CREW
2015 Calendar
FILMS
FILMS 2
ADVERTS
INSIDE INAPATIKANA MADUKANI
FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015
JADA IPO SOKONI
Saturday, October 31, 2015
Davina Ahamasika Kugombea Ubunge Uchaguzi Ujao.
HALIMA Yahya ‘Davina’ amehamasika na mambo ya kisiasa hivyo, kujiandaa kwa kujifua vyema kwa ajili ya msimu ujao wa uchaguzi (2020).
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Davina ambaye ni msanii wa filamu Bongo, alisema kufuatia kupata fursa ya kushiriki kampeni kwa nafasi yake, maeneo mbalimbali ya nchi, amejikuta akishawishika kuwa kiongozi na kwamba baada ya miaka mitano, endapo Mungu atamjaalia uzima, atagombea nafasi ya ubunge, mkoani Iringa.
Saturday, October 24, 2015
Kifo Cha Deo Filikunjombe Kimenihuzunisha Sana: Cathy Rupia
Muigizaji wa muda mrefu, Sabrina Rupia ‘Cath wa Mambo Hayo’, amekiri kuumia vibaya kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe kutokana na ukaribu wao na jinsi alivyokuwa na moyo wa kuwajali wengine.
Akizungumza kwa uchungu na mwandishi wetu kwa njia ya simu kutoka Ludewa alikohudhuria mazishi ya mbunge huyo, Cath alisema maumivu aliyonayo kamwe hayasimuliki na kwamba itamchukua muda mrefu kumsahau Deo na kwamba ataendelea kumuombea kwa Mungu, ampumzishe kwa amani.
Thursday, October 22, 2015
Natamani Sana Kupata Mtoto: Jackie Pentezel
Msomaji: Mbali na sanaa unafanya shughuli gani?
Jack Chuz: Nina saluni yangu Sinza na duka la nguo. Pia ni mtaalam wa kusuka na make up.
Msomaji: Nasikia bila ndumba huwezi kukubalika kwenye sanaa, unaliongeleaje hilo?
Jack Chuz: Si kweli, uzuri wa kazi zako ndiyo uchawi wako.
Msomaji: Mumeo (Gadner) ni Muislam na dini inamruhusu wake wanne akitaka kuoa tena utafanyaje?
Tuesday, October 20, 2015
Lugha Ya Kiingereza Ni Tatizo Kwa Wanafunzi: Jokate
Miss Tanzania namba mbili 2006 na mmiliki wa kampuni ya ‘Kidoti’, Jokate Mwegelo aka Jojo, siku chache zilizopita alifanya ziara yake katika shule za secondari jiijini Dar es Salaam kama Jangwani, Azania, Benjamini Mkapa nk na kupokelewa vizuri na Waalimu pamoja na Wanafunzi. Je ziara yako ilifanikiwa kwa kiasi gani na changamoto ipi umeiona kwa wanafunzi?
Rayuu Asema Maisha Yake Mitandaoni Ni Tofauti Na Nyumbani.
Mrembo anayetikisa kiwanda cha filamu nchini, Rahma Rayuu ‘Rayuu’ amesema maisha yake halisi na maisha anayoonyesha kwenye mitandao ya kijamii ni tofauti hivyo watu wanaodhani ndivyo alivyo wanakosea.
Friday, October 16, 2015
Wanaume Hukimbia Nikiwatajia Suala La Ndoa: Nora
MSANII wa Filamu za Bongo, Nuru Nasoro ‘Nora’ amefunguka kwamba wanaume wengi wanaomtaka kimapenzi humkimbia anapowataka wasubiri hadi watakapofunga ndoa.
Nora alisema ameweka sharti hilo ili ampate mwanamume wa kweli, lakini anaona kama amejiwekea gundu kwa kuwa wengi waliojitokeza kwake hukimbia anapowaeleza masuala ya kusubiri hadi ndoa.
Monday, October 12, 2015
Kayumba Ajinyakulia Mil.60 Za Bongo Star Search.
Shindano la kusaka vipaji vya waimbaji wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Star Search limemalizika huko kijana mdogo toka Temeke Kayumba Juma akijinyakulia zawadi ya kitita cha Tsh.Mil.60. Shindano hilo lilikuwa na ushindani mkali akiwemo Naseeb Fonabo toka Arusha aliyeshika nafasi ya pili ambapo yeye na Kayumba walionyesha uwezo mkubwa tangu awali.
Thursday, October 8, 2015
Shamsa Ford Amuacha Mtoto Kwa Bibi Yake Ili Kufanya Kampeni
MTOTO wa staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford aitwaye Terry, analelewa na mama yake mzazi wakati yeye akiwa bize na kampeni kuelekea uchaguzi mkuu.
Shamsa akithibitisha jambo hilo, aliliambia gazeti hili kuwa amelazimika kumuacha mwanaye kwa bibi yake ili aende na kasi ya kampeni, lakini hujitahidi kuzungumza naye kwa simu kila siku ili kumfanya ajisikie vizuri.
Bonge La Nyau Adatishwa Na Uzuri Wa Irene Paul.
Urembo na uchapakazi wa mwanadada anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu, Irene Paul umemdatisha msanii wa muziki, Bonge La Nyau aka Nyauloso.
Nyauloso ameiambia Nje ya Box ya kipindi cha Planet Bongo cha EATV, kuwa anatadishwa mno na miondoko ya mwanadada huyo.
Tuesday, October 6, 2015
Filamu Zinalipa Kuliko Siasa
MKURUGENZI wa Jerusalem Film Company, Jacob Stephen ‘JB’ ameweka wazi kuwa kamwe hafikirii kuwa mwanasiasa kwani sanaa inamlipa zaidi.
Akizungumza na mwanahabari wetu katika mahojiano mafupi, JB alisema kipindi cha nyuma ziliibuka tetesi kuwa huenda anaweza kuwa mwanasiasa lakini ukweli kutoka moyoni, sanaa inamlipa.
Honeymoon Aljabri Afanya Filamu Nchini Marekani.
MWONGOZAJI bora wa filamu mwenye tuzo ya ZIFF 2015, Honeymoon Aljabri, yupo mbioni kukamilisha filamu yake ya pili ya ‘Forgotten Hero’ mwishoni mwa mwaka huu.
Mwongozaji huyo Mtanzania anayeishi Houston, Marekani, aliliambia MTANZANIA kwamba ameandika na kuiongoza filamu yake hiyo nchini Marekani, huku akidai kwamba ujumbe katika filamu hiyo unaonyesha uhusiano wa wapendanao ambao mmoja wao aliwahi kushiriki vita.
Sikia Point Ya Hemedy Kwa Wasanii Juu Ya Uchaguzi Mkuu.
Hemed Suleiman ‘Phd’ ametoa rai kwa masanii wengazke kutoa elimu juu ya upigaji kura katika Uchaguzi Mkuu wa badaye mwezi huu badala ya wenyewe kuwa mashabiki wa vyama.
Subscribe to:
Posts (Atom)