zigamba Amesema Hiki Kufuatia Baadhi Ya Wasanii Kuwa Busy Na Kampeni Za Siasa.

Mcheza filamu Salim Ahmed ‘Gabo’ amesema sanaa haitakufa  licha la wimbi la wasanii wake  kujikita katika maswala ya siasa kwa sasa, kwasababau wapo ambao wameamua kuiendeleza kwa kwenda mbele.

Wolper Asema Hiki Baada Ya Kushindwa Kuhudhuria Maulidi Ya Mtoto Wa Diamond Na Zari.

"40 ya Tiffah Lee Queen Asante bwana Demonde kwa mualiko ..ila ulivyomswahilI kila mualiko nakua nakamtoko au nakua sipo kabisa Dar sasa kivumbi pale kwenye harusi yangu ule mualiko sasa utakavyojisafirisha ili kunilipizia usifanye hvyo mambo yanaingiliana..lol ...hongera sana Naseeb najua furaha uliyonayo Mungu kukuzia Tiffah wako...coz ilikua ni ndoto katika maisha yako kua na mtoto kikubwa Mungu akusimamia kwenye sherehe kuna Mambo mengi so nakuombea uanze salama na umalize salama nawale wageni waalikwa wakose chakukosoa maana tunajijuaga@diamondplatnumz usisahau kutoroka bado ujachelewa"
Jacqueline Wolper “@wolperstylish on Instagram

Picha Toka 40 "Maulidi" Ya Mtoto Wa Diamond Na Zari....Tiffah Dangote

Sura ya mtoto wa Diamond na Zari, Tiffah Dangote imeonyeshwa rasmi leo na kulikuwa na maulidi ya kutimiza siku 40. Hizi ni9 baadhi ya picha.......

Thursday, September 17, 2015

Odama Asema Yeye Si Wa Kuchezewa Hovyo Hovyo.

Jennifer Kyaka ‘Odama’ amesema miongoni mwa mambo ambayo kamwe hayafanyii mzaha ni pamoja na kuruhusu mwili wake ‘uguswe’ kwa urahisi na wanaume wakware.
‘Akibananishwa ukutani’ na ‘kisabengo’ wetu kwa maswali magumu juu ya kutoonekana hadharani au kumwanika mwandani wake hivi karibuni, Odama alisema yeye ni mwanamke thabiti aliyelelewa katika maadili halisi ya kiafrika, hivyo suala la kuwa na mwanaume halihitaji ‘promo’ kwani ni kawaida kwa mtu mzima aliyekamilika kuwa na mwenzi, huku akiweka bayana kuwa mwili wake si sadaka hivyo haguswi kirahisi.

Ray Asema Ushindani Kwenye Filamu Hakuna Baada Ya Kifo Cha Kanumba.

Msanii mkongwe wa filamu nchini, Vicent Kigosi ‘Ray’ amesema baada ya kufariki Steven Kanumba tasnia ya filamu imekosa ushindani wa ndani na nje.
Akizungumza kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV, Ray alisema kazi yake na maisha yake vimetikisika kutokana na kukosa mshindani kama alivyokuwa Kanumba.

Tuesday, September 15, 2015

Picha: Odama Ndani Ya Mtwara .

Odama na wasanii wengine wapo Mtwara katika kupigia chapuo kampeni za CCM. Hapa akiwa hotelini walipofikia...

Ray Kutoa Tamko Kuhusu Tetesi Za Kuhamia CCM Toka UKAWA.

Kufuatia tetesi kuenea mtandaoni kuwa staa wa Bongo Moveis , Vicent Kigosi ‘Ray ‘ amehama UKAWA “team mabadiliko” na kwenda upande wa CCM., Ray amepanga kuvunja ukimya na kutoa tamko lake rasmi juu ya swala hilo.

Irene Uwoya Asikitishwa Na Wasanii Wasioiunga Mkono CCM.

"Sasa narudi kwa wasaniii wasio jitambua!katika tasnia yetu ukweli usio pingika Mh.Kikwete amekuwa karibu Sana na wasaniii na ametufanya tudhaminike.

Shamsa Ford: Nipo Tayari Kupata Mtoto Mwingine Na Nay Wa Mitego.

Shamsa Ford amesema kuwa yupo tayari kuzaa mtoto mwingine na mpenzi wake wa sasa mwanamuziki Nay Wa Mitego. Shamsa aliyasema hayo wakati akizungumza na jarida la habari za mastaa BaabKubwa magazine.

Jokate: Bado Sijaona Wa Kumwamini Kimapenzi.

LICHA ya kuzagaa kwa tetesi juu ya uhusiano wake na msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba, mwanamitindo Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amesema kutokana na kuumizwa na mapenzi mara kwa mara, kwa sasa hajaona mwanaume wa kumuamini hivyo anaelekeza nguvu na akili zake kwenye kazi.

Picha: Odama, Wenma Sepetu, Thea, Wastara, Steve Nyerere Katika Kampeni Za CCM Lindi.

Kama kawaida Odama na wasanii wengine wenye majina wapo busy kuipigia debe CCM katika kampeni zao. hapa wakiwa mkoani Lindi.....

Saturday, September 12, 2015

Mimi Si Mgeni Wa Mapenzi : Diana Kimaro

Msanii wa filamu Bongo, Diana Kimari ameanika ukweli wa moyoni kuwa, alianza kujihusisha na mambo ya mapenzi akiwa anasoma shule ya msingi.

Kitale: Jina Linalonogesha EFM.

Pengine kituo cha redio cha eFM ndio habari ya mjini kwa sasa. Kwenye daladala, vijiweni, sokoni na kwenye baa nyakati za asubuhi, lazima ukute watu wanasikiliza redio hiyo ambayo imeanza kwa nguvu mwaka huu kwa kuajiri watangazaji maarufu kutoka vituo mbalimbali vya redio nchini.
Lakini kivutio kikubwa na matangazo yake yanayowekwa kwa ajili ya kuitangaza redio hiyo.
Ndani ya matangazo hayo yumo Mkude Simba, ambaye vichekesho anavyobuni huwavunja mbavu wengi.

Picha: Odama Katika Kampeni Za CCM Chalinze, Bagamoya Na Mastaa Wengine.

Odama na wasanii wengine wenye majina makubwa kama Wema Sepetu, Bi.Mwenda, Batuli, Snura, Davina, Chuchu Hans, Mama Kibakuli, Bi.Stara, Nyamayao, Chuchu Hans, Thea, Wellu Sengo, Wastara , Ali Choki, Steve Nyerere na wengineo wapo katika kundi la wasanii wanaoiunga mkono CCM irudi madarakani. Hizi ni picha za kampeni walizofanya huko Chalinze na Bagamoyo mkoani Pwani..

Wednesday, September 9, 2015

Ray Awaonya Wasanii Kutokubali Kutumika Kisiasa.

"(FREEDOM OF SPEECH)
"Kuna vitu vingi sana nimegunduakwenye uchaguzi wa mwaka huu nimewajua baadhi ya wasanii waliokuwa na akili na wasiokuwa na akili japokuwa nami nawezakuwa mmoja wapo katika hao wasiokuwa na akili. Why nasema hivi na samahani kama nitakuwa nime2mia lugha kali, Unajua nashanga sana sasa hivi kumekuwa na vita baina ya wasanii wanaosapoti (CCM) Na (UKAWA)

Kingwendu Awasha Moto Katika Kampeni Zake Za Ubunge Huko Kisarawe.

Hizi ni baadhi ya picha za msanii wa filamu za vichekesho nchini, Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’ ambaye ni mgembea ubunge  jimbo la Kisarawe kupitia tiketi ya  chama cha wananchi CUF  alipokuwa akinadiwa na mgombea mwenza wa  urasi kupitia CHADEMA, Juma Duni Haji hivi karibuni.

BASATA Wasema Adhabu Y Shilole Ipo Palepale.

Shilole anaweza akawa anafurahia bata za Marekani baada ya kutumbuiza kwenye show nchini humo, lakini bado BASATA haijamalizana naye.
Katibu Mtendaji wa baraza la sanaa la taifa, BASATA, Geofrey Mngereza ameiambia Radio 5 ya Arusha kuwa adhabu aliyopewa Shilole ya kufungiwa kutojihusisha kwenye masuala ya sanaa kwa mwaka mmoja haijafutwa.

Picha Mbalimbali Odama Na Mastaa Wengine Wakiwa Katika Kampeni Za CCM.

Star mkubwa wa filamu nchini Odama Jennifer Kyaka pamoja na wasanii wenzake wengine wamekuwa katika kampeni za CCM mikoa mbalimbali nchini. Hizi ni baadhi ya picha..

Wednesday, September 2, 2015

Ningekuwa Mjamzito Ningeweka Wazi Haina Haja Ya Kuficha: Wolper

MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Jacqueline Walper ‘Wolper amecharuka vibaya mara baada ya kuulizwa habari za ujauzito.

Ningetaka Kuzaa Mtoto Mweupe Ningezaa Na Mzungu: Aunty Ezekiel

MSANII wa Bongo Movie anayetambulika kwa jina la Aunty Ezekiel amewajia juu mashabiki wake wanaomuongelea vibaya mtoto aliyezaa na mnenguaji wa Diamond Platnumz, Mozee Iyobo.

PICHA: Muonekano Wa Odama Kwenda Kwenye Kampeni Ya CCM Ya Mama Ongea Na Mwanao.

Odama alitokelezea hivi katika uzinduzi wa kampeni ya CCM ya Mama Ongea Na Mwanao.......