INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, December 28, 2015

Picha: Diamond, Zari, AY, Esma, Queen Darleen Wakifurahia Holiday Ufukweni.

Zari, Diamond, Queen Darleen, Esma Platnumz na management ya Diamond waliamua kufanya mapumziko ya holiday katika ufukwe wa bahari ya hindi huku pia wakipanda yatch

Odama, AY Na Bob Junior Kukinukisha Kesho.

Odama atakuwa na special appearance katika party itakayofanyika kesho ukumbi wa Rhapsodys..

Nazingatia Ubora Wa Filamu Kwanza Pesa Baadaye. : JB

‘’Wakati mwingine nakuwa kama kichaa nikitengeneza movie zangu siangalii namna ambavyo nitapata faida kubwa,naangalia jinsi ambavyo naweza kutengeneza kitu kizuri,naaamini katika maisha kuacha historia bora kuliko kitu chochote,hadi sasa nimeshatengeneza zaidi ya filamu 37 kutoka kwenye kampuni yangu ya Jerusalem,’’alisema JB.
‘’Pesa Napata lakini kumbukumbu yangu ni filamu zile ambazo watu wameangalia wakikuona na kukuita yale majina kama Erik Ford,Dj Ben,Danija,Mzee wa Swaga ndiyo majina yanayobaki kuwa kumbukumbu kwa sababu waliona nilichokifanya,sitajali nimetumia mill.100 au mia mbili kwenye local movies hata kama haitorudi ili mradi filamu iwe nzuri,’’alisema JB.
Cloudsfm.com

Jokate Na Wema Katika Show Ya Ali Kiba.

Juzi Ali Kiba Alikuwa na show ya kuwaaga mashabiki wake kwa kumaliza mwaka vziuri katika ukumbi wa Escape One Mikocheni. Miongoni mwa walihudhuria hiyo show ni Wema Sepetu na Jokate. Angalia picha ..

Sunday, December 27, 2015

Mama Lulu Agoma Lulu Kuondoka Nyumbani.

Marufuku! Mama mzazi wa staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila ametia ngumu mwanaye huyo kuondoka nyumbani kwake na kwenda kuishi peke yake kwa kuwa bado anahitaji zaidi kufuata maadili yake.

Riyama Ally Na Flora Mvungi Wakabana Koo Kukata Nyonga.

STAA wa filamu Bongo, Flora Mvungi na shostito wake, Riyama Ally juzikati walijikuta wakigeuka kivutio ukumbini baada ya kufunikana kwa kuzikata nyonga bila aibu kwenye hafla ya kumpongeza mtoto wa Flora, Tanzanite Hamis kuchaguliwa kuwa balozi wa duka la kuuza nguo.

Zamaradi Mketema Kumuingiza Mama Diamond Bongo Movie.

Kufuatia uwezo mkubwa aliouonyesha Mama mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinum, Sanura Kasim kwenye kipande cha video ya wimbo mpya wa diamond , utanimpenda ambapo mama huyo ameigiza kwa kuuvaa uhusika wa mama mwenye maisha magumu ambaye anatafuta msaada akiwa na mtoto mgongoni kitu ambacho kimeshika hisia za watazamaji wengi na wengi kumuona kama ni mama mwenye uwezo mkubwa wakuigiza, mmoja wapo ni mtangazaji na muuandaaji wa filamu hapa Bongo, Zamaradi Mtetema ambaye amekiona kipaji cha mama huyu na kuahidi kumtafuta ili wafanye kazi.

Lady Jaydee Ahamia Ujerumani ?

MOYONI nina majonzi, sina tofauti na mpofu! Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ au ‘Lady Jaydee’ kwa sasa hana makazi maalum Bongo, amehamishia makazi na shughuli zake katika ardhi ya ‘Kansela’ wa Ujerumani, Angelina Merkel kwenye Jiji la Born.
Katika mazungumzo yake na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Jumatatu ya wiki hii, Jide ambaye alidai kwa sasa yupo nchini kwa Sikukuu ya Krismasi (kesho), alisema sababu zilizomfanya akapige kambi nchini humo ni kuchoshwa na maneno ya watu ambao kazi zao ni kutazama nani kafikwa na baya ili waeneze sumu ya maneno.

Tuesday, December 22, 2015

Wema Sepetu Kuonekana Akipika Mahanjumati Wiki Hii.

“This week ntakua Jikoni na my Dada Marion- Alhamis 24th December at 7pm Dstv Maisha Magic Bongo (Channel 160). An Exclusive Interview and Cooking section”-Wema ameandika kwenye ukurasa wake mtandaoni baada ya kutupia picha hizi akiwa jikoni.

Aunty Ezekiel Na Moze Iyobo Kupata Mtoto Mwingine.

Staa maarufu wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel amefungua kinywa chake na kusema kuwa kwa sasa yuko kwenye mchakato wa kumtafuta mdogo wake na Cookie kwa kuwa hataki kukaa muda mrefu ili kupata mtoto mwingine.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni Aunty,alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kwa kuwa anaona kuzaa mapema na kumaliza ndiyo poa ili aweze kuendelea na kazi zake vizuri kuliko kukaa muda mrefu halafu ndiyo ubebe ujauzito tena.

TANESCO Wataja Gharama Wanazomdai Wema Sepetu.

Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limemkaba koo staa maarufu wa Bongo Movies , Wema Sepetu baada ya kubainika kutumia nishati ya umeme kwa njia zisizo halali.
Hivi karibuni TANESCO walifanya ziara ya kushtukiza kwenye nyumba yake na kubaini kuwa muigizaji huyo anatumia umeme wao bure!

Wasanii Wajitokeza Kugombea Nafasi Za Uongozi.

MCHUANO mkali katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya mwenyekiti wa chama cha waigizaji Taifa (TDFAA) huku wasanii wenye ushawishi kwa wasanii wenzao wakijitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo anasema katibu Twiza.
Jimmy Mafufu akichukua fomu ya kugombea kutoka kwa katibu wa TDFAA Twiza Mbarouk .
Jimmy Mafufu akichukua fomu ya kugombea kutoka kwa katibu wa TDFAA Twiza Mbarouk .
“Mchuano ni mkali kila mhusika amepanga kuwa ni mshindi katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya uenyekiti Kitaifa kwa chama cha Waigizaji, hadi sasa ni zaidi ya wasanii wane wameshachukua fomu za kugombea,”anasema Twiza.

Wasanii Tufanye Na Biashara Nyingine Tujikwamue Kiuchumi: Ire Uwoya

MKALI wa filamu nchini, Irene Uwoya, amewataka wasanii wenzake hasa wanawake kujituma katika kazi nyingine kama vile biashara ili kuweza kujikomboa kiuchumi
Irene amesema wasanii wengi wanategemea sanaa ili kuweza kuendesha maisha yao, lakini wanatakiwa kufanya mambo mengi ili kuweza kujiingizia kipato.

Lulu Haishi Vituko, Angalia Alichoandika.

Hapa na Pale: Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao picha wa Instagram staa mrembo wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amewaacha watu hoi baada ya kubandika picha hiyo hapo chini ikimuonyesha yeye na baba yake mzazi ‘Mzee Michael’ na kummwagia sifa baba yake huku akiomba dua aje kuzaa mtoto atakaye fanana na baba yake (Mzee Michael) kitendo ambacho kila shabiki yake mtandaoni alikuwa na yake ya kusema.

Friday, December 18, 2015

Picha Kutoka Birthday Ya Faiza Ally.

Jana ilikuwa birthday ya Faiza Ally ambayo ilihudhuriwa na mastaa kadhaa wa filamu nchini. Faiza pia alivaa gauni la harusi na shela. Hizi ni picha...

Chungu Cha 3 Ya Wema Sepetu Na JB Yapokelewa Vizuri Sokoni.

“Kwanza nawashukuru sana sana kwa kuipokea vyema filamu ya Chungu cha tatu. …pili nawaomba radhi wote ambao jana walikosa nakala zao kwani iliisha tena…lakini leo ipo madukani baada ya mimi mwenyewe kukesha kiwandani nikihakikisha oda zote watu wanapata..mikoani pia sehemu ambazo ziliisha leo zipo…nimepata habari za watu wanaouza feki tayari baadhi yao wako ndani…asanteni..” alisema JB kwenye page yake. Filamu ya Chungu Cha Tatu imechezwa na JB na Wema Sepetu kama wahusika wakuu

Picha Kutoka Zari All White Party 2015 Nchini Uganda.

Zari All White Party nchini Uganda imefanyika jana, Ingawa Diamond alikuwa Uganda pia hakuweza kuhudhuria kutokana na kuwa na show pia. Ila aliyewahi kuwa mume wa Zari yaani Ivan Semwanga alihudhuria. hizi ni picha..
Zari All White Ciroc Party
Zari All White Ciroc Party

Tuesday, December 15, 2015

Shamsa Ford Awatolea Uvivu Waliomnanga Kwa Kuvaa Nguo Fuoi.

"Maisha yangu hayawahusu. Ukiona hufulahishwi na chochote toka kwangu ni unfollow. Hukulazimishwa kunifollow. Yaani kuniona kwenye movie ndo mnajifanya mnanijua mpaka mnipangie maisha ya kuishi.sikilizeni nitavaa nitavyojisikia mm hata nikiamua kukaa uchi kabisaa ni mm na wala hayakuhusu. Ww subili movie Itoke ndo unikosoe. Mnaboa sana. Hebu walekebisheni ndugu zenu wanaovaa madila mchana usiku ni vyangudoa..." ameandika Shamsa Ford baada ya baadhi ya watu kumtukana kwa nguo fupi aliyoivaa akiwa beach na mwanae......

Monday, December 14, 2015

Lulu, Monalisa, Richie Wachaguliwa Tuzo Za Africa magic Viewer's Choice Awards 2016.

Filamu 4 za kitanzania zimechaguliwa katika katika tuzo za Africa Magic Viewers Choice Awards 2016 zitakazofanyika nchini Nigeria mwezi wa tatu. Filamu hizo ni Kitendawili iliyoigizwa Single Mtambalike Richie na Irene Veda, Mapenzi Ya Mungu iliyoigizwa na Lulu, Daddy's Wedding iliyoigizwa na Monalisa na Mpango Mbaya zote zikiwania best East African Film. Huku Kitendawili pia ikichaguliwa kuwania best Indigenous Film(Swahili). Ili kuwapigia kura wasanii hawa angalia maelezo hapo chini....

Kingwendu Apata Deal La Uigizaji Nchini Ujerumani.

Msanii maarufu wa vichekesho na maigizo nchini Kingwendu siku chache zilizopita ameenda nchini Ujerumani kwa ajili ya masuala ya uigizaji. Kingwendu ambaye aligombea ubunge hivi karibuni na kuukosa kabala hajaondoka alisema kuwa mwaka ujao wameamua wasanii wa vichekesho waitangaze tasnia ya filamu kimataifa baada ya waigizaji serious kushindwa kuiendeleza alipoishia Kanumba.

Tuesday, December 8, 2015

Shaa Na Vanessa Mdee Wakerwa na Baadhi Ya Mashabiki Kuwalinganisha Na Kuwashindanisha

Mastaa wa muziki wa kisazi kipya Vanessa Mdee na Shaa kwa nyakati tofauti wakizungumza katika kipindi cha Planet Bongo wameonekana kukerwa na baadhi ya mashabiki kuwashindanisha wao kwa wao wakisema kuwa sio vizuri kwasababu inaleta uhasama baina ya wasanii wa ndani wakati kila mmoja ana nafasi na mchango wake katika sanaa ya Tanzania. Shaa alisema ni heri mashabiki wawashindanishe na wasanii wa nje maana wasanii wa ndani kwa ndani haileti maana

Wema Sepetu Kufanya Makubwa Zaidi.

"I think This should be my Colour ya Lipstick wen it comes to my Brand Kiss..... Naipenda coz it jus makes me feel good nikiipaka.... For a very long time nimekuwa nikitaka sana kuwa na kitu kitacho carry jina langu la Wema Sepetu... I thought of perfume at first ila huko nikahisi ni parefu sana but inshallah hakunaga kubwa ukimtanguliza Mungu katika jambo lako na haswa likiwa jambo la kheri.... but sababu napenda urembo nikawaza nifanye kitu kiatakacho reflect kwenye urembo na wazo la kwanza lililonijia katika kichwa ni My Kissable Lips..... 🙈🙊 So hapo hapo nikasema Why nat make a Lipstick kuzifanya kissable lips zangu zizidi kuvutia na ziweze kuwafanya na my fellow sisters pia wawe na muonekano mzuri..... Tumeanza na Lipstick jamani... Mdogo mdogo ndo mwendo.... Inshallah kale ka makeup box ketu ambacho wadada hatukosagi kwenye handbag zetu katakuwa na virutubisho vyote vya uso wako kwanzia foundation mpaka wanja vikiwa na jina la your sweetheart Wema Sepetu..... Tuombeane Kheri and like I said hakunaga kubwa kwa Allah.." Ameandika Wema kwenye instagram

Tanesco Wagundua Wizi Wa Umeme Nyumbani Kwa Wema Sepetu, Idris Sultan Ndani Ya Nyumba

Katika Pitapita zao leo kufanya majukumu yao ya kikazi Tanesco walipita mitaa ya Makumbusho kukagua nyumba ikiwemo ya Wema Sepetu ambapo habari zinasema kuwa Tanesco walikuta kuwa umeme unatumika lakini hausomi kwenye mita yaani haulipiwi. Pia Idris Sultan ambaye ni mtu wa karibu na Wema alikuwa ndani ya nyumba akijaribu kuwasihi Tanesco wasikate umeme. Wema Bado kuzungumzia suala hilo. Picha hapo chini ni Idris akiwa nyumbani kwa Wema wakati Tanesco wakifanya yao ambapo pia waandishi wa habari walikuwepo.

Odama Aingia Mzigoni Kushuti Filamu Mpya.

Star wa filamu nchini Odama Jennifer Kyaka ameingia location tayari kuanza kushuti filamu yake mpya baada ya kimya cha muda kidogo.

Quick Racka Akiri Kuwa Katika Penzi Na Kajala

Msanii wa BongoFlava Quick Racka amekiri kuwa na uhusiano na Kajala Masanja licha ya huko nyuma wote kutokuwa tayari kuzungumzia uvumi huo ambao ulichukuwa headline za magazeti. Hata hivyo akizungumza na Clouds Fm Quick Racka aliulizwa kama swali flani la kimitego hivi kuwa ni kweli wameachana na Kajala na ndipo alipojibu kuwa bado wapo pamoja ila hawapendi maisha yao binafsi kuwa katika magazeti kila siku. Quick Racka pia anadaiwa kuwa na tatto yenye jina la Kajala.

Monday, December 7, 2015

Napoleon Asema Lulu Na Wema Sepetu Wana Sifa Za Kufanya Vizuri Hata Hollywood.

Star wa filamu ya Going Bongo inayoendelea kufanya vizuri kimataifa Ernest Napoleon amewataja waigizaji wa Kitanzania Lulu Elizabeth Michael na Wema Sepetu kuwa wana sifa za kufanya vizuri hata Hollywood kama wakipata nafasi na kuwa na management nzuri. Ernest akizungumza na Bongo5 amesema kuwa wengi wanaziponda filamu za Bongo lakini ubovu wa filamu unaweza kusababisha na production mbaya au filamu kutengenezwa ndani ya muda mfupi kwa kuharakishwa lakini suala la uigizaji wa msanii ni kitu kingine.

Sunday, December 6, 2015

Omary Clayton, Timoth Conrad, Filamu Ya Dogo Masai Watamba California Viewers Choice Awards 2015.

Ninaitwa Timoth Conrad Kachumia Director, Producer na Writer wa filamu Tanzania, Ninayofuraha kuwajulisha watanzania kuwa nimefanikiwa kushinda California Viewers Choice Awards 2015, tuzo 2 ikiwa ni Best Feature Film pamoja na Best Director kupitia filamu ya DOGO MASAI, vile vile kutoka katika filamu hiyo hiyo Omary Clayton ambaye ni muigizaji mkuu amefanikiwa kushinda tuzo ya Best Actor.

Saturday, December 5, 2015

Filamu Ya Going Bongo Kuanza Kuonyeshwa Katika Majumba Ya Sinema Nchini Wiki Ijayo.

Filamu ya Kitanzania na ya kimataifa Going Bongo inatarajiwa kuanza kuonyeshwa rasmi kwenye majumba ya sinema nchi kuanzia tarehe 11 mwezi huu wa December. Filamu hiyo iliyochezwa na Ernest Napoleon, Mzee Chilo na wasanii wengine wa kizungu toka mataifa mengine tayari imeshajizolea tuzo katika matamasha kadhaa ya kimataifa na ilianza kuuzwa exclusively katika iTune.